Rais Samia akitaka akumbukwe kwenye utumishi wake basi asiendeshe uchaguzi bila Tume Huru za Uchaguzi Zanzibar na Tanganyika

Unitman

JF-Expert Member
Jul 14, 2021
256
354
Habari wanajamvi,

Huyu mama amekuwa anaupiga mwingi mpaka unamwagika, lakini akitaka tumkumbuke katika utumishi wake asithubutu kutumia fedha hata senti 5 kuendesha uchaguzi kiiinimacho bila tume huru ya uchaguzi Zanzibar na Tanganyika.

Tukubaliane kabisa na wapinzani mkubali hizo fedha tununue vitanda vya kujifungulia akina mama na maisha yaendelee mpaka pale tutakapopata marefa wa ukweli.

Nawasilisha.
 
Habari wanajamvi,

Mama akitaka tumkumbuke katika utumishi wake asithubutu kuendesha uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi Zanzibar na Tanganyika.

Nawasilisha.
Naunga mkono hoja, tena uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ufanyike siku moja na kusimamiwa na Tume huru na Shirikishi ya Uchaguzi.
P
 
Tume huru haiwezi kupatikana kwa katiba mbovu iliyopo. Tume huru itapatikana endapo katiba bora yenye mizizi ya uhuru wa tume itaundwa.

Shina la mchungwa halafu unaomba matunda yawe maembe??

Mpk pale tutakapochapana na kuuana ndiyo tume katiba bora na tume huru vitapatikana.
 
KIAPO CHA SIRI CHA WIZI

"Kipindi cha uchaguzi mkuu, ninaahidi kucheza michezo yote, iwe halali ama haramu, iwe misafi ama michafu, ili kuhakisha kuwa chama chetu CCM hakifii mikononi mwangu wala kuondolewa madarakani. Eeh! Grand Master, naomba unisaidie."
 
Habari wanajamvi,

Huyu mama amekuwa anaupiga mwingi mpaka unamwagika, lakini akitaka tumkumbuke katika utumishi wake asithubutu kutumia fedha hata senti 5 kuendesha uchaguzi kiiinimacho bila tume huru ya uchaguzi Zanzibar na Tanganyika.

Tukubaliane kabisa na wapinzani mkubali hizo fedha tununue vitanda vya kujifungulia akina mama na maisha yaendelee mpaka pale tutakapopata marefa wa ukweli.

Nawasilisha.
Mkuu unashauri 'TUME HURU' iundweje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom