Rais Samia amteua Prof. Said Shehe Aboud kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,830
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Said Shehe Aboud kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).

Prof. Aboud ni Profesa Mshiriki na Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Fedha na Utawala, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dar es Salaam.

Prof. Aboud anachukua nafasi ya Prof. Yunus Daud Mgaya ambaye amemaliza muda wake mwezi Septemba, 2022.

Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Oktoba, 2022.

2F37E88B-D0B9-4DDA-B7B0-34BF6FAFEEC4.jpeg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Said Shehe Aboud kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).

Prof. Aboud ni Profesa Mshiriki na Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Fedha na Utawala, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dar es Salaam.

Prof. Aboud anachukua nafasi ya Prof. Yunus Daud Mgaya ambaye amemaliza muda wake mwezi Septemba, 2022.

Uteuzi huu umeanza tarehe 19 Oktoba, 2022.

1666263464978.png
 
Attachments

  • UTEUZI NIMR.pdf
    98.8 KB · Views: 5
Kongole kwake. Akapige kazi asisahau nimrkafu na ile mitambo ya kujifulizia.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mnaoangalia dini kumbukeni kwamba hii taasisi nyeti inahitaji vichwa hasa bila kujali dini ili kuokoa jahazi la taifa letu. Mimi namshukuru sana Rais kwa kumteua mtu sahihi kwa mustakhabali wa taifa letu.
 
Mbona ameicha university teaching hospital Mloganzila? Tumueleweja?Angekuwa mtanzania wa kwanza kuanzisha university teaching hospital.
 
Wafia dini acheni upuuzi wenu..acheni watu wapige kazi kwa manufaa ya nchi yetu na maendeleo ya wanachi kwa ujumla.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mnaoangalia dini kumbukeni kwamba hii taasisi nyeti inahitaji vichwa hasa bila kujali dini ili kuokoa jahazi la taifa letu. Mimi namshukuru sana Rais kwa kumteua mtu sahihi kwa mustakhabali wa taifa letu.
Kichwa kuliko nani ?.....huijui MUHAS...kwa wanaojua wanaelewa.
 
Back
Top Bottom