Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 2,210
- 4,712
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani amekutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara maarufu kutokea Nigeria Alhaji Aliko Dangote
Mazungumzo hayo muhimu yalifanyika leo Mei 24, 2021 Ikulu Jijini Dar es salaam
Alhaji Dangote ni mfanyabiashara mkubwa duniani aliyewekeza nchini Tanzania kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Kiwanda cha kuzalisha Saruji Mkoani Mtwara
Alhaji Dangote amemshukuru sana Rais Samia kws kuboresha mazingira ya Uwekezaji nchini na ameahidi kuwa ataendelea kuwekeza Tanzania kwenye maeneo tofauti ikiwamo ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea
Rais Samia aliahidi kuwa Serikali yake itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa faida ya pande zote na alwaagiza Mawaziri husika kushughulikia changamoto zinazoikabili Kampuni ya Dangote
Taarifa zaidi kutolewa na Mamlaka husika
Kazi Iendelee