Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,361
- 6,485
Mara tu baada ya kushika kiti cha Urais kwa kula kiapo, Mhe. Rais Samia Hassan Suluhu alisema 'kazi iendelee'. Na kufanya msemo huo kuwa mwitikio wa salamu ili msemo huo udumu na kusikiksa mara kwa mara.
Sasa kuna maswali yafuatayo:
Sasa kuna maswali yafuatayo:
- Kwa kuzingatia lugha ni kwamba kazi hiyo si zaidi ya moja kwani haisemwi 'kazi ziendelee', je, ni kazi gani hiyo anayoiongelea Mhe. Rais Samia? Je, au ni kazi jumuishi?
- Kuna awamu tano kabla ya Mhe. Rais Samia kushika kiti cha Urais, je ni kazi ya awamu ipi inayotakiwa kuendelea? Au awamu zote?
- Je, kuna baadhi ya wananchi wamelengwa hapa au wote?