Rais Museveni anachochea chuki baina ya Tanzania na Kenya

Tatizo kubwa hapa mkuu ni kuwa pamoja na Mganda kumuliko hayo mafuta yeye sio mchimbaji wala mjenzi wa huo mradi.
Mchimbaji na mwekezaji mkuu ni Total, kwa hiyo kinacho define namna ya kuyachimba na kuyauza hayo mafuta sio dhamira ya kisiasa wala kindugu iliyopo baina ya majirani zetu hawa ila ni nguvu ya soko.

Tuko katika zama za kibepari ambapo unaangalia faida zaidi kuliko undugu, kama faida iko Kenya utaenda Kenya, kama iko Tanzania utakuja Tanzania na ndicho anachokifanya Mganda.
Kuvunja mkataba sio ishu kubwa sana katika ulimwengu wa kibiashara.
Mkuu, ninafahamu vizuri hoja yako na sina tatizo katika msingi wa hoja yako.

Tatizo ninaloliona ni maamuzi tofauti kati ya wawekezaji na serikali ya Uganda ambayo yanajenga sintofahamu na kutoaminiana kati ya Tanzania na Kenya.

Mixed statements zinaleta confusion lakini pia zinajenga ufa katika nchi zilizoko ndani ya jumuiya ya EAC.

Statements za Boss wa TOTAL na Rais Museveni zinapishana!
 
Total ndiye mtoa hela na mtafuta wateja, anajua namna atakavyojenga bomba, namna atakavyo pump mafuta na namna atakavyoyauza.
Museveni ni politician na Total ni mtendaji....
 
Huyu mzee Museveni naona anataka kuwachezea hawa vijana Kenyatta na Magufuli. Si ajabu anataka kitu kidogo. Kwa Magufuli hapati kitu labda Kenyatta maana nasikia Kenya ni nchi ya kitu kidogo.
Mkuu kabula sijasoma comments zote imeniladhim nikuqot maana umeandka kitu ninachokiwaza. Maana kwa mazingira haya ni kutaka hongo.
 
Mseveni yuko huru kufanya maamuzi ya kushirikiana na yeyote kwa masilahi ya waganda siyo lazima Tanzania tu
 
Mazee hii ishu si yamchezo.Pini waliyopigwa leo wakenya pale airport ya Tanga si mchezo.Waziri wa nishati wa uganda leo amekuja tanga kwa usafiri wa anga.Kumbe wakenya nao wamejileta ili wasome ramani za kila kitu kinachoendelea. Tena mpka gharama za huyu waziri pamoja na wao wenyewe imelipwa na wizara ya nishati ya kenya.Sasa walivofika tu airport migration wako kama mvua.Kilichofanyika ni kuwaruhusu wananchi wauganda na wazungu wao kupita lakini wote wale wakenya walinyang'anywa passport zao na kuambiwa mtangoja hapa VIP LOUNGE,mpaka hawa wengine warudi. So waganda na uongozi wa gvt ya tanzania walienda kufanya yao.Waziri wao wa nishati na timu yake walibaki wanatoa macho.Mazee tz tuiache ilivo...hili tikio leo lilikuwa lakimafya sana sana.Ni mengi..ila chkueni hayo machache.
Hao wanafikiri hizi ni enzi za mkwere ....sasa ndio watajua kuwa sisi ni wajamaa tuliozibuka ...
 
Mkwere ilikuwa aibu sana. Angekuwa yeye tungepigwa bao la mapema wala Museveni asingehangaika.
Kampuni ya Total wameona ngosha yupo serious.
 
Ikumbukwe kuwa Jumuiya hii mpya ilizaliwa baada ya ile ya awali iliyoanzishwa mwaka 1968 na kuvunjika mwaka 1977 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kushindwa kuelewana kwa wakuu wa nchi wanachama kwa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere (Tanzania), Jommo Kenyatta (Kenya) na Idd Amin (Uganda).

Kile ambacho Uganda inakifanya kwa sasa kuhusu ‘’umalaya’’ katika maamuzi unajenga chuki kati ya Tanzania na Kenya.

Uganda inakuwa kama mwanamke anayetongozwa na wanaume wawili kutoka katika familia moja huku akimkubali kila mmoja. Mbaya zaidi, anajitokeza mbele ya kandamnasi na kusema huyu pia ni mwanamme wangu. Wananchi wengine wanabaki wanashangaa na kujiuliza, what’s going on?

Kinachotia wasiwasi, hatufahamu huyu mwanamke anaongea nini zaidi wakati akiwa ndani ya chumba kuhusu mwanamme mwingine anayedai pia anampenda.

Huu ujenzi wa bomba la mafuta unaweza kuleta matatizo makubwa katika mahusiano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ikumbukwe kuwa, Mwezi August, 2015 tulihabarishwa kuwa Kenya na Uganda wamekubaliana na kuweka saini kujenga hilo bomba la kusafirisha mafuta. Less than two months, on Oct 2015 tukaambiwa Uganda and Tanzania have signed an agreement to explore the possibility of building a crude oil pipeline between the two countries.

Mwezi March 1, 2016, Rais Magufuli na Rais Museveni wakaonekana mbele ya waandishi wa habari wakisema wamekubaliana kuhusu mpango wa kujengwa kwa bomba la kusafirisha mafuta kutoka bandari ya Tanga, Tanzania hadi Uganda.

March 14, 2016, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw. Javier Rielo alienda Ikulu Jijini Dar es Salaam na kumuhakikishia Rais Magufuli kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.

March 21, 2016, Tukaambiwa tena, Rais Kenyatta na Rais Museveni walikutana jijini Nairobi kujadili tena ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kati ya nchi hizo mbili. Mkutano huu ulifanyika siku chache tu baada ya Uganda na Tanzania kuafikiana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta kutoka bandari ya Tanga hadi nchini Uganda.

Kwa sasa jopo la wataalam wa Uganda wamebaki Kenya wakitembezwa huku na kule ili kujionea hali halisi ya fursa zitakazopatikana baada ya kujengwa bomba.

Kuna wengine wanaweza kudhani hili ni suala la kawaida lakini mimi ninaliona ni suala hatari sana katika mstakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ningemwelewa Rais Musevevi kama angekuwa anafanya huu ''umalaya'' kwa nchi ambazo haziko ndani ya EAC.

Rais Museveni anachochea ugomvi/uhasama sio kwa Marais wa Tanzania na Kenya pekee bali hata kwenye Mstakabali wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Rais Musevevi asikubaliwe kufanya biashara kwa mgongo wa kujenga chuki kati ya Tanzania na Kenya. Huu ni unafiki na uzandiki wa kiwango cha juu.

Someone must tell Rais Museveni to stop it, just play fair business game. He doesn't have to do all that mumbo jumbo.

Thats why nataka niandike paper kuhusu regional integration .SADC still remail the best.
 
M7 ana haki ya kutafuta the best deal kwa raslimali yake kwa kuangalia mambo mbalimbali; nafikiri hili swala tusilibebe kisiasa sana, ni la kibiashara na kiuchumi zaidi; na kwa jinsi siasa za ndani kule Kenya ya Kenyatta zinavyokwenda; tanganyika bado tuna nafasi ya kuukwaa mradi huo; leo hii wabunge wa county ya Turkana kuliko na mafuta wameapa bomba hilo halipiti ng'o! Tutumie soft power badala ya kashfa na matusi kwa kaka M7; kwani mwenye chake muungwana!
 
Mazee hii ishu si yamchezo.Pini waliyopigwa leo wakenya pale airport ya Tanga si mchezo.Waziri wa nishati wa uganda leo amekuja tanga kwa usafiri wa anga.Kumbe wakenya nao wamejileta ili wasome ramani za kila kitu kinachoendelea. Tena mpka gharama za huyu waziri pamoja na wao wenyewe imelipwa na wizara ya nishati ya kenya.Sasa walivofika tu airport migration wako kama mvua.Kilichofanyika ni kuwaruhusu wananchi wauganda na wazungu wao kupita lakini wote wale wakenya walinyang'anywa passport zao na kuambiwa mtangoja hapa VIP LOUNGE,mpaka hawa wengine warudi. So waganda na uongozi wa gvt ya tanzania walienda kufanya yao.Waziri wao wa nishati na timu yake walibaki wanatoa macho.Mazee tz tuiache ilivo...hili tikio leo lilikuwa lakimafya sana sana.Ni mengi..ila chkueni hayo machache.
[emoji15] [emoji15] [emoji15] yakweri hayo
 
Tanzania ni taifa kubwa kwa nchi za afirica mashariki tunapaswa kuonyesha ukubwa wetu kwa kumwita mganda ikiwezekana tumpunguzie gharama ili tuweze kupata mradi huu kwa kuwa tuna vyanzo vingi vya mapato,

huu mradi tuufanye wa ziada ili kumkomesha huyu mkenya anayetuchokoza kila leo mara mlima kilimanjaro wa kwake,
akitunyanganya huu mradi tutadhalilika sana.
Nadhani tatizo sio kumwita Mganda na kupunguza gharama, tatizo ni Mganda kutokusomeka au kueleweka anataka nini?

Mganda anakuja Tanzania tunakubaliana naye halafu baada ya siku mbili anaenda Kenya, wanakubaliana naye kwenye suala lile lile tulilokubaliana.

Anachokifanya Mganda ni ''umalaya'' kwenye maamuzi!
 
Mazee hii ishu si yamchezo.Pini waliyopigwa leo wakenya pale airport ya Tanga si mchezo.Waziri wa nishati wa uganda leo amekuja tanga kwa usafiri wa anga.Kumbe wakenya nao wamejileta ili wasome ramani za kila kitu kinachoendelea. Tena mpka gharama za huyu waziri pamoja na wao wenyewe imelipwa na wizara ya nishati ya kenya.Sasa walivofika tu airport migration wako kama mvua.Kilichofanyika ni kuwaruhusu wananchi wauganda na wazungu wao kupita lakini wote wale wakenya walinyang'anywa passport zao na kuambiwa mtangoja hapa VIP LOUNGE,mpaka hawa wengine warudi. So waganda na uongozi wa gvt ya tanzania walienda kufanya yao.Waziri wao wa nishati na timu yake walibaki wanatoa macho.Mazee tz tuiache ilivo...hili tikio leo lilikuwa lakimafya sana sana.Ni mengi..ila chkueni hayo machache.
E bana mkuu hili umelisema ni kweli au unatupoza na kutupa moyo??
Maana nimejikuta nimefurahi na kuangua kicheko kikubwa cha ushindi! Safi sana watz. Huu ndo umafia kenya wanatakiwa kufanyiwa.. Unyama unyamani..
Enhee sasa wale wakenya ikaishiaje mkuu? Hebu tupe nyama zaidi...
 
u are nuts! business is business tena hao nyang'au ndio wajuaji kweli. wakikosa wasilete vitisho vya wapumbavu
 
Dawa ya malaya kumti tu"
Bado nina imai Tanzania kuna mafuta its abt time tu maana exploration zinaendelea baadhi ya maeneo..
Huyu mzee asituchanganye kama vp atutolee balaa alipitishie huko anakoona sawa kwa wajaluo"
 
Mseveni kafanya kitu cha kishenzi sana.
Usindani wa kisiasa na kiuchumi na kunyang'anyana tonge inakubalika kabisa.
Lakini ukishatangaza hadharani kuwa umeshapatana na Tz kwenye dili afu kwenda kuanza mazungumzo mapy na mwingine ni unyang'au na umalaya.
Kama alikuwa hajaridhika na dili ya Tz basi angenyamaza na sio kuitangaza huku kavaa ule mkofia wake.
Mkuu, ulichoandika ndio msingi wa hoja yangu.

Kwa nini Rais Museveni anatoka nje na kusema tumekubaliana suala fulani na anaenda mbele zaidi na kusaini makubaliano wakati anafahamu kuwa hakubaliani au hayuko serious katika makubaliano.

Matendo ya Rais Museveni katika suala hili la ujenzi za bomba yanajenga ufa na kutokuaminiana katika EAC.
 
Dawa ya malaya kumti tu"
Bado nina imai Tanzania kuna mafuta its abt time tu maana exploration zinaendelea baadhi ya maeneo..
Huyu mzee asituchanganye kama vp atutolee balaa alipitishie huko anakoona sawa kwa wajaluo"
Kuna faida nyingi kuhakikisha bomba linapita kwetu. Yanaweza kugunduliwa mafuta maeneo linapita au karibu tukatumia bomba hilo hilo.
Pia suala la heshima kama nchi. Tusikubali kabisa kama Museveni aliji commit na kampuni ya Total inapendelea Tanzania.
Si vibaya kufanya a bit of arm twisting pia. Tuwakumbushe bila sisi Amin angewadhuru zaidi. Wapi shukurani zao? Wakati ule Kenya walikuwa upande wa nduli
 
Museven aseme moja sasa"
 
Mkuu, wewe ndiyo umenipa mwanga.

Siku zote nchi za Africa ni kuchezewa tu na mataifa makubwa. Nyuma ya pazia kuna vita kati ya kampuni ya Total (Wafaransa?) na Tullow Oil (Uingereza?). Ukweli wenyewe Uganda, Tanzania na Kenya tunacheza sindimba ya wakubwa hao.
Kwa hiyo unadhani Rais Museveni hafahamu kama yeye hana uamuzi wa mwisho katika maamuzi ya ujenzi wa bomba.

Kama Rais Museveni anafahamu hana maamuzi ya mwisho, kwa nini anazunguka huku na kule kujadili na kuweka signature kwenye suala mbalo liko nje ya uwezo wake?
 
Unaishi dunia ipi wewe?
 
Back
Top Bottom