Watanzania kwa kuchagua hovyo tumevunja rekodi. Kila uchaguzi tunachagua hovyo zaidi na hatujifunzi. Mtu hata mkewe alikuwa anasita kuungana naye kwenye kampeni hatugutuki! Tumelikoroga na sasa yabidi tulinywe...watakaobakia hadi 2020 labda watakuwa wamepata aikili za kuchagua kwa umakini zaidi.
Swahiba...
Kitu ambacho sikielewi kabisa ni hiki: tokea tupate uhuru hatujawahi kuongozwa na chama kingine chochote kile zaidi ya CCM [tukizingatia na ubadilishwaji wa jina].
Kwa msingi huo, CCM ndo inawajibika moja kwa moja na hali tuliyonayo leo - dhiki iliyokithiri, huduma za jamii mbovu zilizo chini ya viwango, ufisadi, rushwa, maradhi, na mengineyo.
Cha ajabu, chaguzi baada ya chaguzi watu huishia kuwapa kura walewale ambao ndo wameileta hali tuliyonayo licha ya kutuaminisha kwamba eti sisi ni nchi tajiri sana. Tunaenda kufikia miaka 60 ya kutawaliwa na chama kilekile. Aibu.
Sasa, mtu unaweza kujenga hoja ya kwamba CCM huwa hawashindi kihalali kwa sababu mazingira ambayo chaguzi hufanyika si ya huru, haki, na uwazi.
Sawa, hiyo ni hoja nzuri na yenye mashiko. Lakini mimi binafsi bado naamini kabisa kuwa kwamba watu kwa umoja wetu tukiamua kabisa kutokuipigia kura CCM tunaweza, hata kama CCM itaamua kuchakachua matokeo au kuleta mizengwe [kama ilivyofanyika Zanzibar].
Na ikitokea tukafanya hivyo na CCM kuchakachua na kuendelea kung'ang'ania madarakani walau tutakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuishinikiza mpaka itoke. Ila kwa sasa inakuwa vigumu kwa sababu hata bunge limejaa hao hao CCM na hivyo kuifanya hoja ya chaguzi kutokuwa huru na haki kukosa nguvu kidogo.
Yaani kwa kweli ingekuwa ni juu yangu mimi basi ningependa sana kujaribu na watu wengine [zaidi ya CCM] ili tuone na wao wana nini la kutupa Watanzania.