Rais Samia hashauriki au ana washauri wabaya?

Rais Samia hashauriki au ana washauri wabaya?

Kinachoendelea hivi sasa nchini Tanzania inaonyesha aidha rais Samia Suluhu Hassan hashauri (haambiliki) ama ana washauri wabaya wanaompotosha

Kukamatwa kwa mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu na kufunguliwa kesi ya uhani ni jambo la kushangaza ambalo linaonyesha pengine lengo ni kudhibiti kasi yake kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu

Kufungiwa kwa Kanisa la ufufuo na uzima la Askofu Josephat Gwajima kwa kutumia haki yake ya kikatiba kutoa maoni yake kukemea utekaji ni jambo lingine la kushangaza

Wataalam wa mambo ya Kidiplomasia na siasa wanajiuliza hivi rais Samia hana washauri ama anashauriwa na kukaidi ushauri wa wasaidizi wake?

Pia wabobezi wa siasa za nchi hii wanajiuliza chama cha CCM kimeshindwa kumshauri mwenyekiti wake ambaye pia ni rais wa nchi kujitenga na sintofahamu hii ya kesi ya Lisu na sakata la kufungiwa kanisa la Gwajima ili kukinusuru chama na Serikali yake.

Ushauri wangu kwa rais Samia aangalie upya kesi ya Lisu ikimpendeza Serikali kupitia kwa mwanasheria mkuu iiambie Mahakama kuwa haina nia ya kuendelea na kesi hiyo hivyo ifutwe

Pia rais angemuagiza waziri wake wa mambo ya ndani kulifungilia kanisa la Gwajima na kuwaacha waumini wawe na uhuru wao wa kuabudu

Aidha rais anatakiwa aende mbali zaidi na kuahidi kufanya marekebisho ya uchaguzi kwa kuweka tume huru kweli kweli ya uchaguzi na sheria na kanuni rafiki za uchaguzi kwa kipindi hiki kifupi kilichobaki kabla ya uchaguzi

Kwa upande wa katiba mpya anatakiwa kuahidi kuahidi kwamba itapatikana baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu kupita

Kama rais Samia atafanya uamuzi huu mgumu ataziishi zile 4R zake ambazo awali alivyoingia madaraka na kuzitangaza na kuzitekeleza kwa kipindi kile zilimpatia umaarufu mkubwa na kukubalika ndani na nje ya nchi

Lakini cha kushsngaza baadaye hapa upepo wa kisiasa ukabadilika ndipo watu wanaoitakia mema nchi hii wanajiuliza hivi rais ana washauri kweli au haambiliki?

Mwalimu Julie's Nyerere kipindi cha utawala wake aliwahi kuwa mkaidi hasikilizi ushauri wa wasaidizi wake na wananchi wake juu ya hali ngumu ya maisha na kumtaka abadilishe mfumo wake wa siasa hasa sheria ngumu za Azimio la Arusha aligoma katakana kugeuka nyuma wakamtunga jina la haambiriki

Baada ya kuona hali ya uchumi imezidi kuwa ngumu mwaka 85 akaang'atuka madarakani na kumuachia nchi Ally Hassan Mwinyi ambaye alifita Azimio la Arusha na kutangaza Azimio la Zanzibar

Mwinyi akfungua milango ya uchumi huru akaingiza siasa za kibepari huku chama chake kinaimba siasa za ujamaa na kujitegemea

Sasa rais Samia akikaidi ushauri wa wasaidizi wake na wananchi naye ataitwa "haambiliki" ni vyema akachukua hatua sasa hivi kurudi 4R zake ili kurejesha heshima yake ya awali

Comasava
Siasa imevamiwa na watu wachache wenye ngvu sana, na ndyo wanao dhibiti nguvu ya chama na mustakabali wa uchaguzi
Hawa Russia wanaitwa OLIGARCHS, ila PUTIN amewadhibiti na hata kuwatanguliza peponi

OLIGARCHS (wachungaji/ wanamamlaka wachache) rich business leaders with a great deal of political influence
OLIGARCHS wengi wao hawaonekani lkn wana nguvu sana.
Hata awamu ya kwanza walimjaribu JKN lakini akwashinda, na ni wakati alikuwa vulnerable sana

View: https://youtu.be/mDH-TF7OYt0?si=6hwUmUtN3s34AOpE
 
Mkuu umeongea kimafumbo sana na mifano migumu umetuacha hewani funguka vizuri inaonyesha una madini mengi muhimu
 
Msikubali uhuni wa wachache
 
Kinachoendelea hivi sasa nchini Tanzania inaonyesha aidha rais Samia Suluhu Hassan hashauriki (haambiliki) ama ana washauri wabaya wanaompotosha

Sasa rais Samia akikaidi ushauri wa wasaidizi wake na wananchi naye ataitwa "haambiliki" ni vyema akachukua hatua sasa hivi kurudi 4R zake ili kurejesha heshima yake ya awali
Comasava
Naunga mkono hoja, niliwahi kuuliza Inawezekana ni Kiburi na Jeuri or Real Busy? Wasaidizi wake hawajamwambia ukweli wa ubatili wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi?,Tufanye nini kupata Haki?

Pia niliuliza Wasaidizi wa Magufuli walimuogopa hadi kushindwa kumsaidia, Je Wasaidizi wa Samia wanamsaidia kwa kumweleza ukweli au nao wanamuogopa? Tumsaidie au..?
P
 
Mkuu umeongea kimafumbo sana na mifano migumu umetuacha hewani funguka vizuri inaonyesha una madini mengi muhimu
Umeelewa ila unataka kunifukunyua, ili niwe victimised
 
Ishu ya katiba mpya Mkwele Kikwete ndio alikorofisha kwa uoga wake ile rasmu ya Warioba watu wakamtisha wakamuambia chama kitakufia mikononi mwako akaogopa katengeneza speaker wa wa bunge la katiba Samweli Sita wakavuruga mchato wote

Kikwete alikuwa na nafasi kuweka regency ta kuwa rais aliyeleta katiba mpya nchini lakini wapi washauri wake wakapotosha kanajisi mfumo mzima wa katiba mpya ukafa kifo cha mende

Sasa huyu bimkubwa akiweza kuleta katiba mpya kwenye utawala wake pamoja na changamoto zote hizi anazopitia atajiwekea heshima kubwa siku za usoni hata asipokuwepo ulimwenguni atakumbukwa kwa hilo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom