Odhiambo cairo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 16,352
- 22,958
Anawauudhi eh, pole yule ni commender huwezi kumtenganisha na mafanikio ya CDMKama vile tuabuduvyo mzee wa Hai!
Sent from my SM-J110F using JamiiForums mobile app
Anawauudhi eh, pole yule ni commender huwezi kumtenganisha na mafanikio ya CDMKama vile tuabuduvyo mzee wa Hai!
Sema wewe Diva wangu.Baba j hapendi mawazo kinzani yeye anajiona correct, ana create situation ambayo ikija kubuma itakua hatari. Na anaweza sema kweli ifungwe mana hulka ya wasiotaka kukosolewa huwa kuwanyamazisha opponents wao.
Ndio kinachofuata, Mama mchungaji wa st. Marys alipambana na hii kitu akashindwaNa akionaa mnamsema sana jf ,anaipiga marufukuuu
Ni kweli jingalao,hapo nakubaliana nawewe mkuuMbona sijawahi tukana humu?
Mleta mada kaja na kichwa cha habari chenye mfano wa maneno ya Kanga...hajaweka ni matamko gani ya kukurupuka ...
By the way kushindwa kwa Magufuli kutaelezewa na kushindwa kutekeleza ilani aliyoiahidi...so far ameshagusia maeneo mengi ya Ilani haswa haswa kwenye Elimu bure,Mahakama ya mafisadi,Ushuru usio na tija,na utumbuaji wa watendaji wabuvu.
Ukimpinga Magufuli fanya hivyo kwa data na rejea ilani ya Ccm.
Kwa kiasi gani wafanya biashara wana hiyo "multiplier effect"?
Taratibu watatuelewa
Na watu wengi hawajamsoma hulka yake tu anko ni zaidi ya tumjuavyo ukitaka ukosane naye mwambie ukweli. Kazi tunayo Watanzania maana wengi watapotezwa.Sema wewe Diva wangu.
Maana wengine tushasema sana mpaka salio tumemaliza. Tukisema hata kwa kukopa tunaweza kuonekana "huyo Kiranga kawaida yake tu".
Mwenyewe kasema tutalimia meno. Watu wakafikiri anatania.Na watu wengi hawajamsoma hulka yake tu anko ni zaidi ya tumjuavyo ukitaka ukosane naye mwambie ukweli. Kazi tunayo Watanzania maana wengi watapotezwa.
Nyani Ngabu, mwaka 2005 niligombana si na marafiki tu bali hata ndugu nikipinga Kikwete kugombea Urais kwamba hana sifa wala uwezo wa kuongoza, nikaambiwa niache kumkashifu chaguo la mungu, tumaini lililokuwa likisubiriwa!Swahiba...
Kitu ambacho sikielewi kabisa ni hiki: tokea tupate uhuru hatujawahi kuongozwa na chama kingine chochote kile zaidi ya CCM [tukizingatia na ubadilishwaji wa jina].
Kwa msingi huo, CCM ndo inawajibika moja kwa moja na hali tuliyonayo leo - dhiki iliyokithiri, huduma za jamii mbovu zilizo chini ya viwango, ufisadi, rushwa, maradhi, na mengineyo.
Cha ajabu, chaguzi baada ya chaguzi watu huishia kuwapa kura walewale ambao ndo wameileta hali tuliyonayo licha ya kutuaminisha kwamba eti sisi ni nchi tajiri sana. Tunaenda kufikia miaka 60 ya kutawaliwa na chama kilekile. Aibu.
Sasa, mtu unaweza kujenga hoja ya kwamba CCM huwa hawashindi kihalali kwa sababu mazingira ambayo chaguzi hufanyika si ya huru, haki, na uwazi.
Sawa, hiyo ni hoja nzuri na yenye mashiko. Lakini mimi binafsi bado naamini kabisa kuwa kwamba watu kwa umoja wetu tukiamua kabisa kutokuipigia kura CCM tunaweza, hata kama CCM itaamua kuchakachua matokeo au kuleta mizengwe [kama ilivyofanyika Zanzibar].
Na ikitokea tukafanya hivyo na CCM kuchakachua na kuendelea kung'ang'ania madarakani walau tutakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuishinikiza mpaka itoke. Ila kwa sasa inakuwa vigumu kwa sababu hata bunge limejaa hao hao CCM na hivyo kuifanya hoja ya chaguzi kutokuwa huru na haki kukosa nguvu kidogo.
Yaani kwa kweli ingekuwa ni juu yangu mimi basi ningependa sana kujaribu na watu wengine [zaidi ya CCM] ili tuone na wao wana nini la kutupa Watanzania.
Mwenyewe kasema tutalimia meno. Watu wakafikiri anatania.
Ndugu yangu wee acha tu! cart in front of the hose (track number ya Rosetta ninayo by the way).Hahahaaa mzee wa 'mfumo'...
Vumilieni tu.
Mlizoea vya kunyonga vya kuchinja hamviwezi.
Magufuli kabana njia zote hakuna sehemu ya kuiba,dili hakuna,hakuna kusafiri hovyo hovyo.
Vumilieni ingawa mnaumia ipo siku mtazoea kuishi bila kutegemea fedha za semina,warsha,makongamano,safari nk.
No sense ' in jpm voice'Nyani Ngabu, mwaka 2005 niligombana si na marafiki tu bali hata ndugu nikipinga Kikwete kugombea Urais kwamba hana sifa wala uwezo wa kuongoza, nikaambiwa niache kumkashifu chaguo la mungu, tumaini lililokuwa likisubiriwa!
Miaka kumi baadaye, 2015, nikagombana tena na marafiki wale wale, ndugu wale wale nikionya yale yale kuwa Magufuli hana sifa, busara wala hekima ya kuongoza labda kuliko hata Kikwete, nikarushiwa maneno yale yale kama ya mwaka 2005!
Ajabu ni kwamba wale wale ambao mwanzoni walishinda mtandaoni wakimsifia Kikwete hivi sasa hawamsifii tena badala yake wanamsifia Magufuli kama mkombozi na kukosa kabisa uvumilivu kwetu tunaomkosoa kwa ukurupukaji wa hovyo.
Kikwete aliingia madarakani na kifurushi cha kashfa, lakini huyu mwenzetu kaingia madarakani na gunia zima la kashfa lakini washikaji wake hili hawalioni, badala yake wanawalaumu ambao hawajawahi hata kukamata madaraka ya nchi hii!
Naam, ndio Tanzania yetu hii, nchi inayodaiwa kuwa ya amani na utulivu huku polisi na vyombo vyote vya usalama vikiwa mkononi mwa dikteta uchwara ambaye hajawahi kuheshimu mipaka yake ya uongozi kikatiba, kisheria wala kikanuni!
Lakini baya kuliko yote ni kwamba wapo raia wa nchi hii, walio tayari kumsifia kwa vifijo na nderemo mfalme wao hata kama anatembea uchi, wakitumia ushawishi wa nguvu kujaribu kutuaminisha jinsi alivyovaa! Cry my beloved country!
Tatizo kubwa sana ninaloliona ni kwamba Rais wetu hana mpangilio katika kufanya kazi zake. kwa mfano, aliamua kushughulikia tatizo la vitanda katika Hospitali. Ni kweli vitanda ni tatizo kubwa na linahitaji ufumbuzi. lakini je, katika muktadha wa afya na matibabu, ukosefu wa vitanda ndio tatizo namba moja? uwepo wa vitanda utapunguza vifo katika hospitali zetu kwa kiwango kikubwa? maana kuna matatizo ya vifaa tiba, kuna matatizo ya madaktari na wauguzi, na juu ya yote kuna matatizo ya mfumo. mfano kama hospitali za chini zinaimarishwa, maana yake mrundikano utapungua Muhimbili.
Katika Elimu, pamoja na matatizo lukuki yaliyopo katika sekta hii: ubovu wa mitaala, matatizo ya walimu, nyumba za walimu, madarasa, maabara, madawati, na mengine mengi, yeye akakomaa na madawati. ni kweli ni moja ya matatizo, lakini je, linaweza kuleta mabadiliko makubwa, impact kubwa katika elimu kama likitatuliwa kwanza hilo?
Kukosa mpangilio kunakuja pia katika maamuzi. ana utaratibu wa kutoa maamuzi ya ghafla. bila mpango, bila bajeti. mfano mzuri ni hii amri ya Serikali kuhamia Dodoma. haijulikani kama kuna tathmini imefanyika kuona impact ya kuhamia ghafla namna hii.
Mwendo wa namna hii matokeo huwa baadaye ni kujikuta umesababisha matatizo mengi kuliko unavyoweza kuyakabili. JK alikuwa na kawaida ya kupaa kwenda majuu mambo yanapomzidia. Magu yeye atakuwa na kautaratibu gani ili angalau apumue? kutumbua majipu zaidi?
Mbona hajaitumbua IPTL kama kweli haogopi kufanya maamuzi, mbona hajaenda kukaba kwenye madini..huko...tusiwe wajinga..hata yeye mwenyewe alisema kwa hali ilivyosasa ni bora kufanya maamuzi kama kunamakosa basi yatarehekebishwa kuliko kutofanya maamuzi yeyote kwa kuogopa