Rais Museveni anachochea chuki baina ya Tanzania na Kenya

Rais Museveni anachochea chuki baina ya Tanzania na Kenya

Biashara ni kufukuzia Fursa. Mimi ni machinga mtaji wangu wa kupata wateja huwa si kile ninachokiuza bali ni jinsi gani ninavyokiuza hicho kitu. Kama wakenya wameweza kufukuzia hiyo fursa ya kujenga hilo bomba tusimlaumu Museveni ambaye kama mteja siku zote hutafuta unafuu wa bei kwa ubora ule ule wa kitu anachokitafuta sokoni. Bali sisi tuwalaumu viongozi wetu kwa uzembe!!
Sikatai kuwa biashara ni kufukuzia fursa lakini pia naomba uelewe fursa zina mipaka yake.

Hata wale wajuzi wa biashara wanafahamu na kuheshimu kuwa biashara lazima ziwe na regurations, compassionate and also avoid moral hazard.
 
Sikatai kuwa biashara ni kufukuzia fursa lakini pia naomba uelewe fursa zina mipaka yake.

Hata wale wajuzi wa biashara wanafahamu na kuheshimu kuwa biashara lazima ziwe na regurations and also avoid moral hazard.
Kwa vyovyote vile kwenye biashara fursa ni lazima zifukuziwe!!
 
Kwani lazima tuunge bomba nao?!

Kama vipi tuwapige chini.

Sisi wenyewe tuna mafuta sema hatujataka kufuatilia ki hivyo, kwa kuwa bado tumelewa na gesi ya Mtwara.
Tatizo ni Rais Museveni kuja tena Tanzania kutaka kufanya maongezi kuhusu bomba la Mafuta wakati walikuwa wamekubaliana na serikali ya Kenya.
 
Ni kweli kabisa mkuu.
Imefika wakati Magufuli aache kujifungia Magogoni, atoke akatafute Fursa, kwani akikanyaga mafuta kwa ndege yake mpaka pale Kampala kuonana na Museveni akamuweka sawa kuna tatizo gani??

Ikiwezekana hata kutenga bandari ya Tanga ikawa maalumu kwa ajili ya mizigo ya Uganda na Sudani ya Kusini na Rwanda hii inawezekana kabisa, sisi tukawa wakusanya mchuzi tu operations zote wanafanya wao.

Zama za ujamaa wa Nyerere zishapita, Nyerere na ujamaa wake washajifia, ni wakati wa kufanya mambo kibepari bepari tu, hakuna kumuangalia mtu usomi hata kama ni jirani yako linapofika suala la Business

Ziara moja tu ya Rais Magufuli na Officials wake katika maswala hayo itafunga kazi kabisa, Mkenya hatajisumbua tena.
Amini nakwambieni Magu ni kama Obama wa Afrika, ana Influence ya ajabu!
Jambo moja tu, waende wakijua wameenda vitani kupambana na kuua ili kurudi wakiwa washindi, hayo mambo ya 'influence' ni kifuniko tu'
 
Hivi ukiwa umesaini mkataba wa kununua magari kumi ya kampuni........pale Toyota kwa $$500,000.......kesho yake akaja Nissan kwa magari yale yale akakupa offer ya $$350,000...utafanya nini?

Mkuu kikubwa watanzania tuache politics. Tufanye biashara...ulimwengu wa leo ni kunyang'anyana tonge mdomoni. Ndo maana Japan na China wanagombea miradi ya ujenzi wa reli au barabara kama watoto wanaogombea sambusa! (mifano hai..India, Indonesia nk).. Hebu jitahidi kusoma upanue wigo wako. Hapa watanzania lazima tuamke...hapendwi mtu..ni pesa yako tuu.
Unaposema tuache kuongelea politics sifahamu una maana gani wakati kilichoelekea kuathirika katika kadhia hii ni politics za EAC.

Mimi nisingekuwa na tatizo kama hii biashara ingekuwa inahusu nchi mbili ambazo mmoja hayupo kwenye EAC kama mfano wako uliotoa kuhusu China na Japan.

Anachofanya Rais Musevevi ni kama kukubali kutongozwa/kutongoza wanamme wawili kutoka familia moja na mbaya zaidi, wote anawaambia amewakubali.
 
Ikumbukwe kuwa Jumuiya hii mpya ilizaliwa baada ya ile ya awali iliyoanzishwa mwaka 1968 na kuvunjika mwaka 1977 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kushindwa kuelewana kwa wakuu wa nchi wanachama kwa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere (Tanzania), Jommo Kenyatta (Kenya) na Idd Amin (Uganda).

Kile ambacho Uganda inakifanya kwa sasa kuhusu ‘’umalaya’’ katika maamuzi unajenga chuki kati ya Tanzania na Kenya.

Uganda inakuwa kama mwanamke anayetongozwa na wanaume wawili kutoka katika familia moja huku akimkubali kila mmoja. Mbaya zaidi, anajitokeza mbele ya kandamnasi na kusema huyu pia ni mwanamme wangu. Wananchi wengine wanabaki wanashangaa na kujiuliza, what’s going on?

Kinachotia wasiwasi, hatufahamu huyu mwanamke anaongea nini zaidi wakati akiwa ndani ya chumba kuhusu mwanamme mwingine anayedai pia anampenda.

Huu ujenzi wa bomba la mafuta unaweza kuleta matatizo makubwa katika mahusiano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ikumbukwe kuwa, Mwezi August, 2015 tulihabarishwa kuwa Kenya na Uganda wamekubaliana na kuweka saini kujenga hilo bomba la kusafirisha mafuta. Less than two months, on Oct 2015 tukaambiwa Uganda and Tanzania have signed an agreement to explore the possibility of building a crude oil pipeline between the two countries.

Mwezi March 1, 2016, Rais Magufuli na Rais Museveni wakaonekana mbele ya waandishi wa habari wakisema wamekubaliana kuhusu mpango wa kujengwa kwa bomba la kusafirisha mafuta kutoka bandari ya Tanga, Tanzania hadi Uganda.

March 14, 2016, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw. Javier Rielo alienda Ikulu Jijini Dar es Salaam na kumuhakikishia Rais Magufuli kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.

March 21, 2016, Tukaambiwa tena, Rais Kenyatta na Rais Museveni walikutana jijini Nairobi kujadili tena ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kati ya nchi hizo mbili. Mkutano huu ulifanyika siku chache tu baada ya Uganda na Tanzania kuafikiana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta kutoka bandari ya Tanga hadi nchini Uganda.

Kwa sasa jopo la wataalam wa Uganda wamebaki Kenya wakitembezwa huku na kule ili kujionea hali halisi ya fursa zitakazopatikana baada ya kujengwa bomba.

Kuna wengine wanaweza kudhani hili ni suala la kawaida lakini mimi ninaliona ni suala hatari sana katika mstakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ningemwelewa Rais Musevevi kama angekuwa anafanya huu ''umalaya'' kwa nchi ambazo haziko ndani ya EAC.

Rais Museveni anachochea ugomvi/uhasama sio kwa Marais wa Tanzania na Kenya pekee bali hata kwenye Mstakabali wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Rais Musevevi asikubaliwe kufanya biashara kwa mgongo wa kujenga chuki kati ya Tanzania na Kenya. Huu ni unafiki na uzandiki wa kiwango cha juu.

Someone must tell Rais Museveni to stop it, just play fair business game. He doesn't have to do all that mumbo jumbo.


LABDA ANATAKA JENGA MAWILI MOJA KENYA NA JINGINE TANZANIA. WHO KNOWS?
 
MAFUTA YANA LAANA!! YAKIPATIKANA NA BUNDUKI NYUMA INAFATA, KAMA SIO AMERIKA(LIBYA,IRAQ),WENYEWE KWA WENYEWE (SUDAN,NIGERIA) SITAKI MAFUTA KABISA HAPA KWETU.....
Kuna ukweli ndani yake!

Hii watalaam wa uchumi wanatuambia ni paradox of plenty!

Kwa sasa tumeanza kurumbana na kufitinishana kwenye kujenga bomba la kusafirisha mafuta!
 
Hivi ukiwa umesaini mkataba wa kununua magari kumi ya kampuni........pale Toyota kwa $$500,000.......kesho yake akaja Nissan kwa magari yale yale akakupa offer ya $$350,000...utafanya nini?

Mkuu kikubwa watanzania tuache politics. Tufanye biashara...ulimwengu wa leo ni kunyang'anyana tonge mdomoni. Ndo maana Japan na China wanagombea miradi ya ujenzi wa reli au barabara kama watoto wanaogombea sambusa! (mifano hai..India, Indonesia nk).. Hebu jitahidi kusoma upanue wigo wako. Hapa watanzania lazima tuamke...hapendwi mtu..ni pesa yako tuu.
safi sana mkuu tuendelee kuelimisha
 
acheni uongo lini Uganda walidai Mlima kilimanjaro upo kwao au lini uganda walidai olduvai gorge ipo kwao wachochezi ni wakenya walifikiri tukirudisha hii jumhiya wao ndio watakuwa na sauti isitoshe kenya ndio alishawishi rwanda na uganda waanze kupitishia bidhaa kwenye bandari yake na hii iliwezekana kwa sababu tulikuwa na kiongozi asiye na vision leo tumepata kiongozi mchapakazi ndio waseme museveni ni mchonganishi jamani watanzania tunatakiwa kuelewa east africa comunity ipo kiuchumi zaidi na sio siasa
 
Tujenge tu bomba, Museveni akitukubali tufanye naye business, akitukataa tunalibadilishia matumizi liwe bomba la maji, lisaidie kusambaza maji vijijini
Are you serious?

Tanzania haijengi bomba ila inatumiwa tu ardhi yake kupitishia bomba!
 
Kwasasa mambo ya kulialia hayana nafasi
Ni kwenda ki Nyang'au hivyo hivyo
Unajua hawa Wakenya wamesha tuzoea sana
Niwakati na sisi Watanzania tuamke.
Huu mradi ni mzuri sana
$14 kwa pipa ×200000
Kwa siku nimchongo mzuri.
Tusi kae tuanze kuufuatilia kwa nguvu kama wafanyavyo wakenya
Sidhani kama ni haki kuwalaumu Wakenya kwenye hii kadhia wakati wao ndio walikuwa wa kwanza kufanya makubaliano na Uganda kabla yetu.

Mwenye kubeba lawama ni Rais Museveni kwa kufanya biashara kama ya ''umalaya'' kwenye familia moja.

Matendo ya Rais Museveni yanachochea chuki ndani ya EAC na hasa kati ya Tanzania na Kenya.
 
Kwenye kadhia hii siwezi kutoa lawama kwa Kenya kwa sababu mwenye uwezo kwa kumzuia Kenya au kumkubalia ni Uganda.

Kama Uganda alikubaliana na Kenya, hakutakiwa kuja tena Tanzania na kuanza mazungumzo kuhusu suala ambalo walikuwa wamekubaliana na Kenya.

Hata pale Uganda alipokubaliana na Tanzania, hakukuwa na umuhimu tena wa Uganda kwenda Kenya kuanza mazungumzo mengine. Mbaya zaidi, hizi sarakasi zinafanyika ndani ya nchi wanachama wa EAC.

Huu ndio ''umalaya'' ninaosema.


Hapa tunamlaumu bure Yoweri Kaguta, huyu jamaa yetu maji ya shingo yamemfika. Uchimbaji wa mafuta Uganda unahusisha makampuni makubwa mawili TULLOW na TOTAL kiuhalisia TOTAL ndio mwenye mtaji mkubwa hivyo ana turufu. TOTAL ameamua kupitisha bomba Tanzania, Na TULLOW ameonyesha interest ya uchimbaji mafuta Kenya. Hapo Bw. Yoweri Kaguta anahaha kunusuru mambo, tumuonee huruma jamani!!!!!!
 
Kama Mseveni anawataka Wakenya, mwacheni . Sisi tuingie mazungumzo na nchi zingine zinazoweza kuhitaji tena kwa tija zaidi huduma hii. Ziko nchi nyingi zaidi ya Uganda ambazo hazina bahari.

Kizuri hata Kampala inachelewa tu kwa kuwa huwezi kufanya kitu cha kuaminika na Nairobi.
Tatizo la Rais Museveni ni kukubaliana na Kenya halafu tena anakuja Tanzania kuanza mazungumzo na kukubaliana tena. Baada ya wiki moja anaenda tena Kenya na kuanza mazungumzo mengine zaidi.

Kutokuwa na msimamo katika suala hili ninaamini kutasababisha pia chuki ndani ya nchi wanachama wa EAC.
 
Mazee hii ishu si yamchezo.Pini waliyopigwa leo wakenya pale airport ya Tanga si mchezo.Waziri wa nishati wa uganda leo amekuja tanga kwa usafiri wa anga.Kumbe wakenya nao wamejileta ili wasome ramani za kila kitu kinachoendelea. Tena mpka gharama za huyu waziri pamoja na wao wenyewe imelipwa na wizara ya nishati ya kenya.Sasa walivofika tu airport migration wako kama mvua.Kilichofanyika ni kuwaruhusu wananchi wauganda na wazungu wao kupita lakini wote wale wakenya walinyang'anywa passport zao na kuambiwa mtangoja hapa VIP LOUNGE,mpaka hawa wengine warudi. So waganda na uongozi wa gvt ya tanzania walienda kufanya yao.Waziri wao wa nishati na timu yake walibaki wanatoa macho.Mazee tz tuiache ilivo...hili tikio leo lilikuwa lakimafya sana sana.Ni mengi..ila chkueni hayo machache.
 
Naona mambo ya Unyumbu pembeni
Leo naunga Mkono hoja
Mambo ya kulialia Watanzania tuyaache
Hii fursa itakuwa aibu na hasara ikitupita kushoto
Sidhani kama Watanzania wanalia lia bali wengine tunajaribu kuangalia kadhia hii kwa upana zaidi.

Ni vizuri kuwa ambitious lakini pia ambitious without compassionate hasa kwenye jumuiya moja ni kutengeneza chuki na kutokuaminiana.

Rais Museveni anaweza kukipata kila anachokitafuta kwa faida kubwa lakini swali la kujiuliza, At what cost?
 
Back
Top Bottom