Rais Samia amepunguza changamoto za elimu

kalacha mateo

Senior Member
Sep 27, 2021
118
237
Ni siku 702 tangu Rais Samia Suluhu akabidhiwe majukumu ya kuliongoza Taifa la Tanzania. Katika kipindi kifupi cha uongozi wake ameonyesha utayari wake wa kupunguza au kumaliza changamoto za elimu nchini. Miongoni mwa changamoto kubwa zilizokuwepo ni Upungufu wa madarasa na samani, nyumba za walimu, vyoo, mitaala ya elimu pamoja na uhaba wa watumishi.

Katika siku 702 madarasa zaidi ya 23,000 yamejengwa nchi nzima pamoja na kuanzishwa kwa shule mpya ili kuwawezesha wanafunzi kusoma karibu, Nyumba za walimu zimejengwa, ajira zaidi ya 16,000 zilitolewa lakini kubwa ni kuendelea cha mchakato wa upitiaji na uboreshaji wa mitaala ya elimu nchini.

Kwa upande wa elimu ya juu Rais Samia Suluhu amejitahidi kuongeza bajeti ya mkopo kwa elimu ya juu ili wanafunzi wote wenye uhitaji waweze kupata, Lakini pia kuanzishwa kwa SAMIA SCHOLARSHIP imekua msaada kwa watoto wa kitanzania wenye ndoto kubwa.

Rais Samia amedhamiria kuboresha elimu nchini ili kupunguza utofauti wa mazingira ya kujifunzia na kuwapa hamasa watoto kupenda kujifunza zaidi.

1676902259437.png
 
Hizo ajira za ualimu 160000,zipo wapi?
Au aliajiri lini hizo ajira,nikimaanisha upande wa ualimu.
 
Back
Top Bottom