Rais Samia aipongeza ATCL kwa kuchanja mbuga, Kenya sasa ni Tshs 770,000 tu

Kama mambo ndio haya basi Tanzania kama kuna wakati tumepata Rais bora na wa kweli nadhani ni sasa,Tufanye kazi kwa bidii sana,

Hakika huyu Mama ni Mpango wa Mungu,

#WATANZANIA TUFANYE KAZI KWA BIDII
 
" Kwa mwendo huu Tanzania tutafika tunakotaka kwenda tena kwa kuwahi sana, Hongera Mama Samia, Watanzania tuko nyuma yako We chapa kazi achana na Wasio na jema "
 
Rais wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameipongeza ATCL kwa kupanua biashara ya usafiri na usafirishaji ya anga, hasa baada ya ATCL kuongeza safari zake za kibiashara kwa karibu mara tatu.

Rais Samia ameipongeza zaidi ATCL kwa kurejesha Safari za Kenya Nairobi tena kwa gharama ndogo ya KSh37,525 au $334 sawa na TZS 770, Two ways.

Lazima tufahanu kuwa mwendo huu wa kasi wa ATCL ni kabla ya ujio wa ndege mpya tano za kisasa zinazotarajiwa kuingia nchini ndani ya kipindi kifupi kijacho, hakika hakuna kama Rais Samia.

Naipongeza ATCL kwa kupanua huduma za safari za ndege zake ndani na nje ya nchi ikiwemo kurejesha safari za Dar es Salaam - Nairobi, Kenya zitakazoanza Novemba 26, 2021. Ni matarajio yangu kuwa tutaendelea kuiunga mkono ATCL ili ikue zaidi na kutimiza matarajio ya Watanzania.
View attachment 2048429

Hizi nauli wanapaswa kuziangalia sana, hii ni almost nauli ya kwenda Dubai, what is this???

Yaani kweli hiyo pesa yote wanaona ndio ya kupongezwa kweli wakati the price is not worthy of competition?

Nchi ya ajabu sana
 
Back
Top Bottom