Rais Museven amuonya Spika wa Bunge kuwa anaweza kulifuta Bunge

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,492
2,000
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema anaweza kufuta Bunge la nchi hiyo, amemwambia Spika Rebecca Kadaga kuwa asifikirie yuko Peponi anapokuwa Bungeni na anapaswa kufahamu chimbuko la Bunge hilo, mwaka 1971 - 1979 Uganda hakukuwa na Bunge. Unalitazamaje jambo hili? #KwanzaHabari
=====

RAIS MUSEVENI AONYA KUWA ANAWEZA KULIFUTA BUNGE LA NCHI HIYO

Ametoa kauli hiyo alipokuwa akipinga mjadala unaotarajiwa kufanyika juu ya matokeo ya uchunguzi wa Bunge katika vurugu zilizotokea Arua na kusababisha Wabunge na baadhi ya viongozi kupigwa kikatili

Museveni ameripotiwa kutoa vitisho hivyo wakati akiwahutubia Wabunge wa Chama tawala katika ukumbi wa Ikulu mnamo Agosti 27 huku akiwaonya kuwa wafanye machaguo yao kwa umakini

Alisema katika mwaka 1971 hadi 1979(Wakati wa uongozi wa Idd Amini) hakukuwa na Bunge, hivyo Wabunge hao wasidhani wapo Mbinguni wafanye kile kilichowapeleka Bungeni na si vinginevyo

Aidha, Rais Museveni alimshangaa Spika wa Bunge, Rebecca Kadaga kwa kuunda tume ya kuchunguza suala la kupigwa kwa viongozi wakati suala hilo likiwa bado Mahakamani

Bunge linatarajia kujadili matokeo ya uchunguzi uliofanya na Kamati iliyoundwa na Spika kabla ya suala hilo kusahaulika
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
32,138
2,000
Huo ndio unaitwa ulevi wa madaraka, Museveni atatolewa kwa bunduki tu na sio kwa hivi vikaratasi.
Umeniwahi. Ni nadra sana kwa viongozi walevi wa madaraka kukubaliana na bunge. Na kwa mwenendo wa huyo Museveni ni nguvu ya umma tu itakayomtoa madarakani. Viashiria vya kiongozi mkuu wa nchi kutoliheshimu bunge vinaonekana hata pande hizi.
 

Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
11,193
2,000
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema anaweza kufuta Bunge la nchi hiyo, amemwambia Spika Rebecca Kadaga kuwa asifikirie yuko Peponi anapokuwa Bungeni na anapaswa kufahamu chimbuko la Bunge hilo, mwaka 1971 - 1979 Uganda hakukuwa na Bunge. Unalitazamaje jambo hili? #KwanzaHabari
Basically bunge lenenyewe linaweza kumuondoa madarakani muda wowote wakitaka. Kiufup bunge lina nguv kuliko yeye mwenyewe.

So asichimbe biti viongozi
 

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
18,629
2,000
Huyo siku zake zinahesabika hatua anazipiga shatani yupo nyuma yake kishamchoka mwenzie huku kaamza kuropoka hovyo kumbe gesi waligawa kwa mabepari
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom