Rais Samia anamalizia miaka minne ya awamu ambayo kairithi, bado awamu yake ya sita mwaka 2025 mpaka 2035

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Mama Anamalizia miaka minne ya awamu ambayo kairithi kikatiba, bado awamu yake, awamu hii ya sasa yupo kwa niaba ya marehemu.

Mama anamalizia miaka 4 ya kipindi cha pili cha miaka 5 ya awamu ya 5. Akimaliza anaanza awamu yake ya sita mwaka 2025 yenye vipindi 2 vya miaka mitano mitano mpaka 2035. Jumla itakuwa kumi. Ukijumlisha na hii 4 mama tunaye sana tuu kwa miaka 14 jumla.

Kina Maria Nyerer bado wanadunda, Mke wa Mkapa yupi, Janeth nae bado anadunda......Nae mama atafika mbali tu, hivyo swala la kuishi sio la kuhofia sana maana ni wazi wanawake wengi wanaishi kuzidi wanaume.

Tanganyika + Zanzibar = Tanzania
 
Fikra pevu hapa sizioni, kumbuka wale ni wake wa marais walikua hawana mikikimikiki ya kimajukumu kama ya sasa kazi iendelee
 
Unatakiwa kusoma katiba upya. Lakini pia akitaka kumaliza miaka kidogo mbele anatakiwa kuwatii wakubwa zake mwanzo mwisho siku akienda tofauti utarudi hapa na uzi fofauti.
 
Unatakiwa kusoma katiba upya. Lakini pia akitaka kumaliza miaka kidogo mbele anatakiwa kuwatii wakubwa zake mwanzo mwisho siku akienda tofauti utarudi hapa na uzi fofauti.
Hii ni awamu ya tano au ya sita?
 
Mapuuzi ya CCM yalipoona Mbowe ni tishio yakaweka kigezo cha degree ili kumdhibiti huku yakijua hakuna kigezo kama hicho kwenye katiba, kwa hiyo msitegemee sana katiba inasema nini, mafia chama cha wahuni wa CCM kitaamua nani awe mgombea wao kwa vigezo vyao vya kipuuzi visivyofuata sheria
 
Kasome katiba vizuri
Katiba haina kitu kinaitwa "awamu", ni kwa mazoweza tu kuwa awamu ni serikali inayochaguliwa baada ya uchaguzi chini ya manifesto fulani; awamu inaendana na philosophy iliyoahidiwa kwa wananchi wakati wa uchaguzi.

Kiukweli mama alishauliwa vibaya sana kuwa aanze serikali yake mpya jambo ambalo siyo kikatiba; in fact kuna waliomshauri kuwa vunja baraza lote la mawaziri na kuunda jipya as if ameanza upya. Ila katiba inamtaka amalizie kipindi kilichoachwa na rais aliyefariki.

Inawezekana kabisa kuwa rais angefariki mwezi mmoja kabla ya kumalizia kipindichake, huwezi kusema kuwa makamu wa rais atavunja serikali na kuanza awamu yake mpya ya huo mwezi mmoja.

Papara alizoanza nazo baada ya kushika nchi zinasababisha watu wengine watafsiri matukio yote vibaya.
 
Mapuuzi ya CCM yalipoona Mbowe ni tishio yakaweka kigezo cha degree ili kumdhibiti huku yakijua hakuna kigezo kama hicho kwenye katiba, kwa hiyo msitegemee sana katiba inasema nini, mafia chama cha wahuni wa CCM kitaamua nani awe mgombea wao kwa vigezo vyao vya kipuuzi visivyofuata sheria
Mbowe hajawi kuzuiwa kugombania urais Tz
 
Mama Anamalizia miaka minne ya awamu ambayo kairithi kikatiba, bado awamu yake, awamu hii ya sasa yupo kwa niaba ya marehemu...
Tanzania + Zanzibar = Tanzania.

Tanzania + Zimbabwe = Tanzania.

5 + 1/4 = 6

Rais hutakiwa achaguliwe kwa kupigiwa kura japo CCM wameuondoa utaratibu huo wa kikatiba, hivi sasa Rais husimikwa.
 
Kweli hupo sahihi, nimependa na iwe hivyo! Aendele kutupa uhuru, asituteke, asitubambikie mikesi, awe mvumilivu kwenye siasa, nampongeza alipofikia kiasi chake, naamini likiisha swala Mbowe atakuwa vizuri zaidi!
 
Back
Top Bottom