Rais Samia akiwa katika ziara Wilaya ya Kusini Unguja, Zanzibar, leo Agosti 29, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara Wilaya ya Kusini Unguja tarehe 29 Agosti, 2023 visiwani Zanzibar.

Rais Samia amezindua madarasa Mapya 6 Buyuni Shule ya Msingi pamoja na kuzindua holi la Mitihani na Shughuli zingine za watu wa Buyuni ikiwemo Harusi.

Tamasha la Kizimkazi liliasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, likiwa na lengo la kudumisha mila na desturi ya Wananchi wa Kizimkazi limetajwa kuwa kichocheo kikubwa cha utalii Mkoa wa Kusini Unguja.

Tamasha hilo kwa mwaka huu 2023 linafanyika Paje mkoani Kusini Unguja kuanzia Agosti 26 hadi 31, 2023 ambapo lilifunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi.

Rais Samia anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa tamasha hilo katika kilele cha tamasha hilo Agosti 31, 2023 ambapo atafungua miradi mbalimbali mkoani humo pamoja na kutoa misaada kwa wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 80 na watoto yatima.
 
Pangeni mtakavyouza Tanganyika yetu
 
Back
Top Bottom