Rais Samia hashauriki au ana washauri wabaya?

Rais Samia hashauriki au ana washauri wabaya?

Vyote viwili na unaweza kuongeza kuwa hana uwezo mkubwa wa kufikiri ndipo aamue. Wakati mwingine naona kama Khadija Kopo fulani
😄 🤣 eti Khadija ❤️ wa mipasho
 
Wananchi wa TZ siyo waajiri wa rais, rais wa TZ ni tunda la tume yake ya uchaguzi.
Si kaingia madarakani kwa mujibu wa Katiba ya nchi baada ya Mwendazake? Kwa hiyo ni zao la wananchi
 
Maombi ya watu tena watu zaidi ya elfu kumi wa ufufuo na uzima nchi mzima, hata kama Mungu ni kiziwi lazima atasikia hata ombi moja la mja wake pale
 
Lissu kakamatwa na jeshi la polisi sawa na washukiwa wengine wa uhalifu, tunamlaumu vipi Rais? nyie mngewalalamikia waendesha mashitaka na mawakili wa serikali
 
Kinachoendelea hivi sasa nchini Tanzania inaonyesha aidha rais Samia Suluhu Hassan hashauri (haambiliki) ama ana washauri wabaya wanaompotosha

Kukamatwa kwa mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu na kufunguliwa kesi ya uhani ni jambo la kushangaza ambalo linaonyesha pengine lengo ni kudhibiti kasi yake kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu

Kufungiwa kwa Kanisa la ufufuo na uzima la Askofu Josephat Gwajima kwa kutumia haki yake ya kikatiba kutoa maoni yake kukemea utekaji ni jambo lingine la kushangaza

Wataalam wa mambo ya Kidiplomasia na siasa wanajiuliza hivi rais Samia hana washauri ama anashauriwa na kukaidi ushauri wa wasaidizi wake?

Pia wabobezi wa siasa za nchi hii wanajiuliza chama cha CCM kimeshindwa kumshauri mwenyekiti wake ambaye pia ni rais wa nchi kujitenga na sintofahamu hii ya kesi ya Lisu na sakata la kufungiwa kanisa la Gwajima ili kukinusuru chama na Serikali yake.

Ushauri wangu kwa rais Samia aangalie upya kesi ya Lisu ikimpendeza Serikali kupitia kwa mwanasheria mkuu iiambie Mahakama kuwa haina nia ya kuendelea na kesi hiyo hivyo ifutwe

Pia rais angemuagiza waziri wake wa mambo ya ndani kulifungilia kanisa la Gwajima na kuwaacha waumini wawe na uhuru wao wa kuabudu

Aidha rais anatakiwa aende mbali zaidi na kuahidi kufanya marekebisho ya uchaguzi kwa kuweka tume huru kweli kweli ya uchaguzi na sheria na kanuni rafiki za uchaguzi kwa kipindi hiki kifupi kilichobaki kabla ya uchaguzi

Kwa upande wa katiba mpya anatakiwa kuahidi kuahidi kwamba itapatikana baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu kupita

Kama rais Samia atafanya uamuzi huu mgumu ataziishi zile 4R zake ambazo awali alivyoingia madaraka na kuzitangaza na kuzitekeleza kwa kipindi kile zilimpatia umaarufu mkubwa na kukubalika ndani na nje ya nchi

Lakini cha kushsngaza baadaye hapa upepo wa kisiasa ukabadilika ndipo watu wanaoitakia mema nchi hii wanajiuliza hivi rais ana washauri kweli au haambiliki?

Mwalimu Julie's Nyerere kipindi cha utawala wake aliwahi kuwa mkaidi hasikilizi ushauri wa wasaidizi wake na wananchi wake juu ya hali ngumu ya maisha na kumtaka abadilishe mfumo wake wa siasa hasa sheria ngumu za Azimio la Arusha aligoma katakana kugeuka nyuma wakamtunga jina la haambiriki

Baada ya kuona hali ya uchumi imezidi kuwa ngumu mwaka 85 akaang'atuka madarakani na kumuachia nchi Ally Hassan Mwinyi ambaye alifita Azimio la Arusha na kutangaza Azimio la Zanzibar

Mwinyi akfungua milango ya uchumi huru akaingiza siasa za kibepari huku chama chake kinaimba siasa za ujamaa na kujitegemea

Sasa rais Samia akikaidi ushauri wa wasaidizi wake na wananchi naye ataitwa "haambiliki" ni vyema akachukua hatua sasa hivi kurudi 4R zake ili kurejesha heshima yake ya awali

Comasava
Mwache aendelee hivyo hivyo, tunataka kufikia Oktoba mwaka huu ahame Tanganyika arudi kijijini kwake Kizimkazi
 
Lissu kakamatwa na jeshi la polisi sawa na washukiwa wengine wa uhalifu, tunamlaumu vipi Rais? nyie mngewalalamikia waendesha mashitaka na mawakili wa serikali
Mahaka kazi yake kutafsi sheria zilitungwa na Bunge Serikali inasimamia na kutekeleza sheria hivyo wanaokata na kushitaki ni jeshi la Polisi ambalo lipo chini ya muhimili wa Serikali upo hapo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom