Rais Samia ana kwa ana na polisi Moshi

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
413
471
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufungua Kikao Kazi cha Maofisa Wakuu wa Jeshi la Polisi Tanzania kitachofanyika katika Shule ya Polisi, Moshi mkoani Kilimanjaro. Kikao hicho cha siku tatu kitahusisha Wakuu Waandamizi wa makao makuu, Makamanda wa Polisi mikoa na vikosi.

Akitoa taarifa hiyo msemaji wa jeshi la polisi nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi( SACP), David Misime amesema kikao kazi hicho kitaanza Agosti 30, 2022 hadi Septemba Mosi 2022.

Aidha SACP Misime alisema kuwa jeshi hilo kila mwaka hufanya kikao kama hicho kwa ajili ya kufanya tathmini ya utendaji wake kwa kipindi cha mwaka mmoja na kuona wapi Jeshi hilo limefanya vizuri na wapi halijafanya vizuri na sababu zake na kuweka mikakati mipya ya kutekeleza majukumu ya Jeshi la Polisi kwa ufanisi zaidi kwa mwaka unaofuata.

POLISI SAMIA.jpeg
 
Nadhani watajitahidi kuhakikisha wenye vitambi hawamsogelei Rais Samia.
 
Back
Top Bottom