Rais Putin aihakikishia Afrika kuilinda kwa Chakula na Mbolea. Asema Russia na Afrika ni marafiki wa Kufa na Kupona!

Exactly!!
Hapo nadhani wanailump Afrika lakini kama wangekuwa specific wangesema Afrika Kaskazini, Somalia, Ethiopia, Sudani Kusini, na baadhi ya nchi za West Africa ndiko wanahitaji hiyo ngano ya Russia.

Hata hivyo kuna namna fulani hivi ambavyo mwafrika akili yake ni ndogo sana. Udogo wa akili ya mwafrika ni jinsi ambavyo wazungu wanavyoweza kutengeneza tatizo, wakalibrand kuwa ni tatizo kubwa kwa mwafrika, na mwafrika akaibeba mazima mazima hiyo simulizi ya mzungu na kuliona kuwa ni tatizo kwake. Mwisho ni mwafrika kuendelea kuwa tegemezi kwa mzungu milele na milele.

Mfano mdogo ni kuhusu corona. Corona ilivyoanza huko Ulaya na Marekani wakawa wakifa kama kumbikumbi yet simulizi kwenye vyombo vya habari vya wazungu ilikuwa ni jinsi ambavyo Afrika itakuwa "disproportionately hit" na corona. Wakati huo nafikiri Afrika ilikuwa hata haijapata hata mgonjwa mmoja wa corona. Lakini viongozi wa AU save Tanzania walivokuwa busy kujigonga gonga na kulialia kwa mataifa ya Ulaya na Marekani kuhusu chanjo, na jinsi mataifa hayo yanavyokumbatia chanjo utafikiri basi waafrika ndio tunaihitaji chanjo kuzidi wao. Ni akili ndogo tu na utumwa utumwa tu.

Na hata kwenye hii ishu ya Russia na Ukraine na madhara yake kiuchumi. Kama kuna madhara Afrika itayapata kutokana na hii vita hatutakuwa tofauti na watu wa mabara mengine. Huyo Sall kukimbilia Russia kuomba sijui hiki au kile ni utoto utoto tu wa viongozi wa kiafrika.
This is absolutely right.
 
Nchi nyingi za Africa, ( hata zile zisizofungamana na pande zozot, ikiwemo Tanzania) KAMWE hazitachangamkia fursa hiyo kwa sababu wanaogopa wataudhi mabwana zao wa magharibi. Hivyo wapo radhi wanachi wao wateseke kwa mfumuko wa bei ya mbolea, ngano na mafuta kuliko kununua kutoka Urusi.
Anaweza akavileta na viongozi wa Afrika wakashindwa kupokea, kama mafuta wameshindwa kununua ya Russia ambayo ni bei rahisi hizo mbolea na chakula wataweza kuvichukua?
 
Your Too young to understand this matter.
Mimi siiungi hoja.

Simpendi Rais Putin huyu mfalme wa madaraka milele. Wa kuvamia wazungu Ukrain na nchi huru. Wa kutishia kupiga unclear dunia.

Ni hatua ngapi tumetoka na Ulaya wakitusaidia? Yeye Putin kama kiongozi hata Africa hajakanyaga
 
Nchi nyingi za Africa, ( hata zile zisizofungamana na pande zozot, ikiwemo Tanzania) KAMWE hazitachangamkia fursa hiyo kwa sababu wanaogopa wataudhi mabwana zao wa magharibi. Hivyo wapo radhi wanachi wao wateseke kwa mfumuko wa bei ya mbolea, ngano na mafuta kuliko kununua kutoka Urusi.
Afrika hatuna viongozi wanaojitambua ndiyo maana ni Rahisi mabwenyenye wa mgharibi kutuendesha na kutuamulia mustakabali wa maisha yetu
 
Back
Top Bottom