Nimefuatilia kauli na Matendo ya rais Samia nimejiridhisha kwamba siyo mpenda demokrasia kama anavyojinadi majukwaani.
Amejigamba kwamba ana ngozi ngumu na kusema anaruhusu uhuru wa kusema, kukosoa na kujieleza. Kwa taarifa yako ndugu msomaji huyu mama hana ngozi ngumu kwa Mambo yasiyomuumiza tu. Mifano ipo mingi:
1. Aliwaasa wandishi wa habari kuwa "wasimparure".
2. Ndugai akiwa spika, alitoa maoni yake lkn bahati mbaya yakamparura mhe rais. Kilichompata Ndugai sote tunakijua.
3. Amekubali mazungumzo na CHADEMA ili kuleta maridhiano na yameanza kufanyika. Lakini matendo ya serikali yake hayaoneshi kama kuna kujali ama kuheshimu mazungumzo hayo. Tunayaona haya kwenye suala la wabunge 19 waliofukuzwa uanachama na Chadema.
Hapa ni dhahiri kwamba mama anataka maridhiano mdomoni tu lakini moyoni mwake ana ajenda ya siri. Siri yenyewe ni ama anafanya danganya toto (dangany wapinzani) au anatafuta kuaminiwa na mataifa wahisani.
5. Mhe Rais hata katika suala la Loliondo ameonesha jeuri ya hali juu sana. Achilia mbali asasi za kiraia na wanaharakati lakini hata wabunge na wananchi wa Loliondo wamepiga kelele sana kuhusu kupinga maamuzi ya kuwaondoa wamasai toka ardhi yao. Amekaa kimya na kuwapuuza.
Mwisho. Nawashuri chadema kujiondoa kwenye mazungumzo yanayoendelea kwani hayatazaa matunda yoyote. Wanachezeshwa ngoma wasiojua mwisho wake.