Rais Samia aipa Mitaji ya Bilioni 208 Benki ya Maendeleo ya Kilimo

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,475
2,927
Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ametajwa kuwa wa kiongozi wa mfano katika kuipaisha na kuiletea mageuzi makubwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) ikiwemo kuipa mtaji wa bilioni 208 kuwezesha kujiendesha kiufanisi.
Imesema mtaji huo umeiwezesha benki hiyo kutengeneza faida na kukuza mtaji wake hadi kufikia sh. bilioni 302.5 sawa na ongezeko la asilimia 404.17.

Akizunzumza jana Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Frank Nyabundege alisema benki hivo imekuwa na mafanikio makubwa toka ilipoanzishwa mwaka 2015 na kutoa mchango mkubwa kwa wakulima, kampuni zao kupitia mikopo wanayopewa. Mkurugenzi Mkuu Nyabundege alisema katika kikao hicho kilichoitishwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kuwa benki hiyo imekuwa na mchango mkubwa kwa wakulima kutokana na malengo makubwa aliyokuwa nayo Rais Dk. Samia.

Alisema benki imekuwa na mafanikio makubwa ikiwemo mikopo yake kuwa na riba ndogo chini ya asilimia 10, kutoa mikopo ya muda mfupi(chini ya miaka miwili) muda wa kati( chini ya miaka miwili hadi miaka 5), muda mrefu ( kati ya miaka mitano hadi miaka 15) kwa njia ya moja kwa moja.

"TADB imechagiza pia utoaji wa mikopo kupitia benki washirika kwa kutoa dhamana kupitia mfuko wa wakulima wadogo unaochagiza benki na taasisi za fedha kutoa mikopo kwa wakulima" alisema.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu huyo, benki imepata mafanikio makubwa ya faida kutoka milioni 449.7 hadi bilioni
11.38 sawa na ongezeko la asilimia 2,438.9 ambapo kukua kwa faida hiyo kumechagizwa na kukua kwa mapato ya benki.

"Tumeanzisha huduma mbalimbali ikiwemo dawati maalumu la mikopo ya wavuvi, kuanzisha programu maalumu ya sekta ya maziwa, kuendeleza wakulima wadogo na kuleta mageuzi katika mazao ya kimkakati" alisema

Kwa upande wake, Msajili Mkuu wa Hazina; Nehemiah Mchechu alisema taasisi na mashirika ya umma 248 yamepata mafanikio makubwa katika kipindi cha serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt Samia.

Alisema wamefikia malengo hayo na ametangaza kuanzia sasa mashirika na taasisi zote za serikali zitaanza kutoa taarifa za mafanikio yao kwa umma.

"Hili 'ni agizo kwa kuwa sisi Kama serikali tunamashirika mengi na wakati mwingine tuna hisa maeneo mengi lazima watanzania wayajue mashirika yao. Hili tumenuia kwa kiwango kikubwa kuonyesha mafanikio hayo" alisema.
Mchechu alisema malengo ya serikali ni kuwa taasisi au mashirika makubwa yanayofanya biashara na yenye mafanikio, kwenda huko tumechukua hatua madhubuti kuhakikisha malengo hayo yanafikiwa.

"Tusipochukua hatua tutashindwa kufika mbali zaidi na tumeamua kubadilika na kuanza kufanya kazi ya kutoa taarifa na ushirikiano wa pamoja wa mashirika hayo na vombo vya habari kupitia kwa wahariri na waandishi wa habari" alisema.

Hivyo, alisema kuanzia sasa kila shirika la umma au taasisi inapaswa kutoa taarifa kwa umma za mapato yao kwa umma kuona namna serikali inavyoendesha mashirika hayo.
 
Wanaweka hapo waje kuzikwapua wakati wa Uchaguzi mkuu
 
Hizi pesa yeye katoa wapi?
 
Inamaana walishatathmini kwanini uwekezaji wa awali ulifel na Sasa fedha iliyowekezwa italeta mafanikio?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom