Rais Museveni anachochea chuki baina ya Tanzania na Kenya

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Ikumbukwe kuwa Jumuiya hii mpya ilizaliwa baada ya ile ya awali iliyoanzishwa mwaka 1968 na kuvunjika mwaka 1977 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kushindwa kuelewana kwa wakuu wa nchi wanachama kwa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere (Tanzania), Jommo Kenyatta (Kenya) na Idd Amin (Uganda).

Kile ambacho Uganda inakifanya kwa sasa kuhusu ‘’umalaya’’ katika maamuzi unajenga chuki kati ya Tanzania na Kenya.

Uganda inakuwa kama mwanamke anayetongozwa na wanaume wawili kutoka katika familia moja huku akimkubali kila mmoja. Mbaya zaidi, anajitokeza mbele ya kandamnasi na kusema huyu pia ni mwanamme wangu. Wananchi wengine wanabaki wanashangaa na kujiuliza, what’s going on?

Kinachotia wasiwasi, hatufahamu huyu mwanamke anaongea nini zaidi wakati akiwa ndani ya chumba kuhusu mwanamme mwingine anayedai pia anampenda.

Huu ujenzi wa bomba la mafuta unaweza kuleta matatizo makubwa katika mahusiano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ikumbukwe kuwa, Mwezi August, 2015 tulihabarishwa kuwa Kenya na Uganda wamekubaliana na kuweka saini kujenga hilo bomba la kusafirisha mafuta. Less than two months, on Oct 2015 tukaambiwa Uganda and Tanzania have signed an agreement to explore the possibility of building a crude oil pipeline between the two countries.

Mwezi March 1, 2016, Rais Magufuli na Rais Museveni wakaonekana mbele ya waandishi wa habari wakisema wamekubaliana kuhusu mpango wa kujengwa kwa bomba la kusafirisha mafuta kutoka bandari ya Tanga, Tanzania hadi Uganda.

March 14, 2016, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw. Javier Rielo alienda Ikulu Jijini Dar es Salaam na kumuhakikishia Rais Magufuli kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.

March 21, 2016, Tukaambiwa tena, Rais Kenyatta na Rais Museveni walikutana jijini Nairobi kujadili tena ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kati ya nchi hizo mbili. Mkutano huu ulifanyika siku chache tu baada ya Uganda na Tanzania kuafikiana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta kutoka bandari ya Tanga hadi nchini Uganda.

Kwa sasa jopo la wataalam wa Uganda wamebaki Kenya wakitembezwa huku na kule ili kujionea hali halisi ya fursa zitakazopatikana baada ya kujengwa bomba.

Kuna wengine wanaweza kudhani hili ni suala la kawaida lakini mimi ninaliona ni suala hatari sana katika mstakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ningemwelewa Rais Musevevi kama angekuwa anafanya huu ''umalaya'' kwa nchi ambazo haziko ndani ya EAC.

Rais Museveni anachochea ugomvi/uhasama sio kwa Marais wa Tanzania na Kenya pekee bali hata kwenye Mstakabali wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Rais Musevevi asikubaliwe kufanya biashara kwa mgongo wa kujenga chuki kati ya Tanzania na Kenya. Huu ni unafiki na uzandiki wa kiwango cha juu.

Someone must tell Rais Museveni to stop it, just play fair business game. He doesn't have to do all that mumbo jumbo.

UPDATE:
Niliyokuwa nahofia kutokea katika mahusiano kati ya Kenya na Tanzania kwa sababu ya ''umalaya'' wa Serikali ya uganda yameanza kutokea baada ya Waziri wa Kenya na kundi lake kuzuiwa na TISS kwenda kwenye Bandari ya Tanga baada ya kuwasili Airport.

Kwa habari kamili gonga hapa;
Tanzania on Wednesday confiscated the passports of top Kenyan officials, including Energy Cabinet Secretary Charles Keter, and denied them access to the port of Tanga. However, a delegation from Uganda, led by Energy minister Irene Muloni was allowed to proceed with the tour unmolested.

The top Kenyan officials had began their journey in Lamu, where they inspected the proposed Lamu port before flying to the port of Tanga in Tanzania. The trip was part of their mission to unlock a deadlock between Kenya and Uganda over whether a proposed oil pipeline to export Uganda’s oil would pass through Kenya or Tanzania.

Wednesday’s incident turned the quest for Kenya to retain the crude pipeline ugly.
 
Ikumbukwe kuwa Jumuiya hii mpya ilizaliwa baada ya ile ya awali iliyoanzishwa mwaka 1968 na kuvunjika mwaka 1977 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kushindwa kuelewana kwa wakuu wa nchi wanachama kwa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere (Tanzania), Jommo Kenyatta (Kenya) na Idd Amin (Uganda).

Kile ambacho Uganda inakifanya kwa sasa kuhusu ‘’umalaya’’ katika maamuzi unajenga chuki kati ya Tanzania na Kenya.

Uganda inakuwa kama mwanamke anayetongozwa na wanaume wawili huku akimkubali kila mmoja. Mbaya zaidi, anajitokeza mbele ya kandamnasi na kusema huyu pia ni mwanamme wangu. Wananchi wengine wanabaki wanashangaa na kujiuliza, what’s going on?

Kinachotia wasiwasi, hatufahamu huyu mwanamke anaongea nini zaidi wakati akiwa ndani ya chumba kuhusu mwanamme mwingine anayedai pia anampenda.

Huu ujenzi wa bomba la mafuta unaweza kuleta matatizo makubwa katika mahusiano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Ikumbukwe kuwa, Mwezi August, 2015 tulihabarishwa kuwa Kenya na Uganda wamekubaliana na kuweka saini kujenga hilo bomba la kusafirisha mafuta. Less than two months, on Oct 2015 tukaambiwa Uganda and Tanzania have signed an agreement to explore the possibility of building a crude oil pipeline between the two countries.

Mwezi March 1, 2016, Rais Magufuli na Rais Museveni wakaonekana mbele ya waandishi wa habari wakisema wamekubaliana kuhusu mpango wa kujengwa kwa bomba la kusafirisha mafuta kutoka bandari ya Tanga, Tanzania hadi Uganda.

March 14, 2016, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Total Afrika Mashariki Bw. Javier Rielo alienda Ikulu Jijini Dar es Salaam na kumuhakikishia Rais Magufuli kuwa kampuni hiyo itaanza ujenzi wa mradi wa bomba la kusafirisha mafuta haraka iwezekanavyo, kwa kuwa fedha za kutekeleza mradi huo zipo.

March 21, 2016, Tukaambiwa tena, Rais Kenyatta na Rais Museveni walikutana jijini Nairobi kujadili tena ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kati ya nchi hizo mbili. Mkutano huu ulifanyika siku chache tu baada ya Uganda na Tanzania kuafikiana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta kutoka bandari ya Tanga hadi nchini Uganda.

Kwa sasa jopo la wataalam wa Uganda wamebaki Kenya wakitembezwa huku na kule ili kujionea hali halisi ya fursa zitakazopatikana baada ya kujengwa bomba.

Kuna wengine wanaweza kudhani hili ni suala la kawaida lakini mimi ninaliona ni suala hatari sana katika mstakabali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais Museveni anachochea ugomvi/uhasama sio kwa Marais wa Tanzania na Kenya pekee bali hata kwenye Mstakabali wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.

Rais Musevevi asikubaliwe kufanya biashara kwa mgongo wa kujenga chuki kati ya Tanzania na Kenya. Huu ni unafiki na uzandiki wa kiwango cha juu.

Someone must tell Rais Museveni to stop it, just play fair business game. He doesn't have to do all that mumbo jumbo.
Tatizo sio mseven tatizo ni Tullow oil kutaka kuchimba mafuta kenya. Total kaona mwenzie anamletea ujanja uganda wako wote mwenzie alivyoenda kenya kamweka kando sasa total anapiga mkasi tuone tullow oil atatokea wapi, mchina nae kaona tullow oil kamwacha solemba kwanini uganda wawe wote imefika kenya anakula winga.
 
Biashara ni kufukuzia Fursa. Mimi ni machinga mtaji wangu wa kupata wateja huwa si kile ninachokiuza bali ni jinsi gani ninavyokiuza hicho kitu. Kama wakenya wameweza kufukuzia hiyo fursa ya kujenga hilo bomba tusimlaumu Museveni ambaye kama mteja siku zote hutafuta unafuu wa bei kwa ubora ule ule wa kitu anachokitafuta sokoni. Bali sisi tuwalaumu viongozi wetu kwa uzembe!!
 
Kwani lazima tuunge bomba nao?!

Kama vipi tuwapige chini.

Sisi wenyewe tuna mafuta sema hatujataka kufuatilia ki hivyo, kwa kuwa bado tumelewa na gesi ya Mtwara.
 
Hivi ukiwa umesaini mkataba wa kununua magari kumi ya kampuni........pale Toyota kwa $$500,000.......kesho yake akaja Nissan kwa magari yale yale akakupa offer ya $$350,000...utafanya nini?

Mkuu kikubwa watanzania tuache politics. Tufanye biashara...ulimwengu wa leo ni kunyang'anyana tonge mdomoni. Ndo maana Japan na China wanagombea miradi ya ujenzi wa reli au barabara kama watoto wanaogombea sambusa! (mifano hai..India, Indonesia nk).. Hebu jitahidi kusoma upanue wigo wako. Hapa watanzania lazima tuamke...hapendwi mtu..ni pesa yako tuu.
 
Huyu mzee Museveni naona anataka kuwachezea hawa vijana Kenyatta na Magufuli. Si ajabu anataka kitu kidogo. Kwa Magufuli hapati kitu labda Kenyatta maana nasikia Kenya ni nchi ya kitu kidogo.
Mchezo anaofanya ni mbaya sana!

Mbaya zaidi, kila upande anaweka signature ya MOU and acceptance of an offer!
 
Fitna ndo mtaji wa wakenya. Nasi inabidi twende kwa style hi yo hiyo. Kuliko kubaki kulia lia.
Kwenye kadhia hii siwezi kutoa lawama kwa Kenya kwa sababu mwenye uwezo kwa kumzuia Kenya au kumkubalia ni Uganda.

Kama Uganda alikubaliana na Kenya, hakutakiwa kuja tena Tanzania na kuanza mazungumzo kuhusu suala ambalo walikuwa wamekubaliana na Kenya.

Hata pale Uganda alipokubaliana na Tanzania, hakukuwa na umuhimu tena wa Uganda kwenda Kenya kuanza mazungumzo mengine. Mbaya zaidi, hizi sarakasi zinafanyika ndani ya nchi wanachama wa EAC.

Huu ndio ''umalaya'' ninaosema.
 
Kwasasa mambo ya kulialia hayana nafasi
Ni kwenda ki Nyang'au hivyo hivyo
Unajua hawa Wakenya wamesha tuzoea sana
Niwakati na sisi Watanzania tuamke.
Huu mradi ni mzuri sana
$14 kwa pipa ×200000
Kwa siku nimchongo mzuri.
Tusi kae tuanze kuufuatilia kwa nguvu kama wafanyavyo wakenya
 
Kwenye kadhia hii siwezi kutoa lawama kwa Kenya kwa sababu mwenye uwezo kwa kumzuia Kenya au kumkubalia ni Uganda.

Kama Uganda alikubaliana na Kenya, hakutakiwa kuja tena Tanzania na kuanza mazungumzo kuhusu suala ambalo walikuwa wamekubaliana na Kenya.

Hata pale Uganda alipokubaliana na Tanzania, hakukuwa na umuhimu tena wa Uganda kwenda Kenya kuanza mazungumzo mengine. Mbaya zaidi, hizi sarakasi zinafanyika ndani ya nchi wanachama wa EAC.

Kama Mseveni anawataka Wakenya, mwacheni . Sisi tuingie mazungumzo na nchi zingine zinazoweza kuhitaji tena kwa tija zaidi huduma hii. Ziko nchi nyingi zaidi ya Uganda ambazo hazina bahari.

Kizuri hata Kampala inachelewa tu kwa kuwa huwezi kufanya kitu cha kuaminika na Nairobi.
 
Biashara ni kufukuzia Fursa. Mimi ni machinga mtaji wangu wa kupata wateja huwa si kile ninachokiuza bali ni jinsi gani ninavyokiuza hicho kitu. Kama wakenya wameweza kufukuzia hiyo fursa ya kujenga hilo bomba tusimlaumu Museveni ambaye kama mteja siku zote hutafuta unafuu wa bei kwa ubora ule ule wa kitu anachokitafuta sokoni. Bali sisi tuwalaumu viongozi wetu kwa uzembe!!
Naona mambo ya Unyumbu pembeni
Leo naunga Mkono hoja
Mambo ya kulialia Watanzania tuyaache
Hii fursa itakuwa aibu na hasara ikitupita kushoto
 
Kwani lazima tuunge bomba nao?!

Kama vipi tuwapige chini.

Sisi wenyewe tuna mafuta sema hatujataka kufuatilia ki hivyo, kwa kuwa bado tumelewa na gesi ya Mtwara.
Hayo mawazo niyakijinga kwasasa
Unatakiwa kwenda na wakati muda ndio huu.
Kwanza anza na fursa iliopo kisha uangalie nyingine
 
Hivi ukiwa umesaini mkataba wa kununua magari kumi ya kampuni........pale Toyota kwa $$500,000.......kesho yake akaja Nissan kwa magari yale yale akakupa offer ya $$350,000...utafanya nini?

Mkuu kikubwa watanzania tuache politics. Tufanye biashara...ulimwengu wa leo ni kunyang'anyana tonge mdomoni. Ndo maana Japan na China wanagombea miradi ya ujenzi wa reli au barabara kama watoto wanaogombea sambusa! (mifano hai..India, Indonesia nk).. Hebu jitahidi kusoma upanue wigo wako. Hapa watanzania lazima tuamke...hapendwi mtu..ni pesa yako tuu.
Bado mijitu inakalia ujirani,utu, sijui kujuana Mara jumuia
Tubadilike sasa
Hii nikama vita
 
Back
Top Bottom