Rais Samia aagiza Darasa la Saba waliofutwa kazi walipwe stahiki zao

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Jan 1, 2019
7,567
9,026
Hongera Rais , kwa kuamua kulipa haki zao stahiki Mungu akubaliki sana . Katika hotuba yake leo amesema watumishi wa darasa la na vyeti feki walikuwa wakichangia mifuko ya hifadhi ya jamii hivyo amewataka waajiri wote kuhitimisha utumishi wao kwa kuwalipa stahiki zao.

=========

RAIS SAMIA SULUHU: Changamoto nyingine ni suala la watumishi wa darasa la saba waliostaafishwa ajira, kuhusiana na suala la watumishi hawa waliositishwa ajira kama mnavyokumbuka serikali ilitoa msamaha na kuwarejesha kazini watumishi walioajiriwa kabla ya tarehe 20 May 2004 ambao hawakufanya udanganyifu wa vyeti pamoja na watumishi waliojiendeleza na kujipatia sifa stahiki kwa mujibu wa miundombinu ya utumishi wa umma.

Kupitia msamaha huo, nafahamu kuwa watumishi 4,380 walirejeshwa kazini, hata hivyo napenda kutumia fursa hii kurudia maelezo ya serikali kwa waajiri kuhusu kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kuhitimisha ajira za watumishi walioajiriwa kwa elimu ya darasa la saba na wale walioghushi vyeti.

Hapa niwaagize waajiri wote waliokuwa na wafanyakazi wa aina hii, wafanye inavyowezekana kila mwenye haki aweze kupatiwa haki yake. Natambua kwamba, wafanyakazi hawa walikuwa wanakatwa makato inayokwenda kwenye mifuko ya jamii, ile ni haki yao. Walitoa jasho lao wakakatwa wakapeleka kule.

Kwa hiyo niombe sana waajiri, niwaombe sana waajiri, wale wasio na kumbukumbu za wafanyakazi wale waziweke kumbukumbu vizuri na wale ambao na wale ambao hawajalipwa kwa kisingizio kwamba serikali haikutoa muongozo, muongozo sasa ni huu, kila mwenye haki yake alipwe haki yake.

Na hapa naitaka ofisi yangu ya utumishi na utawala bora kusimamia zoezi hili.

Rais Samia Suluhu_Wafanyakazi.jpg

Rais Samia Suluhu akihutubia siku ya wafanyakazi duniani jijini Mwanza
 
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela, wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa kauli na matamko yatayowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani.

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.
 
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa zitakazowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Zamani watu walikuwa wanatumia vyeti vya watu kujiendeleza...........
Kama huduma zao zilikubalika hakuna tatizo yale mafao yao waliokatwa wakipewa. Unless ww huna ubinadamu.
 
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa zitakazowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Hivi unawajua wanasiasa kuwa wanaongoza kwa kughushi .
 
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa zitakazowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Wewe unahangaika bure mama kaishasema walipwe sikiliza hotuba dakika ya kumi na tatu mpaka kumi na sita , mambo ya roho mbaya za Jiwe hakuna tena .
 
Kwa hili nadhani mama Samia ameliwazia kisiasa zaidi badala ya kiweledi.....

Mtu aliyeghushi vyeti vya kitaaluma ni mhalifu na angetakiwa awe jela......wanasiasa wetu wana akili ndogo sana, daima wanawaza kutoa zitakazowafurahisha wapiga kura ili waendelee kubakia utawalani........

Mtu anayekalia nafasi ambayo ametumia njia za udanganyifu kuipata anazuia nafasi kwa wengine waliovuja jasho kwa ajili ya nafasi hiyo.......
Mwezi mtukufu huu.
 
Back
Top Bottom