Rais Samia ebu wambie Mawaziri Makamba, Nape, Mwigulu na Dotto ya kuwa wao ni Mawaziri sio Marais watarajiwa. Hii misafara hawana hadhi hiyo

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Kwanza nianze kwa kupongeza Wakurugenzi na watendaji wa mtandao pendwa wa JamiiForums.

Pili naomba nikili yawazi yakuwa maboresho yaliyofanywa na JF Kuna wanaJF wengi tumekuwa nje ya nje ya online off, kkwa sababu ya maboresho haya.

Niende kwenye mada, hivi majuzi Mimi nilikuwa,miongoni mwa vijana tulio shuhudia Waziri wa habari na technolojia akizindua mnara wa kkwa ajili ya upatikanaji wa internet kutoka moja kwa Moja mlima Kilimanjaro.

Nikili wazi Mimi ni miongoni mwa mapota walio kuwa tumebeba mizigo mizito kwakweli.

Kilichonoleta hapa ni kuhoji wingi wa msafara wa Magali aliombatana nao Nape naye kupitia maeneo ya Marangu yaaani alikuuwa na utilili wa magari hatari na king'ora juu yake Sasa najiuliza huo msafara ulikuwa wa Nini?

Kulikuwa na umuhimu gani kuwa na magari zaiddi ya 50 kumsindikiza nape?who are you by dhen way?

Uwaziri ndo unakupa hadhi ya kutembea na ving'ora kweli?

Nikuombe Mh mama Rais maana hii imekuwa kama ni fasheni.
 
Rais Samia amekuwa sikio la kufa halisikii dawa. Mpaka sisi wana CCM tumemchoka maana anakumbatia majizi na majitu yanayomhujumu. Ngoja hiyo 2025 tuone, tutaanza naye kumtosa ndani ya CCM akishangaa atakuwa na kesi za kujibu
 
Nchi ishakuwa UKOO wa KAMBALE huu, kila mtu ana sharubu.

Unayemuomba, unadhani hajui? Pengine mtazamo wako na wake ni hasi na chanya!
  • Kalipa malimbikizo, kapandisha madaraja, nyongeza 23%, TOZO ZAKE sasa!
  • Wanaua miradi ili waanzishe miradi
  • Wanakopa ili kuweza kusafiri
  • Wanakagua maji ya mito kwa helicopter, wakishajua ni pungufu, watafanya nini?
  • Anateua na kutengua kabla hajaapisha
  • Hii alistahili mtangulizi wangu....mtangulizi wangu tulipingana
  • Bei ya mafuta Znz iko constant, soko la dunia inashuka, Tanganyika bei inakwea minazi
  • Tozo zinajenga madarasa, mikipo inajenga madarasa, UMEYAONA?
  • Wamasai wananyang'anywa ardhi, bandari kakabidhiwa mwarabu, unaelewa chochote?
  • Pesa ya makinikia, wanasema 600b imelipwa, unajua hata kama imelipwa na iko wapi?
  • Jumla ya Tozo za simu zilizokusanywa zilitangazwa mara moja tu, kwanini hawakuendelea na utaratibu huo?
  • Wanasema kuna kiongozi anaishi kwa mtindo wa pembe tatu, nini tatizo?
  • Zile ndege zilizopigiwa kelele kutokuwa na tija kwa taifa, zinatumika? Wanasema wamelipia nyingine, za nini?

Ngoja tuendelee tu
 
Kilichonoleta hapa ni kuhoji wingi wa msafara wa Magali aliombatana nao Nape naye kupitia maeneo ya Marangu yaaani alikuuwa na utilili wa magari hatari na king'ora juu yake Sasa najiuliza huo msafara ulikuwa wa Nini?
Hao ni wapambe wake humo wameletwa kwaajili ya perdiems ili wamwone anafaa
 
Rais Samia amekuwa sikio la kufa halisikii dawa. Mpaka sisi wana CCM tumemchoka maana anakumbatia majizi na majitu yanayomhujumu. Ngoja hiyo 2025 tuone, tutaanza naye kumtosa ndani ya CCM akishangaa atakuwa na kesi za kujibu
Wewe mkata kiuno wa Dikteta umewageuka lini?
 
Ukimtoa majaliwa hawa mawaziri Wengi haswa makamba na nauye Nazi zao wanazifanya kama vile hakuna mtu juu yao hawa watatupa pressure uchaguzi mawazo yaonautendaji wao nikuwa uchaguzi hachagui mpiga kura nimabavu kwenda mbele janga hili
 
Kama yeye anatembea na msafara wa Magari 70 unashangaa nini waziri kuwa na msafara wa Magari 50 hii nchi sijui lini mtakuwa na akili mkiambiwa ccm sio chama bali genge la wahuni muwe mnaelewa hizi ngonjera zenu za keyboard hazita badalisha chochote.

Kidumu chama tawala"
 
Rais Samia amekuwa sikio la kufa halisikii dawa. Mpaka sisi wana CCM tumemchoka maana anakumbatia majizi na majitu yanayomhujumu. Ngoja hiyo 2025 tuone, tutaanza naye kumtosa ndani ya CCM akishangaa atakuwa na kesi za kujibu
Hamna ubavu wa kumtosa Samia achilia mbali kumkemea wewe ni panya mbele ya paka!!

Hapo ukute una account yenye real name yako huko FB na twitter unamuabudu kwa pambio za sifa ukija kwenye ID fake unapumua kwa nyuma!
Kwa namna mlivyo watu wa hovyo huko CCM huyu mama atawanyoosha atakavyo.
 
Bandiko lako zuri ila jitahidi sama matumizi ya L na R uyatumie mahali sahihi maana huwa inakera mno yanapokosewa.
 
Back
Top Bottom