Rais Samia Kuongoza Siku ya Mashujaa Julai 25 Mkoani Dodoma

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,505
3,038

Rais Dkt Samis Suluhu kuwa mgeni rasmi katika Kilele cha Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Siku ya Mashujaa Julai 25, 2023.

Maadhimisho hayo yatafanyika katika uwanja mpya wa kudumu wa Mashujaa uliopo katika eneo la Mji wa Serikali, Mtumba, mkoani Dodoma. Mkuu wa Mkoa huo, Rosemary Senyamule, aliyasema hayo jana wakati
akizungumza na wanahabari. Alisema kilele cha siku hiyo kitatanguliwa na uwashaji Mwenge wa Mashujaa saa
6:00 usiku wa Julai 24, 2023 kuamkia Julai 25, 2023.

"Nimepewa heshima ya kuwasha Mwenge huo kwa niaba ya wanaDodoma, nachukua fursa hii kumshukuru na kuompongeza Rais Dkt. Samia na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Usalama kwa kuibua wazo, kutoa maelekezo ya kutafuta eneo kubwa la kudumu kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya Mashujaa," alisema.

Pia alimpongeza Rais Dkt. Samia kwa kuwezesha upatikanaji fedha za kujenga Mnara wa Mashujaa na kulisimamia wazo lake hadi limefanikiwa.

Pamoja na hayo, Senyamule alisema maandalizi ya maadhimisho hayo yamekamilika kwa asilimia 100 na kuwakaribisha viongozi na wananchi wote wa Mkoa wa Dodoma, nje ya Mkoa huo kuungana na wana Dodoma kuadhimisha siku hiyo muhimu.

"Pia nawaalika kushiriki nasi katika hafla ya uwashaji mwenge wa Mashujaa tukio ambalo litahudhuriwa na Meya wa Jiji la Dodoma.

Tutumie Maadhimisho haya kumarisha umoja wa kitaifa, amani na utulivu ili muda mwingi utumike kubuni na kutekeleza kazi za kuleta maendeleo," aliongeza.​
 
Huyu mama huyu!!! Mungu ambariki sana, napenda sana namna yake ya kudeal na vinabo.......wala haangaiki nao; anapiga kazi tu.
 
NCHI YETU imechezewa sana.
Na INAZIDI kuchezewa mno.

"Mwalimu alimaliza ushairi wake kwa kusema ole wake Tanzania tusipoisaidia"

Jk nyerere
 
Back
Top Bottom