Rais Magufuli yashamshinda?

Rais Magufuli yashamshinda?

nadhani kuna amri nyingine ameshazisahau na watu wameanza kuzipotezea! kwa mfano kunywa pombe mchana,kukataza pool table na usafi kila jumamosi watu wamerejea hali ya zamani na hakuna kiiongozi anayefuatilia.Uhalifu umerejea kwa kasi kwani Polisi wamekaririshwa kwamba kazi yao ni kupambana na UKAWA na kusahau majukumu yaoyai kulinda raia na mali zao!
Na ile ya ukaguzi wa silaha mkoa wa dar es salaam
 
Ukatili upi..mnamtaka mtu anayechekea maovu sio.. na combart za Jeshi yeye ni Amir jeshi mkuu anatoa command za kijeshi kisheria kuna kosa gani yeye kuvaa kitenge??
 
Nyani Ngabu ,

..mimi huyu nilishamshtukia tangu zamani.

..nilishaonya hapa JF kwamba Magu haamini ktk demokrasia ya vyama vingi na uhuru wa kutoa mawazo.

..nilishaonya kwamba ana dalili za ukatili. Kwamba akitekeleza sheria anafanya hivyo huku akikomoa.

..tulizungumzia tabia yake ya kutopima madhara ya kauli zake ktk majukwaa.

..tukio la mwisho lilikuwa lile la kuvaa KOMBAT za JWTZ. Binafsi tukio lile confirmed my suspicions kuhusu namna ambavyo atatawala.

..Ni kweli tulihitaji kiongozi who is very ASSERTIVE. lakini tumefanya makosa kutokuchagua wabunge wengi wa upinzani ambao wangeweza kumrudisha ktk mstari pale anapovuka mipaka ya madaraka yake.

NB.

..kuna tatizo ktk process ya kumpata Raisi kuanzia kwenye vyama vyetu vya siasa.

..mchakato ungekuwa wa wazi tungeweza kutambua tabia na mwelekeo wa wagombea Uraisi mapema.

..DEBATES pia zingetusaidia kuchuja wagombea na kupata mtu sahihi.
 
Mie sikutegema kuona Kiongozi mbovu Tanzania kama Kikwete lakini nilikosea sana. Huyu jamaa katika hii miezi tisa ametia fora. Kuna uwezekano akaamua kubadilika na hivyo kupunguza ukurupukaji na mwendokasi na kuanza kuomba ushauri toka kwa washauri wake mbali mbali kabla ya kutoa kauli yoyote ile hadharani. Hili litaleta ahueni kubwa sana nchini na pia kuhakikisha watu (subordinates wake) hawamuogopi kama ilivyo sasa hivi. Kama hakubadilika na kuendelea na style yake hii basi nchi yetu ina safari ndefu sana iliyojaa giza nene.

Hivi ni mimi tu au na wengine mpo mnaoona kama vile mambo yashamshinda huyu Magufuli?

Kuna hali fulani hivi naiona ambapo jamaa ni kama anaamka tu kila asubuhi na kutoa maamuzi ya kukurupuka kurupuka.
Yaani yeye ni amri tu....fanya hivi....fukuza huyu....twende kule...nk.

Yapo baadhi ambayo ni mazuri ambapo mtu unaona kabisa hapa nia ni nzuri lakini mengine yana ukakasi kidogo.
 
Aliyeivuruga CHADEMA ni Mbowe na wala sio Dr Slaa

..that was a big miscalculation by Freeman Mbowe.

..cdm ilikuwa inataka kwenda ikulu kwa njia ya mkato.

..hata Dr.Slaa naye alikuwa na matatizo yake. Mojawapo ni kutoshaurika. He did a lot of good for the party though.

..lingine chama kinatakiwa kiwe na mwanachama zaidi ya mmoja mwenye sifa na anayekubalika kugombea uraisi.

..pia tulijielekeza mno kwenye Uraisi tukasahau ubunge. Hapa uongozi wote unapaswa kubeba lawama.

..pia hoja zetu ni za kuokoteza-okoteza. Kitengo cha UTAFITI na SERA, pamoja na kitengo cha HABARI vinahusika.
 
Opinions. Uncle Ngosha yuko sawa. Ninamuelewa kwa sababu nilishamuelewa kabla hajawa Raisi. Ni ngumu kuielewa management style yake, mimi huwa naiita "JUST DO IT style"
Inawafa huko huko mlikokuwa kwenye kijiwe chenu, sio kwenye kuongoza Taifa........Wananchi wanastahili kujua kesho kutatokea nini...... JK Nyerere"1996"
 
Ukatili upi..mnamtaka mtu anayechekea maovu sio.. na combart za Jeshi yeye ni Amir jeshi mkuu anatoa command za kijeshi kisheria kuna kosa gani yeye kuvaa kitenge??
Hahaha ujue hata wewe uliyeandika hapa wala huna uhakika Na maisha bora.... Nina uhakika mnaishi kwa matumaini hakika miaka kumi itapita kavu
 
Ukisema rais fulani ni bora kuliko rais fulani bila kuainisha unaongelea uwanja gani, tayari ushanioesha kwamba huna umakini.
Naongelea uwanja wote, ambao rais anaruhusiwa kucheza! Magufuli ana mapungufu lakini Kikwete alikuwa ni zaidi. BTW wanaopiga kelele Tanzania sasa hivi kumlaumu Magufuli ni wale watu waliokuwa wanafaidika na mfumo dhaifu wa Kikwete. Watu wa kawaida maisha bado ya yale yale na hakuna kilicho badilika.
 
Mie sikutegema kuona Kiongozi mbovu Tanzania kama Kikwete lakini nilikosea sana. Huyu jamaa katika hii miezi tisa ametia fora. Kuna uwezekano akaamua kubadilika na hivyo kupunguza ukurupukaji na mwendokasi na kuanza kuomba ushauri toka kwa washauri wake mbali mbali kabla ya kutoa kauli yoyote ile hadharani. Hili litaleta ahueni kubwa sana nchini na pia kuhakikisha watu (subordinates wake) hawamuogopi kama ilivyo sasa hivi. Kama hakubadilika na kuendelea na style yake hii basi nchi yetu ina safari ndefu sana iliyojaa giza nene.
Tabia haina dawa alishasema kauli za ajabu ajabu toka enzi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mifano mbona mingi tu bana.

Fuatilia yanayojiri nchini na utaipata tu.
yaliyojili ni kazi nzuri but mapungufu madogo hayakosi...sema followers tulijisahau sasa inatupa shida kwa mfumo huu..kulipa kodi, kufuata sheria, tulizoea maneno matamu hata tunapokosea na maisha ya dili dili tu.
lugha kali tuivumilie, followers tumuunge mkono kwa mazuri yake..malengo ni mazuri tu, tuijenge nchi kwa nafasi tuliopoalie juu hawezi fanya kila kitu.
 
Ni kweli kabisa nchi imeshamshinda ndo maana amekuwa mtu wa kutoa matamko ya kukurupuka kila siku sijui hata yule mshauri wake anafanya kazi gani?
 
..watanzania tulitaka rais wa aina ya magufuli, tulitaka rais ambaye ana maamuzi magumu, mwenye kutoa amri na kusimamia anachokiamini,ndiye huyu sasa tumempata! M ungu alisikiliza sala zetu! wewe na vulijimaswali lako kama ulishatumbuliwa au ndugu zako wa karibu wamekubwa pole sana!..mimi niko na magufuli 100% hapa kazi tu! kaandamane uone cha mtema kuni!
 
Haya tuambia huko Hotlanta Au kokote ulipo mji mzima msafi si ndio?


20160730_165529_001.jpg
20160730_165545.jpg
 
saiv tuu hajapanick...sijui akipanick atakuwa na maamuz gan huyu jamaa.
Na navo jua kupanick nilazma sabab atafika 2020 hakuna alilofanya........nataman sana niwe hai nishuhudie kampeni za 2020.....za kuanzia ndan ya chama na uchaguz kw ujumla
 
Kauli zake hizi Dr Rais Magufuli tumuiteje?
Usiogope wewe
Beleshi iitwe Beleshi wala sio Kijiko kikubwa
"Mikutano ya kisiasa hadi 2020"
Lkn yy anafanya mikutano
DIKTETA UCHWARA huyu
Malafyale gwa kukaja abhana akubhaleka nani? ni nongwa isi. nndeke itolo umundu uju akaja gwa kunjobha.
 
Naongelea uwanja wote, ambao rais anaruhusiwa kucheza! Magufuli ana mapungufu lakini Kikwete alikuwa ni zaidi. BTW wanaopiga kelele Tanzania sasa hivi kumlaumu Magufuli ni wale watu waliokuwa wanafaidika na mfumo dhaifu wa Kikwete. Watu wa kawaida maisha bado ya yale yale na hakuna kilicho badilika.
Obviously Heisenberg's Uncertainty Pronciple hujaifahamu ama hujaelewa inaenda mpaka kwenye kulinganisha marais.

Ni hivi, jinsi inavyozidi kuwa general ndivyo unavyozidi kuwa inaccurate. Ndiyo unavyozidisha margin of error.

Ili kuwa accurate zaidi inabidi uwe soecific zaidi.

Kwa mfano, Kikwete kampita sana Magufuli kwenye kuheshimu demokrasia na uhuru wa habari.

Magufuli anaweza kuwa kampita Kikwete kwenye kurudisha nidhamu katika utumishi wa umma na kukusanya kodi.

Watu wasio na uhuru wa demokrasia hata kuwa na nidhamu yabkweli ni shida. Hivyo Magufuli anaweza juwa anaendesha nchi kwa kutia watu woga zaidi.

Hapo utapimaje nani zaidi ya mwenzake bika kutaja specifics?
 
Kwani Cuba wana vyama vingapi na wana maisha gani? Hata Tanzania tutarudi kwenye chama kimoja na tutakuwa na maisha mazuri sana kama Cuba hakuna shaka. Demokrasia haiji kwa kulazimisha inabidi watu wawe tayari ama sivyo ufalme uendelee. Usiwe na shaka.
kwa akili yako unaona Cuba wana maisha mazuri duh.
 
Back
Top Bottom