Rais Samia, haya mambo ya kupotea watu ni doa kwenye serikali yako

field marshall1

JF-Expert Member
Sep 17, 2017
1,171
2,730
Mheshimiwa Rais, naomba nichukue nafasi hii nikupongeze kwa mambo mengi mazuri unayoyafanya ila kwa hili la watu kuanza kupotea kwenye utawala wako tayari ni doa kwenye serikali yako. Wiki mbili zilizopita kuna habari zimetokea magazeti kuwa kuna vijana watano wamepotea wakiwa wanaenda kusherekea Krismasi kwenye fukwe hapa Dar es Salaam.

Kwa maelezo yao ni kuwa walikamatwa na Police na wakawa wanapelekwa central police, baada ya hapo hawakusikika tena hadi leo wiki ya tatu licha ya jitihada za kuwatafuta kwenye vituo vya police zote za Dar, kwenye mahospitali na mortuaries zote. Hii style tuliona wakati wa utawala wa awamu ya tano ya Magufuli na wewe ukiwa makamo wa rais, tumeona yaliyompata Azory Gwanda, Ben Saanane, Roma Mkatoliki na wengine wengi waliokuwa wakiokotwa kwenye magunia na viroba.

Mheshimiwa Samia, nikuulize swali moja. Je, bado unayaendeleza yale yale ya kupoteza watu na kuwatupa mtoni? Mbona wewe unajifanya muislamu safi? Je, dini yako inaruhusu uue na kupoteza watu?

Au unashindwa kuwakemea huyo Sirro na polisi wake? Haya ndiyo yale mambo yaliyofanyika miaka iliyopita ya akina Abdallah Zombe na wenzake walivyowauwa vijana wasio na makosa wafanyabiashara wa madini na kuwaibia pesa zao? Haya ndiyo yale yale ya kuwaua vijana wapatao 7 Arusha waliokamatwa na polisi kwa kushukiwa kuwa wanapanga kuvizia na kuiba kwenya gari la benki lililokuwa likipeleka pesa Kiteto?

Inasikitisha kuona wananchi wanatoka majumbani mwao lakini hawarudi. HATA KAMA NI WASHUKIWA NA WAMEKAMATWA, KUNA TARATIBU ZAKE ZA KUPELEKWA MAHAKAMA NA FAMILIA ZAO KUFAHAMISHWA. Wewe mheshimiwa Rais Samia kwenye hotuba moja ulisema ulikamatwa kwa kosa la taa ya gari kutokuwaka. Je, ungewekwa mahabusu au kuumizwa, je familia yako ingefanyaje? Haingekuwa simanzi? Usifurahie mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu uchungu!

Hivi rais Samia unaona raha gani raia wako wakipotezwa au wakiuawa? Kweli una roho ngumu kiasi hiki kama Adolf Hitler! Onea huruma raia wako. Usifurahie unayoyaona, kama unafurahia ujue kuna KARMA.

HADI LINI WATU WATAENDELEA KUPOTEA?
 
Mama wale wale tu,Kamnada Ciro hakupaswa kuwepo alipo, kwenye wigo wake yamefanyika mengi tu ya hovyo!!!

Kitengo Cha supika kufokewa hadi kukimbia kazi kisa kahoji madeni,hatuna tofauti na Magufuli alivyomnyanyasa Assad kisa kasema kuna hela imepigwa!!!

Tunaenda kuweka historia ya kua na uchwara wa kike!!
 
Mfumo wowote ulioasisiwa, ukishasimama na ukajizatiti, kamwe hauwezi kupotea au kuondoka mara moja.

Tukumbuke wakati wa Magufuli, siyo Magufuli aliyekuwa akiteka au akiua kwa mkono wake, bali aliuimarisha na kuupa nguvu mfumo uliokuwa ukiteka, kupoteza na kuteka watu (naamini kuwa huo mfumo hakuasisi yeye, ulikuwepo hata kabla yake). Hii ina maana kuna watu waliajiriwa na kazi yao ilikuwa ni kuteka, kupoteza na kuua watu.

Wengi wa hawa wauaji na watekaji, baada ya kuteka na kuua sana, wakati wa marehemu, walipandishwa vyeo. Hawa watu bado wapo, na wengi wao wanashikilia ofisi zile zile au za juu zaidi, huku wakijua kuwa ni utekaji na uuaji ndivyo vilivyowapandisha mpaka kufika walipo sasa.

Akina Kingai, Goodluck, Mahita, Jumanne , etc, mnawaona wakiendelea kwenye ofisi za umma, tena wakiwa na madaraka makubwa zaidi. Kama kazi zao ndizo hizo, na bado wapo maofisini, mnafikiri wanafanya nini?
 
Mfumo wowote ulioasisiwa, ukishasimama na ukajizatiti, kamwe hauwezi kupotea au kuondoka mara moja.

Tukumbuke wakati wa Magufuli, siyo Magufuli aliyekuwa akiteka au akiua kwa mkono wake, bali aliuimarisha na kuupa nguvu mfumo uliokuwa ukiteka, kupoteza na kuteka watu (naamini kuwa huo mfumo hakuasisi yeye, ulikuwepo hata kabla yake). Hii ina maana kuna watu waliajiriwa na kazi yao ilikuwa ni kuteka, kupoteza na kuua watu.

Wengi wa hawa wauaji na watekaji, baada ya kuteka na kuua sana, wakati wa marehemu, walipandishwa vyeo. Hawa watu bado wapo, na wengi wao wanashikilia ofisi zile zile au za juu zaidi, huku wakijua kuwa ni utekaji na uuaji ndivyo vilivyowapandisha mpaka kufika walipo sasa. Akina Kingai, Goodluck, Mahita, Jumanne , etc, mnawaona wakiendelea kwenye ofisi za umma, tena wakiwa na madaraka makubwa zaidi. Kama kazi zao ndizo hizo, na bado wapo maofisini, mnafikiri wanafanya nini?
Acha upumbavu wako! Hata wakati wa kikwete watu walikuwa wanauliwa kama mwanahabari Mwangosi, Dr Mvungi,Mtikila pia alipata ajali ya ajabu ajabu pia Dr Ulimboka alitekwa,mauaji ya waandamanaji Arusha, Jeshi la polisi kuua wauza madini Morogoro na matukio ya ujambazi kila kona ya nchi! Wewempumbavu unakuja kuongea ujinga hapa! Huyo bibiako mbona kila siku misiba ya mauaji? Basi sema anawaua Rais Samia!
 
Mheshimiwa Rais, naomba nichukue nafasi hii nikupongeze kwa mambo mengi mazuri unayoyafanya ila kwa hili la watu kuanza kupotea kwenye utawala wako tayari ni doa kwenye serikali yako. Wiki mbili zilizopita kuna habari zimetokea magazeti kuwa kuna vijana watano wamepotea wakiwa wanaenda kusherekea Krismasi kwenye fukwe hapa Dar es Salaam.

Kwa maelezo yao ni kuwa walikamatwa na Police na wakawa wanapelekwa central police, baada ya hapo hawakusikika tena hadi leo wiki ya tatu licha ya jitihada za kuwatafuta kwenye vituo vya police zote za Dar, kwenye mahospitali na mortuaries zote. Hii style tuliona wakati wa utawala wa awamu ya tano ya Magufuli na wewe ukiwa makamo wa rais, tumeona yaliyompata Azory Gwanda, Ben Saanane, Roma Mkatoliki na wengine wengi waliokuwa wakiokotwa kwenye magunia na viroba.

Mheshimiwa Samia, nikuulize swali moja. Je, bado unayaendeleza yale yale ya kupoteza watu na kuwatupa mtoni? Mbona wewe unajifanya muislamu safi? Je, dini yako inaruhusu uue na kupoteza watu?

Au unashindwa kuwakemea huyo Sirro na polisi wake? Haya ndiyo yale mambo yaliyofanyika miaka iliyopita ya akina Abdallah Zombe na wenzake walivyowauwa vijana wasio na makosa wafanyabiashara wa madini na kuwaibia pesa zao? Haya ndiyo yale yale ya kuwaua vijana wapatao 7 Arusha waliokamatwa na polisi kwa kushukiwa kuwa wanapanga kuvizia na kuiba kwenya gari la benki lililokuwa likipeleka pesa Kiteto?

Inasikitisha kuona wananchi wanatoka majumbani mwao lakini hawarudi. HATA KAMA NI WASHUKIWA NA WAMEKAMATWA, KUNA TARATIBU ZAKE ZA KUPELEKWA MAHAKAMA NA FAMILIA ZAO KUFAHAMISHWA. Wewe mheshimiwa Rais Samia kwenye hotuba moja ulisema ulikamatwa kwa kosa la taa ya gari kutokuwaka. Je, ungewekwa mahabusu au kuumizwa, je familia yako ingefanyaje? Haingekuwa simanzi? Usifurahie mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu uchungu!

Hivi rais Samia unaona raha gani raia wako wakipotezwa au wakiuawa? Kweli una roho ngumu kiasi hiki kama Adolf Hitler! Onea huruma raia wako. Usifurahie unayoyaona, kama unafurahia ujue kuna KARMA.

HADI LINI WATU WATAENDELEA KUPOTEA?
Kazi iendelee.
 
Acha upumbavu wako! Hata wakati wa kikwete watu walikuwa wanauliwa kama mwanahabari Mwangosi, Dr Mvungi,Mtikila pia alipata ajali ya ajabu ajabu pia Dr Ulimboka alitekwa,mauaji ya waandamanaji Arusha, Jeshi la polisi kuua wauza madini Morogoro na matukio ya ujambazi kila kona ya nchi! Wewempumbavu unakuja kuongea ujinga hapa! Huyo bibiako mbona kila siku misiba ya mauaji? Basi sema anawaua Rais Samia!
Hao ni wapumbavu Pro chadema na kawaida yao kudandia matukio na kutageuza political mileage.
 
Back
Top Bottom