Rais Museveni anachochea chuki baina ya Tanzania na Kenya

chige,

..kama Ethiopia na Kenya wameweza kupata pesa za kujenga reli mimi sioni kwanini Tz tunashindwa.

..mimi nadhani we have to think outside the box jinsi gani tutajenga reli zetu. tukisubiri wawekezaji toka western world tutasubiri sana kama alivyosema Meles Zenawi[r.i.p].

..tunahitaji miradi mikubwa ya miundombinu ambayo itakuwa ni fahari kwa nchi na italeta multiplier effect ktk sekta nyingi za uchumi hapa Tz.
 
Sio kamba hakuwa na choice bali matatizo ya kuchanganya siasa na uchumi. Wakati haya yanatokea ilikuwa ni wakati wa cold conflict kati ya Tanzania na Rwanda na Kenyatta kwavile ni mjasiriamali wa kuzaliwa, akaamua kutumia hiyo fursa kupenyeza agenda zake na zilikubalika kirahisi kv tayari watu walishakuwa na vinyongo vyao tangia zamani!
...chige, take note kwamba, nimesema toka PK alipoingia madarakani. That is waaay back, ndugu.

Kwamba Rwanda walionesha interest tangu zamani ni kweli lakini hapa kulikuwa na conflicting objectives ambazo watu walishindwa kuziona. Wakati Rwanda wakiona as if Tanzania ni wazembe wanaochelewesha mradi wa reli, Tanzania kwa upande wake walikuwa na vipaumbele tofauti at least kwa muda husika. Tanzania walifahamu hawakuwa na ubavu wa kujenga reli ya kisiasa kwahiyo wakajikita sana kwenye ujenzi wa barabara... wakati huo Rwanda bila shaka wakiona tungeanza na reli badala ya barabara wakati gharama za kilometa moja ya reli ni karibu mara 10 ya gharama za kilometa moja ya barabara. Sasa sidhani kama kuna taifa duniani lingechukua hiyo option manake hata hao wenzetu Wakenya, ule mradi wa reli ya standard gauge ni wa miaka na miaka lakini nao hawakuwa na jinsi bali kuanza na kile ambacho kingewezekana.
...Mpango wa kuboresha reli ya kati ni wa muda mrefu pia. Kuna mengi yameongewa kuhusu hili na barabara. Tujiuleze, kwanini wenzetu wanajenga reli kila siku. Hapa namaanisha nchi ambayo inaendelea kujijenga kama China.

...Gharama za kujenga reli -au barabara kwa maana hiyo- ziko kwenye kulipa fidia ya ardhi, kujenga madaraja na kutoboa milima, kwa inayopita juu. Gharama hii kwetu zikoje? Usinijibu, tujiulize tu.

...Je, kwani nini kila leo nchi zenye kusafirisha vitu in bulk -kama madini, mizigo, n.k- zinazidi kujenga reli?

Lakini kama nilivyosema, hoja ya msingi hapo haikuwa kutokuwa vinginevyo sioni mantiki ya kuurejea mradi ambao haujaanza kuwekwa hata tofali moja wakati ule wa Kenya umeshaanza! Hii ni kwa sababu, baada ya kutulia walikuja kugundua kwamba walikuwa wanapelekeshwa pelekeshwa na kuacha kufanya rational decisional. Sasa kv ameshajitoa kwenye mradi wa Kenya na kurudi Dar to Kigali Project huku wao Rwanda wakipewa shavu la kushughulikia mradi; ndipo hatimae watafahamu kujenga reli si sawa na kujenga barabara hususani kwa linchi likubwa kama Tanzania.
...Kuna sehemu unaongelea kutopiga siasa kwenye mambo kama haya. Mbona unaelekea huko.

...They had two choices, the way i see it. Watusubiri au waangalie kwingine. Kama ulivyosema, M7 aliwageuka!

Hilo la kutokuwa na option ni moja tu lakini viongozi wetu wana ile silika ya kuchanganya mambo ya siasa na uchumi. Kipindi kile kilikuwa ni ambacho tupo kati kati ya diplomatic conflict na Rwanda... conflict ambayo ilianza miezi michache tu tangia Kenyatta aingia madarakani! Alichofanya Kenyatta ni kutumia hiyo loophole ya conflict na kuharakisha mradi wa reli wa na Kenyatta alipoingia madarakani akaamua kutumia hiyo loophole na kuwaaminisha things can be done without a moment's hesitation. Sasa kv tayari watu walishakuwa na some egos ta
...Actually, Kenyatta alitumia avenue zote mbili. Kutokuwapo mpango wa kushikika wa ujenzi wa reli kati yetu na Rwanda, pamoja na kutoelewana.
 
...Katika moja ya vitu vinavyonipa hasira at times ni reli ya kati.



...Actually, kama si rushwa na terrain katika ujenzi wa reli, gharama si kubwa kivile. Reli ya Mombasa-Nairobi inasemwa kuna hela inategenezwa, matata.



...This thing is long overdue.

...Nategemea afanye hivyo.


...That was my point, and why the Kenyans will not let go of this easily.

...Ethiopia wanaonekana kuwa na appetite ya kuwekeza miundo mbinu kuelekea Djibouti. Wana barabara na reli tayari. Meli zao zipo huko pia. It makes sense, but, many eggs in one basket.

...Wanategemea pia kuchimba mafuta. They've being very aggressive of that front of late.

..nakubaliana na hoja zako zote.

..mimi ninachoomba huyu waziri wa miundombinu wa sasa hivi adumu ktk wizara hiyo.

..kumekuwa na tatizo la kila waziri anayeteuliwa wizara hiyo ku-push a reset button ktk masuala ya bandari na reli.
 
Uliyosema ni kweli kabisa kwamba huenda Magufuli atawachangamsha! Lakini hapa tujiulize kwanza jambo moja. Hivi awamu iliyopita haikujenga reli hata kama walikuwa tayari na financing au walishindwa kujenga kwavile walikuwa bado hawajapata financers? Ukifanya research juu ya gharama za ujenzi wa reli, Tanzania labda itumie mapato yake yooote (bila kupunguza senti) ya miaka miwili mfululizo ndipo tunaweza kuwa na ubavu wa kujenga reli ya Dar to Kigoma bila ku-include matawi yake! Sasa kwa staili hiyo, there's no way tunaweza kujenga reli bila kupata strong pockets back up kama waliyopata Wakenya manake hata Wakenya pamoja na mbwembwe zao zote za kujifanya wapo juu kiuchumi bado ule mradi wao wa standard gauge wana-finance chini ya 15% ya gharama. Kwa kumbukumbu zangu, sijawahi kusikia kwamba mradi wa reli ya kati umepata serious investor X just waiting for the government greenlight to start the project. Sijasikia.
...Kwenye ujenzi wa bomba la gesi, hela zimetoka wapi? Si tumekopa sehemu. Hivi ndivyo miradi kama hii hufanywa. Hutumii hela ya makusanyo ya ndani na ya nje. Labda kama wewe ni China.

...Ukishasema miaka miwili ya mapato -sina uhakika, utanielimisha- basi tunaweza kukopa mkopo wa makumi ya miaka.

...Miradi hii haitegemei kujengwa kwa hela za ndani ndugu. You have to raise money somewhere. Take the case of Grand Renaissance Dam.

Sasa kama bado hajapatikana investor ambao anachosubiri is just "anza" basi hata huyo Magufuli atatuchangamsha kisiasa tu kama ilivyokuwa kwa serikali ya JK ambayo kila siku ilikuwa ukisikiliza simulizi za standard gauge railway, basi mtu angedhani wiki ijayo mradi unaanza.... lakini wapi!
...Sidhani kama JPM anapiga siasa kwenye hili.
 
DAR si LAMU,
Nakubali kwamba PK amekuwa na mpango na reli ya kati since then lakini kama nilivyosema hapa tunazungumzia reli ya standard gauge across a very large poor country. Nitajie nchi moja ya SADC ukiondoa SA ambao wamefanikisha kujenga hii reli.
...Actually, Southern Africa wanatumia kipimo kinaitwa Cape gauge -3 ft 6 in- ambayo inawafanya waweze kushirikiana kupitisha train zao, maeneo yao. Hapa msisitizo wangu uko kwenye mizigo zaidi. Angola -ambao nao wanatumia cape gauge- katika miaka ya karibuni wamepeleka reli hadi mpakani na DR Congo.

...Gautrain, ambayo ni kwa ajili ya rapid transport kati ya Pretoria -actually, Hatfield- na Jo'burg, yenye 80 kms ndio standard gauge. Issue ni speed na usalama wa abiria kwa maana hiyo.

...Inasemwa standard gauge ina gharama kuliko cape gauge, lakini, haiondoi umuhimu wa reli kwenye usafirishaji wa mizigo na faida yake kwa uchumi.

...Sie si masikini -kama wimbo huu unavyoimbwa, mara kwa mara- ila mawazo yetu ndio masikini.

...Addis Ababa-Djibouti railway yenye urefu wa 656 kms -achilia mbali double track za 115 kms- na yenye kutumia umeme, inakaribia kumalizika -at 87%- na mpango ni mwaka huu. Wamewezaje? Hili swali linahitaji majibu.

...Kwa faida ya majadiliano -na wengine watakaokuwa interested- soma na hii ya Nigeria, ina mpaka gharama na concern zako zimezungumziwa pia, ila, kazi inapigwa.

...Na hapa, check railway network ya Nigeria. Take note kwamba, baadhi ya hizo proposed zimefanyiwa au zinafanyiwa kazi.

Ninachotaka kusema ni kwamba, kwa such costful investment; sisi wenyewe hatuna ubavu wa ku-finance angalu 50%. Kwavile hatuna huo ubavu, the only way to make things done ni kupata potential investors. For what I know, hadi sasa hajapatikana na kama yupo nitajie maybe am missing something. Na tusisahau, kwa miradi mikubwa kama hii si kila investor ana ubavu wa kutia pua yake! Na sometimes investor anaweza akapatikana lakini bado hiyo nayo haiwezi kuwa guarantee ya kuanza project manake hawa investors wanachofanya ni ku-express interest na akishapewa mradi; wanaanza ku-gather resources and that phase can take years as well!
...This is why i've said, we are suppose to raise the money. We don't have the money at hand, some ppl have them. We need to come up with a good plan, to finance the project. It can be done!

...Nakubaliana nawe, we need investors. Lakini, kwa kiasi gani? Afrika Kusini, Ethiopia na Nigeria miradi hii ni ya Serikali. Hatuwezi kusubiri investors ndio tujenge! Wakijenga wengine -nchi jirani- wakatupita, pesa itaenda kwao!

...I'm not counting them -investors- in as such. Labda kwenye reli kati ya Mtwara na Mbamba Bay au Mchuchuma/Liganga for that case. Naongelea kuchimbwa kwa chuma. Hii ngoma ni ya Serikali, in larger part.

Sasa kv PK aliwaona wenzake wazembe, na tayari alishakuwa na negative perceptions against JK; ndo maana kwake ikawa rahisi kwenda Kenya ambako tayari project ilikuwa underway. Lakini hapa pia tusisahau ule mradi wa Kenya nao ni wa muda mrefu... si kwamba Kenyatta kaingia tu madarakani akaanza initiative and six months later mradi uka-take-off; NO! Na hawa investors wana interests na priorities zao... it's not a matter of country X kuna investment Y ndo basi tena wanakimbilia! Mfano mzuri chukulia sakata la Bandari ya Bagamoyo! Wengi wanahoji kwanini isingekuwa Tanga... investor anataka Bagamoyo! Na hili limemkuta Mu7 na bomba lake! Wakati am certain yeye alishakuwa interested na Mombasa lakini mdau mkuu Total anataka Tanga!
...Kenya wanajenga wenyewe -wao ndio investor- kwa mkopo wa mChina. China ana appetite na tumbo la kutoa mikopo!

...Nadhani kwa Bagamoyo, mChina aliitaka kwa ajili yake yeye mwenyewe -inasemwa 50 yrs, i'm not sure- ili aweze kufika Rwanda, Burundi na DR Congo. Can you imagine the magnitude na effects of this? Nakuelewa!

Pia unauliza bomba la gas pesa zinatoka wapi? Kwanza, maelezo yangu ya hapo juu nimeshaweka wazi si kila investment inakimbiliwa na kila investor! Gharama za lile bomba ni $1.3 Billion ambazo zimewezesha kutandaza bomba umbali wa zaidi ya 500KM. Ukichukua hizo $1.3 Billion ukaziweka kwenye reli si ajabu ikaishia Morogoro au isifike kabisa! Sasa ulinganishe gharama za ujenzi wa bomba umbali wa 600 KM na reli across almost 1200 KM excluding zile pacha zinazounganisha miji mingine? Hiyo 1200KM nime-exclude rail ya Tabora to Kigoma; Kaliua to Mpanda na ile ya Isaka to Mwanza ambazo nazo ni part of the project not mentioning ile ya Kaskazini!!
...Ndio, hizo hela kwa reli ni ndogo, na tunahitaji zaidi ya hizo! Hatuwezi jenga reli yote kwa mkupuo! I would venture kwamba, kipande cha kwanza kifike Dodoma, na kuwe na bonge la inland port, mizigo iweze tawanyika nchi nzima tokea hapo, and beyond. This can be done!

...Nakuelewa kwenye urefu wa reli, tena sana, ndugu yangu. Tujenge kwa vipande! Hata wakoloni walijenga kwa vipande. Ujenzi huu ufanywa kwa vipande.

...Corridor isiyo na traffic kubwa ya mizigo, isiwe kipaumbele cha reli. Pesa inatarudi vipi?

Kuhusu miaka miwili ya makusanyo yetu! Nimetafuta gharama za ujenzi wa reli ya Kati nikakosa hivyo nikaamua nitumie za Kenya as a benchmark. Mombasa to Nairobi ni 609KM standing at $3.8Billion. Hizo $3.8Billion ni zaidi ya Trilion 7 za Tanzania na hiyo 609KM hata Tabora haufiki--- wakati tunaitafuta Kenza (near the boarder of Rwanda & Burundi Tanzania side). Hapo pia nimetoa pia line to Kigoma and Mwanza. Sasa endapo hizi gharama za Kenya zingekuwa ni directly proportional to Central Line cost basi hiyo TZS 7 Trillion zilizotumika Mombasa to Nairobi basi kwa project yetu ingekuwa ni almost 7*3 ambayo ni Trillion 21. Samuel Sitta mwaka jana (but ignore him because it's political) alidadi gharama za ujenzi ni Trillion 14. Kwa kuangalia hayo, ndo nikasema ni makusanyo yetu ya miaka 2!!
...I would be careful to use that project as a benchmark! Ina kasoro kadhaa. Kwanza, bei inasemwa imechezewa, ili watu wapate chakula. Pili, kuna ujenzi mkubwa wa madaraja ya juu katika njia, kitu kinachoongeza gharama.

...But still, like i said hapo juu. Ujenzi huu tutaufanya kwa awamu. Dar-Dom, halafu mbele kwa mbele. Tr 7 -ingawa nafikiri hiyo bei sio sahihi kihivyo- ni hela ya kawaida kwasasa kwa mradi kama huu.

...Huwa linaangaliwa pato la Taifa! Hiyo hela sio issue. Tatizo ni balls za kujenga hiyo reli. Itabidi miradi mingine tuitafutie namna, au kuipotezea kwa muda. Ndio ukweli. Its about choices, as you once said!

Kwamba tunaweza kukopa; ni sawa lakini hata huko kukopa si kwanza lazima apatikane potential investor na wewe unamdhamini? Na kama unamaanisha kukopa nchi kama nchi; pia inawezekana lakini si rahisi kiasi hicho... remember, tunazungumzia Billions of dollar hapa.
...Tunatakiwa kukopa kama nchi, yes, ndio namna miradi mikubwa kama hiyo huwa financed. Walipakodi watalipa deni!

...Issue kubwa ni mkataba, kwa maana ya malipo, riba na muda. Na uwezo wa kuongeza muda kama mambo hayatakuwa mazuri. Hatuhitaji kumwamini mtu, bali mkataba ulio mezani.

Kwamba miradi kama hii haitegemei pesa za ndani nimeshasema hilo kabla lakini hapa napo, tunarudi palepale... je, huyo investor alishapatikana? INvestor mkubwa wa miradi kama hii ni China lakini nae anaenda hatua kwa hatua kulingana na interest zake kwa wakati husika. For the past 3 years alikuwa kwenye railway and port investment upande wa Horn of Africa na West kisha akarudi Kenya! Tenda iliyotangazwa July mwaka jana ya Dar to Kigali (DIKKM) China Constructions nao wameomba! Lakini hili nalo kwa sababu zile zile ambazo nimetaja hapo juu; wala tusidhani kwamba ndo basi tena the project will take off soon! And remember, Rwanda ilipewa usukani wa hili jambo since 2014 na leo 2016 lakini bado investor HAJAPATIKANA! However, am certain kwa sasa atapatikana kwa sababu huu mradi wa DIKKM ni wa tangu 2009 na tangu hapo ulikuwa ni mradi wa PAMOJA kati ya Tanzania, Rwanda & Burundi but since then ikawa unaonekana kama ni wa Tanzania peke yake! Sasa kv wote wamerudi mezani na kutekeleza dhana ya Partnership Project, basi hivi sasa tunaweza kupata mwekezaji!
...Investor ni Serikali. Inabidi iwe hivyo, ama sivyo reli haijengeki.

...China, through mabenki yake, kwa udhamini wa serikali yake, ni financier. Yeye anajali hela yake irudi tu. Akiona haitaweza kurudi, hakupi. Of course na umuhimu wa link ya mradi na masilahi yake ya kibiashara na kisiasa.

...Imeanza mbali zaidi, na is long overdue!

Kwamba Magufuli na siasa kwenye reli. Nilichosema ni kwamba; for what I know hajapatikana potential investor. Sasa kama hajapatikana, Magufuli leo hii akileta suala la reli ya kati itakuwa ni siasa! By the way, nini kinakufanya uamini huyo JPM asiwe anapiga siasa? Ni mara ngapi kapiga siasa za flyovers Dar es salaam? Hata nondo moja ya flyover haijawekwa lakini hivi sasa anataka kutujengea barabara ya juu kwa juu inayokatiza bahari (but I like the project) kuanzia Ocean Road to Coco Beach!! A politician is a politician; he'll always tell you what you want to hear!
...Bado hajaanza kuingia kwenye hilo, bado. But for how long, sijui.

...Naamini, anafikiria kama sie wengine tunavyofikiria kuhusu reli. Issue itakuwa namna ya kutekeleza na sio mradi kuanza au kutoanza. Believe me.

...Ile pale maungano ya Nyerere na Mandela inaanza. Tuongelee nyingine!

...Hiyo ya Coco beach, sijui. Ile ya Chalinze njia sita, sijui.

...Uzuri wa issue ya reli ni kwamba, si jambo tunalotaka kusikia liburudishe masikio yetu, bali ni suala la lazima, hatuna namna. Hatuna namna!


PS. chige, nashukuru kwa mchango wako. Umechangamsha akili yangu!
 
Samahani. Kuna gharama Mara mbili. 1, Gharama ya kujenga reli kwa kupitia tuta LA zamani. 2, Gharama LA kujenga tuta jipya. Tuangalie apo.
 
Samahani. Kuna gharama Mara mbili. 1, Gharama ya kujenga reli kwa kupitia tuta LA zamani. 2, Gharama LA kujenga tuta jipya. Tuangalie apo.
...Ni kweli.

...Kwa mfano. Kama sie tukiwa tayari sasa -kwa kuwa reli ni kama haitumiki- tunaweza fumua Dar - Dodoma, tukibandika nyingine. Gharama haitakuwa kubwa kama kuanza mpya kabisa, pengine ikipitia eneo tofauti. Ila, Morogoro kujenga pale ni gharama, pengine t-beams ndogo au tuta kubwa na madaraja yatahitajika maeneo yanayokumbwa na mafuriko.

...Ukiangalia ujenzi wa njia mpya/tuta jipya Nairobi - Mombasa, tafauti iko wazi. Tuta limenyanyuliwa zaidi, madaraja na t-beams kadhaa, hii yote ikipelekea gharama zaidi.
 
Wakati Tz inatangaza kujenga bandari ya Bagamoyo kenyatta alibwata sana kwa sababu aliona kapigwa bao na ubora wa bandari ya mombassa itakuwa sio kitu kwa bandari ya bagamoyo.Mwaka mmoja baadae kenyatta kaanza kujenga bandari ya kisasa kama itakavyokuwa ya Bagamoyo huko lamu.Kenyatta na wabongo wengine walemavu wa akili wakabwata sana kusema hakuna umuhimu wa bandari ya bagamoyo,sasa kenyatta anataka kutupiga bao sisi tunalalama na hii ndio tabia ya wabongo ,wenzetu wanasonga sisi ni kubwabwata tu.Kenya wametupiga bao mlima kilimajaro sisi ni kubwabwata tu,juzi juzi tumepigwa bao la olduvai g sisi ni kubwabwata tu oooh kenya ,kenya wenzetu message sent.
Mr Pombe soma ujumbe huu kisha uelewe bongo tunasifika kwa kubwabwata na unafiki wenzetu wanasonga mbele.Wenzetu wapo kwenye business sisi tunasubiri tupewe sifa.
Uwekezaji kenya unasifa sisi huku ooh JK ,ooh JK nenda Rwanda uone uwekezaji unakuwaje ni mazingira ya kuvutia kenya wanataka kutumia ubora wa miundombinu yao kuchukua tender ya bomba Wake up maaaaan

Mambo mawili au matatu hapa yanahitaji umakini mkubwa: Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ulikujaje? Ulifanyiwa economic appraisal na tafiti nyingine muhimu kabla ya kuamua uendelee badala ya kuboresha bandari za Dar, Tanga na Mtwara? Nasikia mradi huo uliibuliwa ghafla tu wakati wa ziara ya rais wa China hapa TZ. Sidhani kuwa ulikuwepo hata kwenye ajenda za EAC.
Pili: Nimesoma mahali kwamba TZ imejitolea mafuta ya Uganda kupitia bomba litakaloyafikisha hadi Tanga yatasafirishwa bure! Inasemekana kwamba uamuzi huyo umefanywa kuwavutia Waganda wachague njia ya Tanzania badala ya Kenya, ambao inasemekana watatoza dola kadhaa kwa kila barrel au Lita ya mafuta yatakayopita kwenye ardhi yao kutoka Uganda.Kama taarifa hizi ni za kweli, swali langu ni uamuzi huo ni wa busara? Nitowe mfano hapa ili wenzangu mnielewe: Njia ya reli ni ardhi iliyotengwa mahsusi kwa shirika la reli, mtu asiyehusika haruhusiwi hata kukanyaga eneo hilo la mita kadhaa upande wa kushoto na wa kulia mwa reli. Kwa maana nyingine hata serikali haina mamlaka na ardhi hiyo. Kwahiyo ardhi na bomba la mafuta ya Uganda vitalindwa na nani humo litakamopita hukuTZ ikiwa hakutakuwa na kodi au tozo yoyote kwa bomba hili? Na TZ itarudisha vipi gharama za ujenzi au mkopo wa bomba hilo?
Tatu kuhusu gharama za mradi huu: Nasikia utagharimu dola za USA bilioni 4 hivi. Hapohapo nimesikia Egypt na Saudi Arabia wanna mpango wa kujenga daraja kuunganisha nchi hizo mbili litakalopita juu ya Bahari ya Sham au Red Sea, kwa ghrama ya dola za USA bilioni 4 pia! Jamani! Mbona siewlewi?
Mwisho: Tukumbushane kwamba TZ iliwahi kuzungumzia ujenzi wa bomba la mafuta kati ya Dar na Mwanza pamoja na sababu nyingine bomba hili lingepunguza uharibifu wa barbara kutokana na usafirishaji wa mafuta kwa magari na pengine hata bei ya mafuta kwa kanda hiyo ingepungua. Huyo ulikuwa mradi watu wenyewe, kwanini haukutekelezwa? Kama ungetekelezwa mafuta ya Uganda si yangepitia njia hiyo au bomba hilohilo? Ndiyo mana tumesema TZ isitegemee saana majirani kwa kila miradi mikubwa na tusipange mambo kisiasa tu, kama magorofa na madaraja baharini.
 
Mambo mawili au matatu hapa yanahitaji umakini mkubwa: Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ulikujaje? Ulifanyiwa economic appraisal na tafiti nyingine muhimu kabla ya kuamua uendelee badala ya kuboresha bandari za Dar, Tanga na Mtwara? Nasikia mradi huo uliibuliwa ghafla tu wakati wa ziara ya rais wa China hapa TZ. Sidhani kuwa ulikuwepo hata kwenye ajenda za EAC.
Pili: Nimesoma mahali kwamba TZ imejitolea mafuta ya Uganda kupitia bomba litakaloyafikisha hadi Tanga yatasafirishwa bure! Inasemekana kwamba uamuzi huyo umefanywa kuwavutia Waganda wachague njia ya Tanzania badala ya Kenya, ambao inasemekana watatoza dola kadhaa kwa kila barrel au Lita ya mafuta yatakayopita kwenye ardhi yao kutoka Uganda.Kama taarifa hizi ni za kweli, swali langu ni uamuzi huo ni wa busara? Nitowe mfano hapa ili wenzangu mnielewe: Njia ya reli ni ardhi iliyotengwa mahsusi kwa shirika la reli, mtu asiyehusika haruhusiwi hata kukanyaga eneo hilo la mita kadhaa upande wa kushoto na wa kulia mwa reli. Kwa maana nyingine hata serikali haina mamlaka na ardhi hiyo. Kwahiyo ardhi na bomba la mafuta ya Uganda vitalindwa na nani humo litakamopita hukuTZ ikiwa hakutakuwa na kodi au tozo yoyote kwa bomba hili? Na TZ itarudisha vipi gharama za ujenzi au mkopo wa bomba hilo?
Tatu kuhusu gharama za mradi huu: Nasikia utagharimu dola za USA bilioni 4 hivi. Hapohapo nimesikia Egypt na Saudi Arabia wanna mpango wa kujenga daraja kuunganisha nchi hizo mbili litakalopita juu ya Bahari ya Sham au Red Sea, kwa ghrama ya dola za USA bilioni 4 pia! Jamani! Mbona siewlewi?
Mwisho: Tukumbushane kwamba TZ iliwahi kuzungumzia ujenzi wa bomba la mafuta kati ya Dar na Mwanza pamoja na sababu nyingine bomba hili lingepunguza uharibifu wa barbara kutokana na usafirishaji wa mafuta kwa magari na pengine hata bei ya mafuta kwa kanda hiyo ingepungua. Huyo ulikuwa mradi watu wenyewe, kwanini haukutekelezwa? Kama ungetekelezwa mafuta ya Uganda si yangepitia njia hiyo au bomba hilohilo? Ndiyo mana tumesema TZ isitegemee saana majirani kwa kila miradi mikubwa na tusipange mambo kisiasa tu, kama magorofa na madaraja baharini.
Uki zungumzia mradi wa bandari ya Bagamoyo ule ilikuwa ni kupeleka fadhila tu nyumbani na hata Air-port ili zungumziwa kuwepo Bagamoyo sijui ndege zingepishana vipi na flying saucers(nyungo) ila kama iki zungumziwa manufaa ya kibiashara kwa nchi bandari kuwa Tanga(Mwambani) ndio mahala pake kabisa.
 
Back
Top Bottom