Rais Samia: Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere kujaribiwa mwakani

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Rais Samia Suluhu Hassan leo ameshuhudia utiaji saini wa mikataba ya kuimarisha Gridi ya Taifa na usambazaji wa umeme Vijijini iliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023. Kwenye hotuba yake Rais Samia anasema wakati anakabidhiwa madaraka jambo lililokua linamuumiza kichwa ni wapi atapata pesa za kukamilisha miradi mikubwa ya SGR na JNHPP.

Rais Samia anasema kwa kua alikua na nia ya dhati ya kukamilisha miradi hiyo alipambana na hatimaye leo iko kwenye hatua nzuri ikiwemo bwawa la Mwalimu Nyerere ambalo Mwakani Mungu akijaalia litawashwa kwa ajili ya kuzalisha umeme wa majaribio.

"Kwenye nia pana njia leo SGR nina pesa mpaka ya lot ya 6 kufika Kigoma sikutegema. Lakini kwa upande wa bwawa nadhani mwakani mapema mapema tunaanza kuliwasha na ku-generate umeme wa awali wa majaribio."- Mhe. Rais Samia Suluhu

Fo7KsgEXEAIhhHG
 
Asante sana Mhe. Rais. Dhamira yako ya dhati kabisa ilianza siku ya kwanza ulipokula kiapo kuongoza nchi. Mwenyezi Mungu akubariki zaidi uikamilishe miradi ya kimkakati ya nchi. 🙏🙏🙏
 
Mkuu,hilo bwawa linahutaji not less than misimu mitatu ya mvua za kutosha, otherwise ni mba mba mba.
Hayo ndio tunayoyataka, sio ohhooo miti mil. Sijui imekatwa ,Mara sijui haliwez kujaa labda miaka 3, sijui huwa wanasema hayo kumkomoa Nani.
 
Ndio Tunayo Hitaji Kuyasikia
Pia Ahadi Waliyo Pewa Watanzania Kuwa Bei Ya Umeme Itapungua kwa kiwango Kikubwa ndio izingatiwe Haswa
 
Haya ndio mambo ya kuwaambia watanzania,sio story za marehemu wakati na yeye alikua msaidizi wa marehemu,watanzania hatutaki porojo na manung’uniko tunataka tuone kazi zinafanyika.
Nyie ndio mnaosababisha Marehemu atajwe tajwe! Badala uoneshe tofauti kwa kujadili au kwasilisha yanayofanana na uzi umemleta Marehemu!!
 
Safi sana mama,watumishi tunakukubali sana kwa kuondoka ukritimba kwetu,mungu akujalie heri
 
Back
Top Bottom