Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,868
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema anaweza kufuta Bunge la nchi hiyo, amemwambia Spika Rebecca Kadaga kuwa asifikirie yuko Peponi anapokuwa Bungeni na anapaswa kufahamu chimbuko la Bunge hilo, mwaka 1971 - 1979 Uganda hakukuwa na Bunge. Unalitazamaje jambo hili? #KwanzaHabari
=====
RAIS MUSEVENI AONYA KUWA ANAWEZA KULIFUTA BUNGE LA NCHI HIYO
Ametoa kauli hiyo alipokuwa akipinga mjadala unaotarajiwa kufanyika juu ya matokeo ya uchunguzi wa Bunge katika vurugu zilizotokea Arua na kusababisha Wabunge na baadhi ya viongozi kupigwa kikatili
Museveni ameripotiwa kutoa vitisho hivyo wakati akiwahutubia Wabunge wa Chama tawala katika ukumbi wa Ikulu mnamo Agosti 27 huku akiwaonya kuwa wafanye machaguo yao kwa umakini
Alisema katika mwaka 1971 hadi 1979(Wakati wa uongozi wa Idd Amini) hakukuwa na Bunge, hivyo Wabunge hao wasidhani wapo Mbinguni wafanye kile kilichowapeleka Bungeni na si vinginevyo
Aidha, Rais Museveni alimshangaa Spika wa Bunge, Rebecca Kadaga kwa kuunda tume ya kuchunguza suala la kupigwa kwa viongozi wakati suala hilo likiwa bado Mahakamani
Bunge linatarajia kujadili matokeo ya uchunguzi uliofanya na Kamati iliyoundwa na Spika kabla ya suala hilo kusahaulika