Chief Kabikula
JF-Expert Member
- Jan 1, 2019
- 7,567
- 9,026
Hongera Rais , kwa kuamua kulipa haki zao stahiki Mungu akubaliki sana . Katika hotuba yake leo amesema watumishi wa darasa la na vyeti feki walikuwa wakichangia mifuko ya hifadhi ya jamii hivyo amewataka waajiri wote kuhitimisha utumishi wao kwa kuwalipa stahiki zao.
=========
RAIS SAMIA SULUHU: Changamoto nyingine ni suala la watumishi wa darasa la saba waliostaafishwa ajira, kuhusiana na suala la watumishi hawa waliositishwa ajira kama mnavyokumbuka serikali ilitoa msamaha na kuwarejesha kazini watumishi walioajiriwa kabla ya tarehe 20 May 2004 ambao hawakufanya udanganyifu wa vyeti pamoja na watumishi waliojiendeleza na kujipatia sifa stahiki kwa mujibu wa miundombinu ya utumishi wa umma.
Kupitia msamaha huo, nafahamu kuwa watumishi 4,380 walirejeshwa kazini, hata hivyo napenda kutumia fursa hii kurudia maelezo ya serikali kwa waajiri kuhusu kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika kuhitimisha ajira za watumishi walioajiriwa kwa elimu ya darasa la saba na wale walioghushi vyeti.
Hapa niwaagize waajiri wote waliokuwa na wafanyakazi wa aina hii, wafanye inavyowezekana kila mwenye haki aweze kupatiwa haki yake. Natambua kwamba, wafanyakazi hawa walikuwa wanakatwa makato inayokwenda kwenye mifuko ya jamii, ile ni haki yao. Walitoa jasho lao wakakatwa wakapeleka kule.
Kwa hiyo niombe sana waajiri, niwaombe sana waajiri, wale wasio na kumbukumbu za wafanyakazi wale waziweke kumbukumbu vizuri na wale ambao na wale ambao hawajalipwa kwa kisingizio kwamba serikali haikutoa muongozo, muongozo sasa ni huu, kila mwenye haki yake alipwe haki yake.
Na hapa naitaka ofisi yangu ya utumishi na utawala bora kusimamia zoezi hili.
Rais Samia Suluhu akihutubia siku ya wafanyakazi duniani jijini Mwanza