Tripper
JF-Expert Member
- Nov 15, 2020
- 727
- 1,308
Hao uliowataja kipind kile walikuwa wanateka watu kwa sababu gani?
Na Sasa wanaendelea kuteka kwa sababu gani?
Na Sasa wanaendelea kuteka kwa sababu gani?
Mfumo wowote ulioasisiwa, ukishasimama na ukajizatiti, kamwe hauwezi kupotea au kuondoka mara moja.
Tukumbuke wakati wa Magufuli, siyo Magufuli aliyekuwa akiteka au akiua kwa mkono wake, bali aliuimarisha na kuupa nguvu mfumo uliokuwa ukiteka, kupoteza na kuteka watu (naamini kuwa huo mfumo hakuasisi yeye, ulikuwepo hata kabla yake). Hii ina maana kuna watu waliajiriwa na kazi yao ilikuwa ni kuteka, kupoteza na kuua watu.
Wengi wa hawa wauaji na watekaji, baada ya kuteka na kuua sana, wakati wa marehemu, walipandishwa vyeo. Hawa watu bado wapo, na wengi wao wanashikilia ofisi zile zile au za juu zaidi, huku wakijua kuwa ni utekaji na uuaji ndivyo vilivyowapandisha mpaka kufika walipo sasa. Akina Kingai, Goodluck, Mahita, Jumanne , etc, mnawaona wakiendelea kwenye ofisi za umma, tena wakiwa na madaraka makubwa zaidi. Kama kazi zao ndizo hizo, na bado wapo maofisini, mnafikiri wanafanya nini?