Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe Jakaya Kikwete atunukiwa medali kwa mchango wake katika harakati za kurejesha amani nchini Burundi

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,402
2,000
Rais wa Burundi, Mhe. Evariste Ndayishimiye amemtunuku medali Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe Jakaya Kikwete kwa mchango wake katika harakati za kurejesha amani nchini Burundi.

kIKWETE.jpg

Chanzo: ForeignTanzania

Sisi akina Mzukulu tunaomba tuambiwe haraka kama Rais Mstaafu huyu Jakaya M Kikwete ana Vinasaba vya Uhutu kutoka nchini huko Burundi.
 
ligend

JF-Expert Member
Oct 14, 2019
472
1,000
Ni mapenzi binafsi tu, na pia jeshi la Burundi lina wabongo wengi sana na ujue kuwa BURUNDI ndo inajipendekeza kwa bongo.
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
9,450
2,000
Rais wa Burundi, Mhe. Evariste Ndayishimiye amemtunuku medali Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe Jakaya Kikwete kwa mchango wake katika harakati za kurejesha amani nchini Burundi.

Chanzo: ForeignTanzania

Sisi akina Mzukulu tunaomba tuambiwe haraka kama Rais Mstaafu huyu Jakaya Mrisho Kikwete ana Vinasaba vya Uhutu kutoka nchini huko Burundi.

CHAPISHO zuri lakini muda umekwenda...

Mpwaa naona unatutafuta ubaya wee kwi kwi kwi....
Kwa harakaharaka;

Wahutu Wahutu Wahutu Wahutu

Miaka mingi nyuma huko,baadhi ya WAAFRIKA WEUSI TII waliokuwa WANAISHI CAMEROON ya sasa waliamua kutafuta maeneo mengine yenye rutuba na Hali ya hewa nzuri.
Kama KAWAIDA ya misigano ya Koo na Vita vya kikabila,msukumo huo ULIWAFIKISHA MAENEO YA GABON,wengine walifika afrika ya Kati,wengine wakafika eneo la Kongo ya Brazaville,Ruanda na Urundi ya sasa na wengi wakafikia misitu ya Kongo Kinshasa.

WATU HAWA NDIO WALIOKUJA KUITWA WABANTU...

WABANTU wakasambaa mashariki na kusini mwa ziwa Tanganyika,wakazaliana hapa Tanganyika,Uganda,Kenya,Zambia,Malawi,Msumbiji,Zimbabwe,Lesotho,Eswatini,Namibia mpaka Afrika ya kusini.

Makabila yote ya Tanzania kasoro machache kabisa yakaieneza asili yao ya UBUNTU.....

KIASILI WABANTU NI WAFUGAJI ILA SI KWA UKUBWA SANA.HAWA WANAISHI KWA KUWINDA,KURINA ASALI NA KULIMA.

Ukiwaangalia utauona wajihi wao wa weusi wa RANGI ya kukoza, KAVU ISIYOMETAMETA.Wana vimo vifupi,vifua vipana,mikono yenye nguvu,kule juu shingo zao ni fupi,vichwa vikubwa na mviringo,usoni pua kubwa pana na bapa.Macho yao madogo na ya saizi ya Kati,pia ya rangi nyeusi.Wana nywele nyeusi,kavu na kipilipili.

NITAENDELEA
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
42,980
2,000
Rais wa Burundi, Mhe. Evariste Ndayishimiye amemtunuku medali Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe Jakaya Kikwete kwa mchango wake katika harakati za kurejesha amani nchini Burundi.

Chanzo: ForeignTanzania

Sisi akina Mzukulu tunaomba tuambiwe haraka kama Rais Mstaafu huyu Jakaya M Kikwete ana Vinasaba vya Uhutu kutoka nchini huko Burundi.

Kitu nakukubali mkuu ni kutobakia na jina moja la kampuni kwa muda mrefu! Huwa unaweza kubadili badili jina la kampuni ili usipigwe kodi kubwa. Lakini mtu akipata huduma yako anagundua ladha ile ile kwa jina la ile kampuni nyingine.

Hii inasaidia sana hasa kwa mazingira ya demokrasia yetu. Acha sisi tubakie na majina ya kampuni zetu ya muda mrefu hapa jukwaani.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,329
2,000
CHAPISHO zuri lakini muda umekwenda...

Mpwaa naona unatutafuta ubaya wee kwi kwi kwi....
Kwa harakaharaka;

Wahutu Wahutu Wahutu Wahutu

Miaka mingi nyuma huko,baadhi ya WAAFRIKA WEUSI TII waliokuwa WANAISHI CAMEROON ya sasa waliamua kutafuta maeneo mengine yenye rutuba na Hali ya hewa nzuri.
Kama KAWAIDA ya misigano ya Koo na Vita vya kikabila,msukumo huo ULIWAFIKISHA MAENEO YA GABON,wengine walifika afrika ya Kati,wengine wakafika eneo la Kongo ya Brazaville,Ruanda na Urundi ya sasa na wengi wakafikia misitu ya Kongo Kinshasa.

WATU HAWA NDIO WALIOKUJA KUITWA WABANTU...

WABANTU wakasambaa mashariki na kusini mwa ziwa Tanganyika,wakazaliana hapa Tanganyika,Uganda,Kenya,Zambia,Malawi,Msumbiji,Zimbabwe,Lesotho,Eswatini,Namibia mpaka Afrika ya kusini.

Makabila yote ya Tanzania kasoro machache kabisa yakaieneza asili yao ya UBUNTU.....

KIASILI WABANTU NI WAFUGAJI ILA SI KWA UKUBWA SANA.HAWA WANAISHI KWA KUWINDA,KURINA ASALI NA KULIMA.

Ukiwaangalia utauona wajihi wao wa weusi wa RANGI ya kukoza, KAVU ISIYOMETAMETA.Wana vimo vifupi,vifua vipana,mikono yenye nguvu,kule juu shingo zao ni fupi,vichwa vikubwa na mviringo,usoni pua kubwa pana na bapa.Macho yao madogo na ya saizi ya Kati,pia ya rangi nyeusi.Wana nywele nyeusi,kavu na kipilipili.

NITAENDELEA
Aaah, mkuu, imebidi nikuheshimu tu kwa elimu hii hata kama sijui ukweli wake.

Lakini nina swali moja: Ilikuwaje chimbuko lao la asili likawa sehemu moja hiyo ya CAMEROON? Hakuna sehemu nyingine?

Itapendeza kama utatuwekea na 'reference' ya haya ili nasi tukazame huko.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,329
2,000
Rais wa Burundi, Mhe. Evariste Ndayishimiye amemtunuku medali Rais Mstaafu wa Tanzania, Mhe Jakaya Kikwete kwa mchango wake katika harakati za kurejesha amani nchini Burundi.

Chanzo: ForeignTanzania

Sisi akina Mzukulu tunaomba tuambiwe haraka kama Rais Mstaafu huyu Jakaya M Kikwete ana Vinasaba vya Uhutu kutoka nchini huko Burundi.
Hata kumbukumbu ya muda mfupi hivi ni shida kwako?

Mara hii umesahau mapinduzi ya Godfrey (sijui ndilo jina lake?) na chimbuko lake lilitokea wapi?

Hata ile ahadi ya tishio la 'I will hit him' kwako lilishasombwa na maji?

Tunaposemwa kuwa na akili kama za kuku anayetupiwa mtama ili achinjwe tunalalamika; lakini huo ndio ukweli wenyewe.

Nakukumbuka mkuu 'Mzukulu'; sasa sijui kama mada yako hii ni mwendelezo wa yale tuliyojibizana huko nyuma, hiyo sijui!
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,883
2,000
Kitu nakukubali mkuu ni kutobakia na jina moja la kampuni kwa muda mrefu! Huwa unaweza kubadili badili jina la kampuni ili usipigwe kodi kubwa. Lakini mtu akipata huduma yako anagundua ladha ile ile kwa jina la ile kampuni nyingine. Hii inasaidia sana hasa kwa mazingira ya demokrasia yetu. Acha sisi tubakie na majina ya kampuni zetu ya muda mrefu hapa jukwaani.
Ha haha! Hii ndio JF home of great thinkers ilivyo kuwa kabla haijavamiwa na vibaka! Watu wanauwezo wa kuelewa tofauti ya Coca na Pepsi hata zikiwa kwenye glass
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
29,664
2,000
Tanzania na Burundi uhusiano wetu ni mkubwa mno kila nchi huwa na rafiki mkubwa
tanzania sasa hivi tuna makabila mawili mapya ya wahutu na watusi toka burundi baada ya Serikali ya tanzania kuwapa uraia wakimbizi laki mbili toka burundi waliokuwa wakiishi makambi ya wakimbizi.Sasa hivi wako mikoa kibao wakichacharika na maisha
 
kabombe

JF-Expert Member
Feb 11, 2011
26,042
2,000
Sisi akina Mzukulu tunaomba tuambiwe haraka kama Rais Mstaafu huyu Jakaya M Kikwete ana Vinasaba vya Uhutu kutoka nchini huko Burundi.
Ni protokali tu mkuu
Hata kiulinzi,kikwete ni tofauti na Mkapa na Mwinyi
Magufuli akimaliza,shughuli za kikwete zitapungua,zitahamia kwa Magufuli,na hata ulinzi.utapungua kidogo
Kwa ufupi ni kwamba kadiri Rais mpya anavyokuja,wewe mstaafu majukumu.mengi ya kitaifa na kimataifa yanapungua,anapangiwa uliemuachia urais
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
9,450
2,000
Assalaam alaykum wanajf,kumekucha!

Kabla sijaanza kutembeza Biashara yangu ya Al Kasus nikasema nitabaruku kidogo kutokea pale nilipoishia.

Mtoa hoja ni lazima ujue kutofautisha kati ya SERA ZA NCHI ZA MAMBO YA NJE na DIPLOMASIA YETU...these are two different entities.

Kwa nafasi aliyopo mstaafu mh.Jakaya Kikwete kamwe hawezi kuiwakilisha nchi kwenda kusimamia SERA YA MAMBO YA NCHI ZA NJE.
Yeye anapotoka kutuwakilisha basi hutambaa katika uwanda wa DIPLOMASIA YETU....hatoki nje ya hapo.

SWALI
Je anaweza kuiwakilisha nchi pasina ridhaa ya serikali iliyopo madarakani?!!!
JIBU
Nope,haiwezekani.

SWALI
Je safari yake nchini Burundi amepata mwaliko binafsi?!!

JIBU
Inawezekana ukawa binafsi ama ukapitia foreign affairs.
SWALI
Kama haukuwa wa kibinafsi,je alitumwa kumwakilisha mh.Rais?
JIBU
Inawezekana kuwa ni hivyo.

Niseme tu,mh.Jakaya NI mwanasiasa mbobezi na mwanadiplomasia wa haja zaidi ya mh.Membe,amehudumu foreign affairs muda mrefu.Amefundisha siasa Jeshini,NI mzalendo wa kiwango Cha SGR za magufuli.

Hebu mtafuteni mzee Chizii na mumuulize ni kwa nini marehemu mzee Kingunge Ngombale Mwiru alikuwa anarudiarudia kusema kuwa walikuwa ni vijana watatu tu kwa kipindi kile aliowavisha ITIKADI ya chama na Sera za nchi na wakaiva kwa kiwango cha kukata na shoka.
Nakudokezea tu atakutajia;

1.Dr Jakaya Kikwete
2.Edward Ngoyai Lowassa
3.Abdulrahman Kinana

Kwa hiyo vijana wenzangu mkae mkijua kuwa haya MASUALA ya mh.Kikwete kuzodolewa kuwa eti yeye ni mhutu....ni kutokujua tu historia ya makabila hapa afrika kwani makabila yanabadilika majina kutokana na vizazi kuwa vingi na kuhama kutoka eneo moja kwenda jengine Kama nilivyodadavua hapo juu.
Kwani hao waitwao "wahutu" ndio babu wa makabila yote nchini Tanzania kasoro wale wahamiaji na wafugaji wa asili ya BONDE LA UFA.....

Insh'allah nikimaliza kutembeza Al Kasus yangu hapa Tandale kwa mtogole nitakuja kuwaelezea undani wa mashambulizi yanayoelekezwa kwa mh.Jakaya Mara tu alipoutoa ule ushauri wake kuntu juu ya kukaa mezani kwa mahasimu wa kikabila na kiitikadi wa nchini RWANDA ya komandoo Paul Kagame.

Nawasilisha.
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
9,450
2,000
Hata kumbukumbu ya muda mfupi hivi ni shida kwako?

Mara hii umesahau mapinduzi ya Godfrey (sijui ndilo jina lake?) na chimbuko lake lilitokea wapi?

Hata ile ahadi ya tishio la 'I will hit him' kwako lilishasombwa na maji?

Tunaposemwa kuwa na akili kama za kuku anayetupiwa mtama ili achinjwe tunalalamika; lakini huo ndio ukweli wenyewe.

Nakukumbuka mkuu 'Mzukulu'; sasa sijui kama mada yako hii ni mwendelezo wa yale tuliyojibizana huko nyuma, hiyo sijui!
🤣🤣
 
Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
9,450
2,000
Aaah, mkuu, imebidi nikuheshimu tu kwa elimu hii hata kama sijui ukweli wake.

Lakini nina swali moja: Ilikuwaje chimbuko lao la asili likawa sehemu moja hiyo ya CAMEROON? Hakuna sehemu nyingine?

Itapendeza kama utatuwekea na 'reference' ya haya ili nasi tukazame huko.
Ndugu yangu nakushukuru kwa heshima uliyonipa.

Naam,huu ni mjadala wa kihistoria.

Maelfu ya miaka iliyopita,kulitokea makabila yaliyokaa afrika ya kati,hasa Cameroon ya sasa,watu hao waliitwa SAO wakazaliana na kuwa wengi mfano wale waitwao BAKA wanaoishi misitu ya Kongo almaarufu(mbilikimo) ama WATWA.

Tutaendelea kujuzana ni wapi lilikuwa chimbuko la hao SAO.

Rejea yangu ni kutoka vitabu VYA historia ya afrika ya kati na afrika ya magharibi,haraharaka mnaweza mkapata kwa uchache kupitia WIKIPEDIA.
 
kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
3,654
2,000
Mnauzi sana maana hamna kumbukumbu! Nkurunziza alipinduliwa akiwa Tanzania. Kikwete akampatia makomandoo wakapitia Ngara na asubuhi yake alikuwa ikulu Bujumbura na hakutoka hadi kifo chake.
 
Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,402
2,000
Mnauzi sana maana hamna kumbukumbu! Nkurunziza alipinduliwa akiwa Tanzania. Kikwete akampatia makomandoo wakapitia Ngara na asubuhi yake alikuwa ikulu Bujumbura na hakutoka hadi kifo chake

Mnauzi ndiyo Kiswahili cha wapi hiki? Mimi nijuavyo Kiswahili Fasaha ni Mnaudhi. Imarisha Kwanza Kiswahili chako kama hujakurupuka Kuchangia.
 
Dr rujana

Member
Feb 11, 2019
99
250
Rais mtaafu Kikwete ndiye aliyekuwa kiongozi mpatanishi wa mgogoro wa Burundi kipindi kile akiwa waziri wa mambo ya nchi za nje,katika usuluishi ule ndo ulisababisha chama cha CNDD-FDD chini ya marehemu Nkurunziza kichukuwe madaraka Burundi,ni haki ya Burundi kuthamini mchango wa Rais wetu mstaafu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom