Rais Samia hashauriki au ana washauri wabaya?

Rais Samia hashauriki au ana washauri wabaya?

Kinachoendelea hivi sasa nchini Tanzania inaonyesha aidha rais Samia Suluhu Hassan hashauri (haambiliki) ama ana washauri wabaya wanaompotosha

Kukamatwa kwa mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu na kufunguliwa kesi ya uhani ni jambo la kushangaza ambalo linaonyesha pengine lengo ni kudhibiti kasi yake kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu

Kufungiwa kwa Kanisa la ufufuo na uzima la Askofu Josephat Gwajima kwa kutumia haki yake ya kikatiba kutoa maoni yake kukemea utekaji ni jambo lingine la kushangaza

Wataalam wa mambo ya Kidiplomasia na siasa wanajiuliza hivi rais Samia hana washauri ama anashauriwa na kukaidi ushauri wa wasaidizi wake?

Pia wabobezi wa siasa za nchi hii wanajiuliza chama cha CCM kimeshindwa kumshauri mwenyekiti wake ambaye pia ni rais wa nchi kujitenga na sintofahamu hii ya kesi ya Lisu na sakata la kufungiwa kanisa la Gwajima ili kukinusuru chama na Serikali yake.

Ushauri wangu kwa rais Samia aangalie upya kesi ya Lisu ikimpendeza Serikali kupitia kwa mwanasheria mkuu iiambie Mahakama kuwa haina nia ya kuendelea na kesi hiyo hivyo ifutwe

Pia rais angemuagiza waziri wake wa mambo ya ndani kulifungilia kanisa la Gwajima na kuwaacha waumini wawe na uhuru wao wa kuabudu

Aidha rais anatakiwa aende mbali zaidi na kuahidi kufanya marekebisho ya uchaguzi kwa kuweka tume huru kweli kweli ya uchaguzi na sheria na kanuni rafiki za uchaguzi kwa kipindi hiki kifupi kilichobaki kabla ya uchaguzi

Kwa upande wa katiba mpya anatakiwa kuahidi kuahidi kwamba itapatikana baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu kupita

Kama rais Samia atafanya uamuzi huu mgumu ataziishi zile 4R zake ambazo awali alivyoingia madaraka na kuzitangaza na kuzitekeleza kwa kipindi kile zilimpatia umaarufu mkubwa na kukubalika ndani na nje ya nchi

Lakini cha kushsngaza baadaye hapa upepo wa kisiasa ukabadilika ndipo watu wanaoitakia mema nchi hii wanajiuliza hivi rais ana washauri kweli au haambiliki?

Mwalimu Julie's Nyerere kipindi cha utawala wake aliwahi kuwa mkaidi hasikilizi ushauri wa wasaidizi wake na wananchi wake juu ya hali ngumu ya maisha na kumtaka abadilishe mfumo wake wa siasa hasa sheria ngumu za Azimio la Arusha aligoma katakana kugeuka nyuma wakamtunga jina la haambiriki

Baada ya kuona hali ya uchumi imezidi kuwa ngumu mwaka 85 akaang'atuka madarakani na kumuachia nchi Ally Hassan Mwinyi ambaye alifita Azimio la Arusha na kutangaza Azimio la Zanzibar

Mwinyi akfungua milango ya uchumi huru akaingiza siasa za kibepari huku chama chake kinaimba siasa za ujamaa na kujitegemea

Sasa rais Samia akikaidi ushauri wa wasaidizi wake na wananchi naye ataitwa "haambiliki" ni vyema akachukua hatua sasa hivi kurudi 4R zake ili kurejesha heshima yake ya awali

Comasava
Huyu ni hatari zaidi ya JPM jiulize mpaka wazee wale walipkua wana mnanga JPM sasa hivi wapo kimyaa refer mzee makamba kama hayupo anajua akiongea kweli tu ana sandishwa.
idd amin mama
 
Huyu ni hatari zaidi ya JPM jiulize mpaka wazee wale walipkua wana mnanga JPM sasa hivi wapo kimyaa refer mzee makamba kama hayupo anajua akiongea kweli tu ana sandishwa.
idd amin mama
Miye nashangaa wazee vingunge wa CCM kina Butiki, Warioba, Makamba Yusuf wakikemea hawamaanishi kutoka moyo kama alivyokuwa akifanya Nyerere kwa Mwinyi wanaongea kiwoga woga wameufyata mpaka anaibuka Gwaji boy
 
Miye nashangaa wazee vingunge wa CCM kina Butiki, Warioba, Makamba Yusuf wakikemea hawamaanishi kutoka moyo kama alivyokuwa akifanya Nyerere kwa Mwinyi wanaongea kiwoga woga wameufyata mpaka anaibuka Gwaji boy
Hao wananufaika umemwona JK now anamtetea samia ilo hali anajua kanisa uwezo hana
 
Kama angelikuwa yuko kwa ajili ya nchi na wananchi, angeliyafanyia kazi yote yaliyoorodheshwa kwenye mada
Ni kweli kabisa asipofanya hivyo tutajua kweli yeye bibi haambiliki
 
Boi Manda kuna kikundi/vikundi ndani ya jeshi la polisi/etc ambavyo ndiyo vinatumika na siyo serikali ila vilipitia mafunzo rasimi ya serikali (rejea kauli ya msemaji wa Jeshi kuhusu vigogo kupeleka majina majeshini), hivyo vikundi ndiyo vinahusika na ukiangalia mfano wale polisi waliopiga mabomu wafuasi wa Gwajiboy unaona kabisa siyo wale wazalendo ila ni wale select wa kile kikundi ila wanatumia uniform na rasilimali za serikali. Maana yake kama hicho kikundi kinamilikiwa labda ya nani hatujui
Kama hicho kikundi kinavaa uniform rasmi za polisi na kushika siraha za kivivita basi kina baraka na Dora kama kile kikindi cha Urusi
 
Mwijaku amekataliwa Kigoma
Mwijaku anatoka na vitoto vya chuo huku ana mke, kwingineko ni mshauri mtema madini.
Hana maadili yule dogo hawezi kutoboa kwenye siasa aendelee tu na fani yake ya umalaya na uchawa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom