Rais Samia afanya ziara ya Kiserikali nchini Msumbiji, ahimiza kutumia fursa za kibiashara zilizopo katika nchi hizo mbili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara ya Kiserikali nchini Msumbiji leo tarehe 21 Septemba, 2022.

Rais Samia ametaka ushirikiano wa ulinzi baina ya nchi hizi mbili hasa ule wa mipaka ulio anzishwa tangu miaka ya 1980 uendelezwe hasa kwenye kipindi hiki muhimu cha kupambana na ugaidi.

Amegusia pia jitihada za kuongeza ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Msumbiji, pia namna bora ya kutumia fursa za kibiashara zilizopo baina ya nchi hizi mbili.

Upande wa elimu wameafikiana kubadilishana wanafunzi, aidha lugha ya kiswahili kwa sasa itapewa kipaumbele nchini Msumbiji.

Kupitia safari hii, Rais Samia anaamini ukurasa mpya wa ushirikiano mwema kati ya Msumbiji na Tanzania utafunguka.
IMG_20220921_212745_692.jpg

Kujua ziara nyingine za Rais tangu aingie madarakani soma Safari/Ziara za nje ya Nchi za Rais Samia Suluhu tangu awe Rais wa Tanzania 19 Mar 2021
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara ya Kiserikali nchini Msumbiji leo tarehe 21 Septemba, 2022.

Rais Samia ametaka ushirikiano wa ulinzi baina ya nchi hizi mbili ulio anzishwa tangu miaka ya 1980 uendelezwe hasa kwenye kipindi hiki muhimu cha kupambana na ugaidi.

Amegusia pia jitihada za kuongeza ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Msumbiji, pia namna bora ya kutumia fursa za kibiashara zilizopo baina ya nchi hizi mbili.

Upande wa elimu wameafikiana kubadilishana wanafunzi, aidha lugha ya kiswahili kwa sasa itapewa kipaumbele nchini Msumbiji.

Kupitia safari hii, Rais Samia anaamini ukurasa mpya wa ushirikiano mwema kati ya Msumbiji na Tanzania utafunguka.

Asante kwa taarifa.
Wenzetu Wachina, hata kama wanazungumza kiingereza, wakihutubia popote duniani, kamwe hawatumii lugha za watu, wanahutubia kwa Kichina na kuwa wakalimani!.
Nashauri Mama Samia akifanya ziara popote Africa, ahutubie kwa Lugha ya Kiswahili, na kuwapatia wakalimani.
Msumbiji lugha yao ya taifa ni Kireno, hakuna sababu ya rais wetu kuhutubia kwa kuzungu, mfasiri atafsiri kwa Kireno, halafu sisi tutafsiriwe Kiswahili.
P
 
Hatari sana nasikia akitoka hapo msumbiji ziara ya siku 3 anaenda NEW YORK kwa ziara ya siku 4...

Kweli huyu mfujaji.
Hapo tumepigwa mkuu hadi miaka yake 10 iishe tutakuwa tuna vi biongo Kwa uzito wa tozo huku zikitumiwa Kwa nauli za kupigia misele.
 
Asante kwa taarifa.
Wenzetu Wachina, hata wanazungumza kiingereza, wakihutubia popote duniani, kamwe hawatumii lugha za watu, wanahutubia kwa Kichina na kuwa wakalimani!.
Nashauri Mama Samia akifanya ziara popote Africa, ahutubie kwa Lugha ya Kiswahili, na kuwapatia wakalimani.
Msumbiji lugha yao ya taifa ni Kireno, hakuna sababu ya rais wetu kuhutubia kwa kuzungu, mfasiri atafsiri kwa Kireno, halafu sisi tutafsiriwe Kiswahili.
P
Wewe umesomea sheria uliisoma kwa lugha gani?je mahakamani inatumika lugha gani?madaktari wanatumia lugha gani?
 
Kumekucha alikuwa kapumzika haya mambo. Niliju lazima aungie nchi nyingine
 
Professional issues inaruhusiwa kutumia technical language inaruhusiwa.
P
Kwa mantiki hiyo unataka watanzania wasome Lini technical language Ili waweze kuwa professional iwapo mnakuza Kiswahili kwa walala hoi na Watoto wenu wapo Feza boys?
 
Attachments

  • B0751E8A-DCD1-4750-839B-3514CC568671.jpeg
    B0751E8A-DCD1-4750-839B-3514CC568671.jpeg
    21.4 KB · Views: 4
Back
Top Bottom