Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,506
- 113,626
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa.
Hili ni swali la pendekezo uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani, usogezwe na kufanyika 2025, ufanyike siku moja na uchaguzi mkuu wa 2025, na usimamiwe na Tume huru ya uchaguzi, by that time pia ile dhulma ya kipengele batili ndani ya Katiba yetu iwe imeondolewa na sheria ya uchaguzi kurekebishwa ili haki za Watanzania kuchagua na kuchaguliwa, zilizoporwa kiubatili, zirejeshwe?
Nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili, baada ya kumsikia Rais Samia, akikizungumzia kitu fulani alicho kiita kivumbi hivyo amemteua mtu mwenye kifua pale Tamisemi!
Msikilize Rais Samia
Japo hapa hakikusemwa ni kivumbi cha nini, ila waelewa tumeisha elewa hiki ni kivumbi cha uchaguzi wa serikali za mitaa!.
Ushauri huu wa leo, niliwahi kuutoa kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019, nilitoa ombo maalum na nilishauri Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa!
Katika bandiko hilo, nilishauri
Hivyo sasa nauliza na kushauri, mnaonaje kama uchaguzi wa Serikali za Mtaa Ufanywe Siku Moja na Uchaguzi Mkuu usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi?
Naombeni tusilete excuse ya chaguzi 4 kufanyika siku moja, yaani uchaguzi wa Rais, Mbunge, Diwani, Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa, wenzetu Zanzibar wanafanya chaguzi 5 kwa siku moja, Rais wa JMT, Rais wa Zanzibar, Mbunge wa Bunge la JMT, Mwakilishi wa BLW, na Shehia!.
Hili likifanyika, Rais Samia na taifa Letu litabarikiwa, na viongozi wetu wabarikiwa, na sisi wananchi wa kawaida pia, tutabarikiwa na kupata neena na mafanikio makubwa, na nchi yetu kupata ustawi mkubwa wa kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali

Nikimnukuu Rais Samia "mwakani kuna kivumbi, mimi nakujua, najua unaweza, kivumbi kile kinafanana na kifua chako, najua unaweza, mwakani ni kazi kazi, ili tu sail vizuri".
Japo hapa hakikusemwa ni kivumbi cha nini, ila waelewa tumeisha elewa hiki ni kivumbi cha uchaguzi wa serikali za mitaa!.
Ushauri huu wa leo, niliwahi kuutoa kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019, nilitoa ombo maalum na nilishauri Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa!
Katika bandiko hilo, nilishauri
Mene Mene Tekeli na Peresi imeisha wahi kutushukia, tusikaribishe tena Mene Mene!.Wanabodi,
Tanzania sio nchi ya watu fulani tuu au chama fulani tuu, Tanzania ni nchi ya Watanzania wote, wa vyama vyote, wa dini zote, wa makabila yote, wa jamii zote, wa jinsia zote, wa rangi zote, wa hali zote za maisha, matajiri na masikini na Watanzania wa circumstances zote.
Mimi nikiwa mwandishi wa habari, nimeshuhudia chaguzi zetu zote za vyama vingi, zimekuwa zikiendeshwa kwa mtindo wa "Mutatis Mutandis"
Hivyo sasa tunapokwenda kwenye uchaguzi, naomba kutoa ombi maalum na angalizo muhimu kwa wahusika wakuu wa uchanguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, uendeshwe kwa kutumia kanuni ya Kilatini ya "ceteris paribus" na sio kutumia zile kanuni zetu za kawaida za "Mutatis Mutandis"!.
Nimesikia sauti, "voices from within" kuwa tukiendelea kufanya chaguzi zetu kwa Mutatis Mutandis, kuna janga fulani litatokea.
Wahusika wakuu wa uchanguzi huu, wakikubali uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2024 na uchaguzi Mkuu ujao wa 2025 kuendeshea kwa ceteris paribus , taifa Letu litabarikiwa, na viongozi wetu wabarikiwa, na sisi wananchi wa kawaida pia, tutabarikiwa na kupata neena na mafanikio makubwa, na nchi yetu kupata ustawi mkubwa wa kisiasa, kiuchumi na kijamii, lakini tukiendelea kutumia ule mtindo wetu wa mutatis mutandis, taifa tutalaaniwa na viongozi wetu watalaaniwa na kuadhibiwa!, and you never know ni adhabu gani viongozi wetu wakuu wataadhibiwa!.
Mungu Mbariki Rais Samia na watendaji wake wapate uwezo, watumie "Ceteris Peribus" kwa vyama vyote na sio kuendeleza "Mutatis Mutandis"
Mungu ibariki Tanzania.
NB. Sijaweka ufafanuzi wa maneno "Ceteris Peribus" na "Mutatis Mutandis" sio kwa bahati mbaya, nimefanya hivi kwa makusudi mazima, kwa sababu ujumbe huu ni ujumbe maalum na mahsus kwa watu maalum na mahsus ambao mimi nawajua huwa wanatembelea sana jf, kwa vile watu hao, wanayajua maneno hayo. Wengine wasio husika hayawahusu, hivyo sikufafanua ili ujumbe huu uwafikie walengwa tuu.
Hata Mungu alipotaka kumfikishia ujumbe maalum mfalme Belshaza, alimtumia kiganja cha mkono kikaandika kwenye ukuta wake, "Mene Mene Tekeli na Peresi", tukiendelea kufanya chaguzi zetu kwa Mutatis Mutandis badala ya kutumia
Ceteris Paribus, then kuna siku Mene Mene Takeli na Peresi itakuja kuishukia Tanzania na kumshukia kiongozi wetu!.
Nawatakia Weekend Njema,
Paskali.