MANKA MUSA
JF-Expert Member
- Jul 9, 2014
- 922
- 1,093
Kutoka angani naliona Bwawa kubwa, liliojengwa kutoka kwenye urithi wetu wa mto Rufiji, katikati ya Hifadhi yenye jina lake Nyerere mtu wa kipekee. Naliona Bwawa lile na kukumbuka kwamba wakati Mama Kizimkazi anaingia madarakani lilikuwa 33% tu, angeliweza kuamua kuachana nalo, lakini kwa mapenzi kwa nchi yake na busara tele alizojaaliwa, sasa ndoto hii inaenda kutimia. Machozi ya furaha yalinilenga.
Mama ni mwenye maono na hesabu kali, ameukwepa mtego wa Umeme wa mafuta kama ule wa Symbion na Richmond kila wakati ulileta kashfa kubwa katika nchi yetu. Mawaziri kutoka kwa Kalemani aliyeanza kutoka asilimia 0-37 hadi kwa January aliyefikisha kutoka asilimia 37 hadi 91 mnastahili pongezi.
Mama amefunga mkanda hatimaye Megawatts 235 zimeingia leo kwenye gridi ya Taifa chini ya usimamizi wa Dkt Biteko mashine moja iliyowashwa kati ya Tisa zilizopo hapa ni sawa na vinu vinne vya bwawa la Kidatu, vinu vinne vina jumla ya megawatts 204 hapa JNHPP kuna vinu 9 kila moja kinazalisha megawatts 235 jumla zitazalisha megawatts 2115.
Mungu mkubwa, yeye alitupa Rais huyu mwenye maono na sasa ndoto ile ya umeme wa uhakika inakwenda kutimia.
Hakika Rais Samia anastahili pongezi toka siku ya kwanza ulipounga mkono kuendeleza jitihada hizi amelipigania utafutaji wa fedha nyingi na kutekeleza, Ulale salama Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuasisi mradi licha ya maneno mengi kwenye mradi huu ulisimama imara. Kwa taarifa miradi ya kimkakati uliyoiacha hakuna kilichosimama. Taifa linakushukuru.
Mama ameandika Historia kubwa sana itakayofuta vilio vya Wananchi wengi nimewaza juu ya kuimarika kwa upatikanaji wa Umeme. Tutawahadithia wajukuu zetu juu ya mgao mkali wa Umeme waone kama ni ndoto au ni jambo la kihistoria nyakati ngumu hazidumu mbele ya viongozi imara kama Rais Samia.
Dear Mama Samia, Hayati Baba wa Taifa na Hayati Magufuli alipo wamefurahi sana kuwa Rais Samia amekamilisha kile kilichokwama zaidi ya miaka 60.
Hongera sana Mama umeweza sana wacha nilie na dua njema, nakuombea.
#MamaYukoKazini