Rais Samia akutana na kufanya mazungumzo mfanyabiashara Alhaj Aliko Dangote

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,191
4,656

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassani amekutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara maarufu kutokea Nigeria Alhaji Aliko Dangote

Mazungumzo hayo muhimu yalifanyika leo Mei 24, 2021 Ikulu Jijini Dar es salaam

Alhaji Dangote ni mfanyabiashara mkubwa duniani aliyewekeza nchini Tanzania kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Kiwanda cha kuzalisha Saruji Mkoani Mtwara

Alhaji Dangote amemshukuru sana Rais Samia kws kuboresha mazingira ya Uwekezaji nchini na ameahidi kuwa ataendelea kuwekeza Tanzania kwenye maeneo tofauti ikiwamo ujenzi wa Kiwanda cha Mbolea

Rais Samia aliahidi kuwa Serikali yake itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini kwa faida ya pande zote na alwaagiza Mawaziri husika kushughulikia changamoto zinazoikabili Kampuni ya Dangote

Taarifa zaidi kutolewa na Mamlaka husika

Kazi Iendelee
D1.jpg

D2.jpg


Dangote.jpg
 
Afadhali, cement itashuka bei, maana walimfanyia figisu mwanzoni, wakati ule cement ya dangote imeshamili mtaani, tulinunua mfuko wa saruji hadi Tsh 10,000 kutoka 15000.

Dikteta alimfanyia figisu za kutisha
Sema Dangote naye ni mtu asiweza kabisa figisu. Biashara zake nyingi ustawi wake unategemea sana kulelewa na serikali. Hata Nigeria iko hivyo.

Ingawa ndio kazi ya serikali kulea sekta binafsi lakini ukipata mtawala roho mbaya kama Magu mambo yanayumba sana.
 
Sema Dangote naye ni mtu asiweza kabisa figisu. Biashara zake nyingi ustawi wake unategemea sana kulelewa na serikali. Hata Nigeria iko hivyo.

Ingawa ndio kazi ya serikali kulea sekta binafsi lakini ukipata mtawala roho mbaya kama Magu mambo yanayumba sana.
Sasa figisu za nini kama kodi anawalipa? muacheni afanye kazi kwa amani, hii mikutano ya aina hii ndio inafungua njia kwa wawekezaji wengine kuwa na amani ya kuja kuwekeza Tanzania.
 
Madereva wake wameajiriwa kama contractors badala ya kupewa full time employment, hilo linawakosesha haki zao za kisheria nyingi ikiwemo uhakika wa kazi zao, kuingizwa kwenye pension schemes, kwenda likizo ya malipo, sick pay na faida wanazopewa wafanyakazi wenzao; bila ya kusahau kupoteza PAYE za TRA.

Hayo ndio mambo ya kumkubusha na yeye. Juzi tu madereva wa Dangote walikuwa kwenye mgomo kisa kuchukuliwa kama vibarua wakati watu wanafanya kazi sehemu moja zaidi ya miaka miwili, hakuna madereva wenye mkataba wa kudumu na kampuni; kuna middleman anaewapa ajira na kuwapunja kwa kuwakata kilicho chao, bila ya ulazima.

Wafanyabiashara sio kuja kuomba mazingira mazuri tu, bali na wao waweke mazingira mazuri kwa waajiriwa, sakata lote la mgomo limeenda karibu week nzima Mhagama kama alikuwa aoni vile na nina uhakika wale madereva madai yao ya msingi ayajatatuliwa.
 
Wawekezaji wanazidi kumiminika Tanzania kufuatia uwepo wa mazingira rafiki na ya kuvutia yatakayofaidisha pande zote mbili mwekezaji mgeni na nchi ya Tanzania.

Juzi pia wawezeshaji European Business Group Tanzania forum European Union Business Group Tanzania – European Union Business Group Tanzania walifanikisha kongamano la European Investors Dialogue Tanzania walikuwa na kikao na wizara mbalimbali na kongamano la kujadili uwekezaji Tanzania
23 May 2021
Majadiliano yamefanyika baina ya Jumuiya ya Wawekezaji kutoka Ulaya na Serikali ya Tanzania juu kufanya uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini. Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia sekta ya Mifugo, Prof. Elisante Ole Gabriel amesema wadau hao wa umoja wa Ulaya kutoka nchi 28 wanatarajia kufanya uwekezaji katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya Mifugo ambapo Tanzania inakamata nafasi ya pili kwa wingi wa Mifugo barani Afrika ikifuatiwa na Ethiopia.



Mambo yanazidi kunoga ktk awamu ya sita upande wa kuwapa imani, mazingira na sera za kiushawishi za uwekezaji pamoja na diplomasia ya uchumi kuanza kuzaa matunda.
 
Back
Top Bottom