Rais Samia akishiriki Maadhimisho ya Sikukuu ya Nanenane Kitaifa, Agosti 8, 2025 Dodoma

Rais Samia akishiriki Maadhimisho ya Sikukuu ya Nanenane Kitaifa, Agosti 8, 2025 Dodoma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
4,783
Reaction score
14,975
Rais Samia Akishiriki Maadhimisho ya Sikukuu ya Nanenane Kitaifa katika Viwanja vya Nanenane Jijini Dodoma, leo tarehe 8 Agosti, 2025.



View: https://www.youtube.com/live/jQHC1KDAtsY?si=wJAJj3luERusy52n
WhatsApp Image 2025-08-08 at 14.31.52_e359ea6b.jpg


=============

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule, akiwahutubia wakazi wakati wa kilele cha maadhimisho ya Nanenane mkoani Dodoma, M amesema kuwa Dodoma na Singida sasa ni miongoni mwa maeneo yenye kilimo halisi, na si hadithi tu.

“Baada ya kuweka miundombinu mizuri, tumehamasisha wakulima na wananchi wetu kutumia fursa hizi muhimu. Uchumi wa Dodoma unaimarika kwa kasi,”

Ametoa takwimu zinazothibitisha maendeleo hayo kwa kusema pato la mkoa wa Dodoma (GDP) liliongezeka kutoka trilioni 4.5 mwaka 2020 hadi trilioni 6.4 mwaka 2024, ambapo asilimia 39 ya pato hilo linatokana na kilimo.
WhatsApp Image 2025-08-08 at 14.31.55_28930432.jpg

WhatsApp Image 2025-08-08 at 14.31.53_2cb153ef.jpg
Aidha, amebainisha kuwa kanda ya kati ina mazao ya kimkakati kama alizeti kwa ajili ya mafuta, mtama unaofaa kwa hali ya hewa, zabibu, mifugo ikiwemo mbuzi na ng’ombe. Pia amezungumzia zao jipya la tufaha ‘apple’ ambalo limeanza kupandwa Singida na linaonesha maendeleo makubwa kama zao la kimkakati.

“Mheshimiwa Rais, wewe umekuwa ukisema Tanzania italisha Afrika na sisi tunakuhakikishia kwamba kanda yetu ni sehemu ya kulisha Afrika,” amesema Senyamule.

======================================
 
Back
Top Bottom