Rais Museveni anachochea chuki baina ya Tanzania na Kenya

Hapa tunamlaumu bure Yoweri Kaguta, huyu jamaa yetu maji ya shingo yamemfika. Uchimbaji wa mafuta Uganda unahusisha makampuni makubwa mawili TULLOW na TOTAL kiuhalisia TOTAL ndio mwenye mtaji mkubwa hivyo ana turufu. TOTAL ameamua kupitisha bomba Tanzania, Na TULLOW ameonyesha interest ya uchimbaji mafuta Kenya. Hapo Bw. Yoweri Kaguta anahaha kunusuru mambo, tumuonee huruma jamani!!!!!!
Mkuu, Naomba unifafanulie vizuri. Rais Museveni anahaha kunusuru mambo gani na kwa nini anusuru?
 
Hakuna kitu kibaya kama kulazimisha biashara. Upo uwezekano mkubwa wa kusacrifice hata utu na heshima yetu ili kupata hii biashara ya Kupitisha Bomba la Mafuta. Tusifikie hapo, ifike mahala nasi tumpe ukweli huyu mnafiki ili ajue analotaka kulifanya halikubaliki na halina mashiko. Kama alishaanza makubaliano na Kenya na wamefika katika hatua nzuri za utekelezaji ni vyema akaendelea nao.
Tukumbuke huyu M7 ni mnafiki anaweza kutugeuka kama alivyoweza kuwageuka jirani zetu. Tusilishabikie hili suala bila kuangalia udugu wetu, heshima yetu, uhuru wetu na fikra zetu na majirani wanaotuzunguka. Huyu M7 ni mnafiki ni bora kumtolea nje ili ajifunze kuishi vizuri na majirani zake. Kumbukeni leo mwenzako kesho kwako.

Mnafiki ni wewe, na utakuwa Mkenya wewe.

Fitna katika biashara haikwepeki na fitna ni tafsiri ya mtu binafsi lakini neno linalstahili ni 'strategy'

Fahamu kuwa the issue is already resolved na issue ni usalama wa bomba, wewe huelewi nn hapo
 
Naona mambo ya Unyumbu pembeni
Leo naunga Mkono hoja
Mambo ya kulialia Watanzania tuyaache
Hii fursa itakuwa aibu na hasara ikitupita kushoto
Asante kwa kujitambua kuwa we ni nyumbu...

Pamoja na hilo ..nami naunga mkono hoja yako...Mda wa kulialia haupo tena.,.Wakenya wa napenda fitna.so lazima twende nao mzobe mzobe...watatukoma kudadadeki zao...
 
Mbaya zaidi, nchi zilizoko kwenye EAC ndio zinapambana zenyewe kwa zenyewe!

Hii ni kama vita ya wenyewe kwa wenyewe!

Kwa mtaji huu, EAC itasalimika?

Usifananishe biashara ya watu binafsi ya baina ya nchi

Hakuna ubaya wowote, Wakenya wakituchikia basi kutakuwa na tatizo jingine na si hili,
 
Well said comrade

No well said here! It is just the splendid show off of ignorance and original layman point of view in issues pertaining bargaining. Among major salient features in existence of weak human capital within a nation is lack of confidence and unreasonable fear and suspicion among her elite class.
 
Mkuu, Naomba unifafanulie vizuri. Rais Museveni anahaha kunusuru mambo gani na kwa nini anusuru?

Mkuu hapa mwenye turufu ni TOTAL na anasisitiza kuwa chaguo ni Tanzania na sivinginevyo. Ndg. Yoweri Kaguta alikwisha establish mazingira ya ujenzi huu kupitia Kenya muda mrefu tu hivyo analalazimika kuokoa hii hali kwa njia yeyote ikibidi kwa gharama.
 
Kama hataki anatufanya cc kama vipofu aende huko Kenya ila najua ges itamleta tena na halo ndipo atakapo pata machungu kweli kweli nasisi tutamfanyia hiv hiv
 
No, Mseveni is exploring an opportunity to strike the best deal.

Niwajibu wa Tz Kupambana kushinda hilo deal kwa FAIDA isijekuwa tu komoa Kenya baadae tukajuta.

Kuna faidi nyingi zinazungumzwa lakini Mpaka sasa sielewi Bomba la TAZAMA linatunufaishaje!
 
MsemajiUkweli,

Nothing personal but opportunities so, mambo eti "anataka kutugombanisha" hayana maana yoyote! Usihofu Mu7 leo kukutana na JPM na kesho na Kenyatta... ni la kawaida! Ni la kawaida coz' kuna kila dalili kwamba JPM &Mu7 WALIKUBALIANA kukutana but remember, unlike Mu7 & JPM, Kenyatta is a business man... a matured capitalist! Mtu mwenye kariba ya Kenyatta asingekaa kimya hata baada ya kuona Mu7 & JPM wanakutana kuashiria opportunity to Kenya is about to vanish in a thin air! Kenyatta kwa kariba yake ya ubepari alikuwa na kila sababu ya ku-fight back kwa kutaka kukutana na Mu-7... no offense and this's what I like about Kenyatta!! Mu-7 kwa upande wake hakuwa na sababu ya kukataa wito wa fellow EA President... kwahiyo hilo la leo anakutana na huyu na kesho anakutana na yule lisikusumbue... it's all about business!!

Kwa upande mwingine unadai hofu yako ishaanza kutimia baada ya Kenyan Team kuzuiwa kuingia Tanga Port!! Kwanza niwape hongera uongozi wa bandari ya Tanga! Ugandan Team ilienda Tanga port kufanya survey ili kujiridhisha ikiwa bandari husika ni muafaka kwao... je, hao Wakenya walienda kufanya nini kama co kutafuta madhaifu ya bandari ili wayauze kwa Uganda kama njia ya kuonesha ni namna gani bandari isivyofaa? I believe, ikiwa a Kenyan Team ni timu ambayo ina watu smart basi hawawezi ku-mind coz' tayari walishafahamu in advance kwamba Watanzania wataturuhusu kuingia Tanga Port IF AND ONLY IF THEY'RE STUPID & IDIOTS!

Way Foward: Badala ya kulia lia kwamba Mu-7 anataka kutugombanisha, tutumie muda huu kumu-encourage JPM aendelee kukaza coz' Kenyatta hatatulia hadi cku bomba la kwanza linatandikwa ardhini! Kwa mtu kama Kenyatta hataona taabu kwa issue za "give and take" coz hivyo ndivyo mambo yanavyoendeshwa. So, JPM na timu yake waki-relax kwa kudhani tayari Mu-7 keshakuwa wetu basi usishangae bomba likakunja kona to Mombasa. Na hapo c kwamba tutakuwa tumekwepesha migogoro among EA Member States bali tutakuwa Tume - expose our highest level of stupidity in front of fellow member states.

Last but not least hebu tuachane na hizi fikra za ujima! I repeat... no offense; ni suala la fursa tu hapa ndilo linagomba! Ni huyu huyu Kenyatta ndie alikuwa anahangaika kui-exclude Tanzania. Fitina zake zikawafanya akina PK waiingie kichwa kichwa kwenye Coalition of Willing (CoW ). Wana-JF wasioelewa wakaanza kuimba na kucheza tune za Kenya kwamba Watanzania ni waoga! Sie wengine ambao huwa tunaweka siasa pembeni yanapokuja masuala ya kitaifa na Uchumi; tukaiunga mkono serikali kwa kuendelea kukaza huku wasioelewa wakiikashifu serikali kwamba ipo slow bila kufahamu kwamba walichokuwa wanafanya Kenya ni kutaka kutuburuza na mwisho wa cku tunakuwa the loser coz we'd nothing to gain! Thanks to JK coz' pamoja na madhaifu yake yote lakini ameondoka akiwa ameshaisambaratisha the late Coalition of Willing manake hata Rwanda nao wameshajitoa tangu August 2015 kwenye mradi wa Standard Rail Gauge from Kigali to Mombasa na badala yake ni Kigali to Dar es salaam... no offense, it's all about business na hata Bepari Kenyatta anayafahamu hayo! Anachotakiwa kufanya JPM ni kuwa mwangalifu tu na Kenyatta lakini akileta mambo yake ya "Hapa Ni Kazi Tu" na kufanya maamuzi ya haraka kwa kila kitu ili aonekane "Hapa Kazi Tu....!" then trust me, tutakuwa kwenye lose side coz' as said above, Kenyatta hatatulia hadi tone lake la mwisho coz' hapa tunapoongea amepagawa kuona ikiwa Rwanda amerudi Dar kadhalika Mu -7 nae ndo huyooo to Tanga; now who'll economically utilize the standard gauge railway to Mombasa?! Kuna kila dalili ile reli ikaishia Nairobi at least for the next one decade manake kama inawezekana kutumia valves tofauti basi hata South Sudan wanaweza ku-opt kujenga bomba to Uganda ambalo linakuwa connected to Tanga or else, hizi ndizo fitina tunazotakiwa kuzipiga kwa sasa hata ikibidi kwa kuwapitishia mabomba yao hata half tax or tax credit coz' sisi tusivyofanya, Kenya can do it! Mbaya zaidi, current possible Kenyan Figures za kuwa Ikulu ya Nairobi ni Kenyatta na Odinga... hawa wote ni mabepari na hawana undugu mbele ya fursa!
Mkuu umeonesha ukomavu wa hali ya juu kuchambua hii ishu, na kuna ishu umezifukua ambazo binafsi sikujua kama zipo.

Hivi kumbe mpaka PK kesharudi tena kutuunga mkono kwenye reli yetu na Bandari yetu??

Mbona hii ishu imefanyika kimya kimya??
 
Didia nakuomba urudi shule. Kama ujui TZ wanavyo faidika. Mbali na kazi za bomba kule kunakopita.. Kodi ya bandari. Na mzigo unaopirishwa kwa pipa. nk
 
Napendekeza Magufuli na Kenyatta wakae kikao ambacho watakubaliana kumsusia M7 na bomba lake! Kama vipi alipitishe kwenye anga ya kimataifa! Haiwezekani M7 atugombanishe na ndugu zetu wakenya kwa misingi ya kibiashara! Huyu M7 haaminiki kabisa, huwezi kujadili biashara na watu Wawili kwa wakati mmoja! Huyu jamaa hana kabisa mshipa wa aibu!

wakenya ndugu zako tangu lini?... hao wanajitambulisha kama MANYANG'AU na dawa yao ni UNYANG'AU tu.
 
Kama hataki anatufanya cc kama vipofu aende huko Kenya ila najua ges itamleta tena na halo ndipo atakapo pata machungu kweli kweli nasisi tutamfanyia hiv hiv

Kwenda kule! This is business na tutaipata.
Pia acha fitna km umetumwa
 
Mnafiki ni wewe, na utakuwa Mkenya wewe.

Fitna katika biashara haikwepeki na fitna ni tafsiri ya mtu binafsi lakini neno linalstahili ni 'strategy'

Fahamu kuwa the issue is already resolved na issue ni usalama wa bomba, wewe huelewi nn hapo

Aksante kaka kwa kunipa cheo nisichokitamani duniani, labda kiswahili chako kimekuzwa katika mapokeo yenye mushkeli na "ashki" zinazotaka kukugombanisha na wenza. Hii inajionyesha jinsi unatumia meneno vibaya bila hata kufikiria, kwa mfano neno strategy kiswahili ni mkakati, sasa sijui ashki zako zinakutuma tofauti na sie wenzako.
Na pia katika biashara hakuna mkakati wa kukufanya upoteze dhamira na heshma yako, sio kila biashara unairukia bila kutizama nini kitakachojiri baadae. Nakupa mfano mmja tunalo bomba la TAZAMA Pipeline mbona wakati likijengwa hatukusikia chokochoko au mikakati ya kinafiki?
Hii ni biashara na ukumbuke Kenya suala la ardhi ni gumu saaana. Wenye maeneo ni watu wazito na wanajua utamu wa hii biashara. Mtu hakubali kupitisha bomba kwenye ardhi yake hivihivi, wanataka kukodisha ardhi sio kuuza vipande vya ardhi bomba likapowakuta watu walio hodhi ardhi.
Nyinyi mnataka kukurupuka kama kawaida yenu ili watu wenye maeneo yatayopitiwa na mradi yauzwe. Lazima mfikiri vizuri, kama umebahatika kuhodhi eneo liliwekwa mnara wa simu utakubailiana nami kwamba ni ujinga kuuza eneo. Dunia hii imebadilika leo hii vijiji linakopita lile bomba la TAZAMA hawapati hata pingili ya shilingi. Wewe unang'ang'ania fitna zisizo na mashiko.
 
Didia nakuomba urudi shule. Kama ujui TZ wanavyo faidika. Mbali na kazi za bomba kule kunakopita.. Kodi ya bandari. Na mzigo unaopirishwa kwa pipa. nk

Sasa shule si umetoa hapa? Unadhani Elimu ni darasani tu? Basi namimi nakupa shule Elimu inapatikana hata hapa JF

Anyway Shukrani
 
Hivi kweli kuna Mtanzania with good and sound mind ambaye anaamini kabisa kuwa East Africa Dream ni ukweli? Kwamba tutaungana baadaye tuwe nchi moja kwa msaada wa EU ambayo sasa hivi inazungumzia Brexit? Tanzania na Kenya zinashindania opportunities za land locked neighbours. Mtu ambaye hauoni huo ushindani, anajidanganya sana.
 
Ikumbukwe kuwa Jumuiya hii mpya ilizaliwa baada ya ile ya awali iliyoanzishwa mwaka 1968 na kuvunjika mwaka 1977 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kushindwa kuelewana kwa wakuu wa nchi wanachama kwa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere (Tanzania), Jommo Kenyatta (Kenya) na Idd Amin (Uganda).

Kile ambacho Uganda inakifanya kwa sasa kuhusu ‘’umalaya’’ katika maamuzi unajenga chuki kati ya Tanzania na Kenya.

Uganda inakuwa kama mwanamke anayetongozwa na wanaume wawili kutoka katika familia moja huku akimkubali kila mmoja. Mbaya zaidi, anajitokeza mbele ya kandamnasi na kusema huyu pia ni mwanamme wangu. Wananchi wengine wanabaki wanashangaa na kujiuliza, what’s going on?

Kinachotia wasiwasi, hatufahamu huyu mwanamke anaongea nini zaidi wakati akiwa ndani ya chumba kuhusu mwanamme mwingine anayedai pia anampenda.

Huu ujenzi wa bomba la mafuta unaweza kuleta matatizo makubwa katika mahusiano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ikumbukwe kuwa, Mwezi August, 2015 tulihabarishwa kuwa Kenya na Uganda wamekubaliana na kuweka saini kujenga hilo bomba la kusafirisha mafuta. Less than two months, on Oct 2015 tukaambiwa Uganda and Tanzania have signed an agreement to explore the possibility of building a crude oil pipeline between the two countries.

Mwezi March 1, 2016, Rais Magufuli na Rais Museveni wakaonekana mbele ya waandishi wa habari wakisema wamekubaliana kuhusu mpango wa kujengwa kwa bomba la kusafirisha mafuta kutoka bandari ya Tanga, Tanzania hadi Uganda.

March 14, 2016, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw. Javier Rielo alienda Ikulu Jijini Dar es Salaam na kumuhakikishia Rais Magufuli kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.

March 21, 2016, Tukaambiwa tena, Rais Kenyatta na Rais Museveni walikutana jijini Nairobi kujadili tena ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kati ya nchi hizo mbili. Mkutano huu ulifanyika siku chache tu baada ya Uganda na Tanzania kuafikiana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta kutoka bandari ya Tanga hadi nchini Uganda.

Kwa sasa jopo la wataalam wa Uganda wamebaki Kenya wakitembezwa huku na kule ili kujionea hali halisi ya fursa zitakazopatikana baada ya kujengwa bomba.

Kuna wengine wanaweza kudhani hili ni suala la kawaida lakini mimi ninaliona ni suala hatari sana katika mstakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ningemwelewa Rais Musevevi kama angekuwa anafanya huu ''umalaya'' kwa nchi ambazo haziko ndani ya EAC.

Rais Museveni anachochea ugomvi/uhasama sio kwa Marais wa Tanzania na Kenya pekee bali hata kwenye Mstakabali wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Rais Musevevi asikubaliwe kufanya biashara kwa mgongo wa kujenga chuki kati ya Tanzania na Kenya. Huu ni unafiki na uzandiki wa kiwango cha juu.

Someone must tell Rais Museveni to stop it, just play fair business game. He doesn't have to do all that mumbo jumbo.

UPDATE:
Niliyokuwa nahofia kutokea katika mahusiano kati ya Kenya na Tanzania kwa sababu ya ''umalaya'' wa Serikali ya uganda yameanza kutokea baada ya Waziri wa Kenya na kundi lake kuzuiwa na TISS kwenda kwenye Bandari ya Tanga baada ya kuwasili Airport.

Kwa habari kamili gonga hapa;

Tanzania tuna bomba la kusafirisha mafuta kupeleka Zambia mpaka sasa hivi kuna faida ya kipekee sana ambayo nchi inaweza kujivunia kwa bomba hilo kupita katika ardhi yetu. Nchi hii ina resources nyingi sana za kuifanya ipae kiuchumi... agriculture, tourism, mining, to mention a few. Kama Kenya wanaona hilo bomba ni deal sana ... lets just decline
 
Back
Top Bottom