Rais Samia aahidi Chuo Kikubwa cha TEHAMA

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Rais Samia Suluhu Hassan amesema TEHAMA ina nafasi kubwa katika maendeleo na Tanzania haiko nyuma, inajipanga kujenga chuo kikubwa cha TEHAMA

Amesema hivi karibuni, Instagram, Facebook na WhatsApp zilipotea kwa saa saba na mmliki akapata hasara ya Tsh. Trilioni 15 ambapo kuna uwezekano wa watanzania pia walipata hasara

Kwa sababu hiyo ametafakari kama mitandao hiyo ingepotea kwa siku nzima, ambapo amesema Tanzania imeamua kujiimarisha kimiundombinu ili kuikuza TEHAMA
 
Karibu kila chuo kinatoa kozi za tehama, binafsi Naona uwekezaji WA Research and Development ndilo la kuipa kipaumbele na sio kujenga chuo kingine. R&D ndio chanzo cha innovation na kukua kiteknolojia.

Tujifunze Kwa nchi kama Taiwan walivyopiga hatua kwenye Nyanja ya electronics(semiconductor) industry.
 
Ikulu moja wapo igeuzwe iwe chuo kikuu cha TEHAMA ni aibu nchi masikini kuwa na ikulu mbili
 
Karibu kila chuo kinatoa kozi za tehama, binafsi Naona uwekezaji WA Research and Development ndilo la kuipa kipaumbele na sio kujenga chuo kingine. R&D ndio chanzo cha innovation na kukua kiteknolojia.

Tujifunze Kwa nchi kama Taiwan walivyopiga hatua kwenye Nyanja ya electronics(semiconductor) industry.
RnD kwa mazingira gani?

Namshauri rais aanza na mambo rahisi kama kurekebisha sheria ambazo zinaturudisha nyuma. Kuna sheria zinapingana na National ICT Policy. Hili ni jambo linalohitaji utashi tu. Then tunaweza kufikiria makubwa mengine.

Mh. Rais ajue kuwa Watanzania hawajashindwa kutengeneza mbadala wa FB et al. Ila bila kuwekewa mazingira mazuri ya kibiashara hilo halitawezekana hata kama kila Mtanzania akiwa nguli wa Tehama. Haya mambo ni biashara pia.
 
Mawazo ya ajabu, kila chuo kinatoa kozi za tehama kama ni kujiimarisha si muimarishe vyuo vilivyopo?

Mama tafuta vitu vyenye tija vitakavyoacha alama yako.
 
RnD kwa mazingira gani?
Namshauri rais aanza na mambo rahisi kama kurekebisha sheria ambazo zinaturudisha nyuma. Kuna sheria zinapingana na National ICT Policy. Hili ni jambo linalohitaji utashi tu. Then tunaweza kufikiria makubwa mengine.

Mh. Rais ajue kuwa Watanzania hawajashindwa kutengeneza mbadala wa FB et al. Ila bila kuwekewa mazingira mazuri ya kibiashara hilo halitawezekana hata kama kila Mtanzania akiwa nguli wa Tehama. Haya mambo ni biashara pia.
Mama Samia ana malengo mazuri sana sema wale mbwa walioachwa na yule kichaa ndio wanamrudisha nyuma maana ni kama wameshikia bunduki
 
Sema wewe ndiyo masikini bwege nini,nani amekwambia duniani kuna nchi masikini?

Umaskini wako usipandikize kwa wengine hiyo ndiyo nafasi yako nchi inakusanya pesa kutokankwa wananchi,inapangisha majengo,inamiliki migodi,ardhi,n.k leo iweje masikini?

Jiongeze
 
Toba! Mbona walizuiaga mitandao humuhumu nchini kwa takribani wiki watu tukaanza kutumia VPN..!! Wanataka watuweke sehemu moja halafu watupige rungu tufe wote Sasa..😂
 
Mama Samia ana malengo mazuri sana sema wale mbwa walioachwa na yule kichaa ndio wanamrudisha nyuma maana ni kama wameshikia bunduki
Acheni upumbavu,kwanini asiwatoe kama wanamkwamisha..Je yeye alikuwa serikali ipi?
 
A518A883-096C-428E-8BEB-5C5FECCE8044.jpeg
 
Akumbushwe kipindi cha uchaguzi 2020 Internet ilizimwa na serikali ya CCM.
 
Back
Top Bottom