Rais Samia amzawadia Gari Mama Kanumba

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,184
Reaction score
17,678
Katika kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemzawadia mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba gari jipya aina ya Harrier New Model.

Hatua hii imekuja kama ishara ya kuthamini mchango mkubwa wa marehemu Kanumba katika kukuza tasnia ya filamu nchini na kuenzi alama aliyoiacha kwenye sanaa ya Tanzania.

Zawadi hiyo ni jibu la ombi la Mama Kanumba kwa Rais Samia, ambapo alieleza changamoto ya usafiri inayomkabili kutokana na umri wake mkubwa.

Akishukuru kwa furaha, Mama Kanumba amempongeza Rais kwa moyo wa upendo na ukarimu, akibainisha kuwa usafiri huo utamsaidia kurahisisha shughuli zake za kila siku ambazo awali zilikuwa ngumu kwake.
Your browser is not able to display this video.
 
Aache kutumia kodi za watu kihisia

Yeye hana hela pesa ni za watu ajue nafasi yake
 
Plot za kitoto kabisa. Hahitaji hakili nyingi ilikuwa Rais wa Tanganyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…