Rais Samia ashiriki Kumbukumbu ya Mashujaa Dodoma. Apendekeza Dodoma pajengwe mnara wenye hadhi ya makao Makuu ya nchi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma leo tarehe 25 Julai, 2022

- Rais amewasili katika viwanja vya mashujaa Dodoma.

- Gwaride la kumbukumbu ya siku ya Mashujaa limefanywa

- Viongozi wa dini mbalimbali wamepewa nafasi ya kufungua shughuli hii kwa maombi.

- Wimbo wa taifa umeimbwa

HOTUBA YA RAIS SAMIA
- Awali ya yote Tumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kujaalia nchi yetu kuwa na amani mpaka siku ya leo muhimu kwetu. Umuhimu wa siku hii ya leo unaonekana si hapa Dodoma tu lakini mikoa mengine yote ambayo leo hii inaadhimisha siku hii, leo hii na wakati huu.

- Mashujaa wetu walipambana katika nyanja mbalimbali
Mashujaa wetu walipambana katika nyanja mbalimbali dhidi ya ukoloni, ukandamizaji na uchokozi. Walipambana kifikra na kivitendo, kati ya vita vilivyopiganwa na Mashujaa wetu ni pamoja na vita vya majimaji, Vita ya pili ya dunia ambapo uwezo wa Mwenyekiti Mzee wetu ni ushahdi wa kwamba Mashujaa wetu walikuwapo na bado wapo.

Halikadhalika walipambana kwenye mapinduzi ya Zanzibar, vita vya ukombozi wa Afrika hasa Kusini mwa Afrika, vita ya Kagera na vita vya ukombozi mbalimbali ndani na nje ya bara la Afrika. Tunawakumbuka na kuwaenzi mashujaa wetu hawa waliojitoa muhanga wakilinda uhuru, uhai pamoja na heshima ya taifa na bara la Afrika.

- Maadhimisho haya si kwa waliopoteza uhai wao tu
Maadhimisho haya si kwa waliopoteza uhai wao tu lakini pia kwa wale waliopata ulemavu wa maisha na waliotoa michango yao kwa njia moja au nyingine. Kwa hali hiyo Watanzania hatuwezi kusahau mchango wa hali, mali na hali uliotolewa na Mashujaa hawa ndiyo sababu siku kama ya leo tunaadhimisha Mashujaa hawa.

Mtakumbuka kwamba kwa hivi karibuni hatukuweza kufanya maadhimisho haya kutokana na janga la Uviko-19 lililoukumba ulimwengu lakini leo Mungu ametujaalia tumeweza kukutana na tutazidi kukutana. Leo pia tunawakumbuka wazee wetu, viongozi wetu walioasisi taifa hili na ambao wametangulia mbele za haki hususani Mwalimu Nyerere na Hayati Karume pamoja na wengine walioshirikiana nao na ambao walikuja kuyaendeleza baada yao. Michango yao hiyo ndiyo imeifanya izidi kujijengea heshima na kutambulika katika mataifa mbalimbali duniani kote.

- Makao makuu ya nchi ni Dodoma hakuna kurudi nyuma
Ni furaha kwamba maadhimisho haya yanafanyika Dodoma makao makuu ya nchi katika uwanja ambapo mwaka 2016 wakati wa maadhimisho haya Hayati Magufuli alitangaza uamuzi wa kishujaa kuhamia Dododma. Napenda kutumia fursa hii kutangaza kuwa serikali imedhamiria kwa dhati kuendeleza uamuzi ule kama sehemu moja wapo ya kuenzi maono ya shujaa wetu Hayati Julias Kambarage Nyerere.

Naomba mniruhusu nirudie wito wa Hayati Magufuli kwamba Makao Makuu ya Tanzania ni hapa jijini Dodoma na hakuna kurudi nyuma. Jitihada za kujenga jiji la makao makuu ya taifa zimeendeezwa kama mnavyojionea wenyewe. Mpaka sasa ujenzi wa awamu ya pili pale Mtumba au Magufuli City unaohusisha majengo ya kudumu yatakayohusisha watumishi wote bado unaendelea.

- Dodoma pajengwe mnara wenye hadhi ya Makao Makuu ya Nchi
Waheshimiwa viongozi ndugu Wananchi, kutokana na umuhimu wa siku hii nataka kupendekeza kwamba kwakuwa jiji la Dodoma linakua na uwanja huu tuko katikati ya mji nipendekeze kwa Waziri Mkuu ofisi yako pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutafuta eneo kubwa kujenga mnara mkubwa wenye hadhi ya Makao Makuu ya nchi kwa gharama zitakazostahimilika.

Aidha, ameongeza amependekeza Ofisi ya Waziri Mkuu na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutengeneza utaratibu wa maadhimisho yenye gharama nafuu zaidi.

Mwisho, Rais Samia amemaliza kwa kuwahimiza Wananchi Juu ya chanjo ya Uviko-19 pamoja na kuhimiza suala la sensa ifikapo mnamo Agosti 23.
 
Sasa anapendekeza au anasema patajengwa? Sasa kama na raisi wa nchi na yeye anapendekeza nani aseme kwamba pajengwe?
 
UVCCM TAIFA
JULAI 25, 2022

KUMBUKUMBU YA SIKU YA MASHUJAA DUNIANI
Nukuu za hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SAMIA SULUHU HASSAN kwenye maadhimisho ya siku ya Mashujaa Duniani yaliofanyika kitaifa makao makuu ya nchi Dodoma kwenye Uwanja wa mashujaa.

#AlipoMamaVijanaTupo
#ShirikiUchaguziKwaUadilifu
#2022JiandaKuhesabiwa
#KaziIendelee.
IMG-20220725-WA0168.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma leo tarehe 25 Julai, 2022

- Rais amewasili katika viwanja vya mashujaa Dodoma.

- Gwaride la kumbukumbu ya siku ya Mashujaa limefanywa

- Viongozi wa dini mbalimbali wamepewa nafasi ya kufungua shughuli hii kwa maombi.

- Wimbo wa taifa umeimbwa

HOTUBA YA RAIS SAMIA
- Awali ya yote Tumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kujaalia nchi yetu kuwa na amani mpaka siku ya leo muhimu kwetu. Umuhimu wa siku hii ya leo unaonekana si hapa Dodoma tu lakini mikoa mengine yote ambayo leo hii inaadhimisha siku hii, leo hii na wakati huu.

- Mashujaa wetu walipambana katika nyanja mbalimbali
Mashujaa wetu walipambana katika nyanja mbalimbali dhidi ya ukoloni, ukandamizaji na uchokozi. Walipambana kifikra na kivitendo, kati ya vita vilivyopiganwa na Mashujaa wetu ni pamoja na vita vya majimaji, Vita ya pili ya dunia ambapo uwezo wa Mwenyekiti Mzee wetu ni ushahdi wa kwamba Mashujaa wetu walikuwapo na bado wapo.

Halikadhalika walipambana kwenye mapinduzi ya Zanzibar, vita vya ukombozi wa Afrika hasa Kusini mwa Afrika, vita ya Kagera na vita vya ukombozi mbalimbali ndani na nje ya bara la Afrika. Tunawakumbuka na kuwaenzi mashujaa wetu hawa waliojitoa muhanga wakilinda uhuru, uhai pamoja na heshima ya taifa na bara la Afrika.

- Maadhimisho haya si kwa waliopoteza uhai wao tu
Maadhimisho haya si kwa waliopoteza uhai wao tu lakini pia kwa wale waliopata ulemavu wa maisha na waliotoa michango yao kwa njia moja au nyingine. Kwa hali hiyo Watanzania hatuwezi kusahau mchango wa hali, mali na hali uliotolewa na Mashujaa hawa ndiyo sababu siku kama ya leo tunaadhimisha Mashujaa hawa.

Mtakumbuka kwamba kwa hivi karibuni hatukuweza kufanya maadhimisho haya kutokana na janga la Uviko-19 lililoukumba ulimwengu lakini leo Mungu ametujaalia tumeweza kukutana na tutazidi kukutana. Leo pia tunawakumbuka wazee wetu, viongozi wetu walioasisi taifa hili na ambao wametangulia mbele za haki hususani Mwalimu Nyerere na Hayati Karume pamoja na wengine walioshirikiana nao na ambao walikuja kuyaendeleza baada yao. Michango yao hiyo ndiyo imeifanya izidi kujijengea heshima na kutambulika katika mataifa mbalimbali duniani kote.

- Makao makuu ya nchi ni Dodoma hakuna kurudi nyuma
Ni furaha kwamba maadhimisho haya yanafanyika Dodoma makao makuu ya nchi katika uwanja ambapo mwaka 2016 wakati wa maadhimisho haya Hayati Magufuli alitangaza uamuzi wa kishujaa kuhamia Dododma. Napenda kutumia fursa hii kutangaza kuwa serikali imedhamiria kwa dhati kuendeleza uamuzi ule kama sehemu moja wapo ya kuenzi maono ya shujaa wetu Hayati Julias Kambarage Nyerere.

Naomba mniruhusu nirudie wito wa Hayati Magufuli kwamba Makao Makuu ya Tanzania ni hapa jijini Dodoma na hakuna kurudi nyuma. Jitihada za kujenga jiji la makao makuu ya taifa zimeendeezwa kama mnavyojionea wenyewe. Mpaka sasa ujenzi wa awamu ya pili pale Mtumba au Magufuli City unaohusisha majengo ya kudumu yatakayohusisha watumishi wote bado unaendelea.

- Dodoma pajengwe mnara wenye hadhi ya Makao Makuu ya Nchi
Waheshimiwa viongozi ndugu Wananchi, kutokana na umuhimu wa siku hii nataka kupendekeza kwamba kwakuwa jiji la Dodoma linakua na uwanja huu tuko katikati ya mji nipendekeze kwa Waziri Mkuu ofisi yako pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kutafuta eneo kubwa kujenga mnara mkubwa wenye hadhi ya Makao Makuu ya nchi kwa gharama zitakazostahimilika.

Aidha, ameongeza amependekeza Ofisi ya Waziri Mkuu na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutengeneza utaratibu wa maadhimisho yenye gharama nafuu zaidi.

Mwisho, Rais Samia amemaliza kwa kuwahimiza Wananchi Juu ya chanjo ya Uviko-19 pamoja na kuhimiza suala la sensa ifikapo mnamo Agosti 23.

Nani amewapa TFS Mamlaka ya Kujenga Makao Makuu yao Mwanza wakati Makao Makuu ya Nchi ni Dodoma?​

406B0CF8-D648-497C-946C-C1C98D6EDAE7.jpeg
 
Back
Top Bottom