Zitto kimsingi sio mpinzani, ni sehemu ya serikali huko Zanzibar, na hata huku bara alishasema hatakuwa anampinga Samia kama alivyofanya wakati wa Magufuli, kwa hiyo hata kama Samia akikosea Zitto atakuwa kimya.
Hii maana yake hapo kwenye huo mkutano wa TCD serikali ndio ilihudhuria huo mkutano, vyama vya ukweli vya upinzani havikuwa na muwakilishi.
Vyema kama kweli wako serious wanataka kuleta amani na maelewano hapa nchini, waanze kwa kuwakaribisha wapinzani lakini sio kujadili jambo ambalo lipo wazi kisheria, huo utakuwa ni utoto.