Rais Samia hashauriki au ana washauri wabaya?

Rais Samia hashauriki au ana washauri wabaya?

Lengo la kumkamata Lissu ni kupoza upinzani haswa kasi ya Lissu maana watu walishaichoka CCM na wenyewe wanajuwa hayo. Huko Zanzibar watu wanaandamana kutaka Muungano uvunjike maana hawaoni umuhimu wake na raia wanalaumu viongozi wa CCM, in short, hata huko pia, CCM HAITAKIWI. Kila zama zina mwisho wake, CCM imefikia taamati, wananchi hatuitaki.

Mama Abdul (Samia) akitaka watu wamchukulie serious, aachane na kuwaweka kina kajamba nani (Steve Nyerere, Dotto Magari, Mwijaku) karibu naye, wale hawana akili za kushauri hata wake zao sembuse kuliongoza taifa. Unawapa vyeo vya usemaji mkuu wa serikali ili iweje?
Kama lengo lake ndio hilo sasa limedunda Watanzania na dunia nzima ndio wamezidi kumpenda Lisu na kuona anaonewa

Sasa hapo hekima ilitakiwa abadilishe gea angani amuachie huru angalau na kumpenda Lisu kinafiki amuite Ikulu wayajenge nchi isonge mbele
 
Wewe ulishawahi kumshauri hakushaurika??

Kuwa na adabu na Rais wako.
 
Mzee mnafiki sana mkuu. Siku ya matokeo ya uchaguz wa kenya aliongea kwa kutumia akili zake ila hapo kaongea kwa kutumia tamaa zake tu
Tena yeye ndiye rais mstaafu pekee aliyebakia alitakiwa awe mzee wa Taifa kusimama kwenye haki kwa watu wote asiwe mtu wa upande mmoja angejijengea heshima kama Mwalimu
 
Wewe ulishawahi kumshauri hakushaurika??

Kuwa na adabu na Rais wako.
Hapa jukwaani nimefanya nini? Si nimemshauri kusoma hujui hata kuona huoni?

Wewe unayeyemuimbia pambio za kumfurahisha huku unajua kabisa Mfalme kakosea humwambii ukweli ndiye unayemkosea adabu
 
Tena yeye ndiye rais mstaafu pekee aliyebakia alitakiwa awe mzee wa Taifa kusimama kwenye haki kwa watu wote asiwe mtu wa upande mmoja angejijengea heshima kama Mwalimu
Mnafiki huyo. Wajuzi wa mambo wanasema yeye ndiye anachezesha hili game hivo ni mnnufaika. Mbona kule Kenya mzee Kenyatta amekuwa mtu wa kuwaunganisha wanasiasa wa kule ila huyu very snitching. Mpaka kale kaheshima tumemvunjia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom