Rais Magufuli: Wasiotutakia mema wanatumia Asasi za Kiraia na NGO kutuhujumu ili kufifisha jitihada zetu kujikomboa kiuchumi kwa maslahi yao binafsi

Mlianza kwa kuzinanga serikali zilizopita hasa ya awamu ya nne. Mnapoulizwa kitu gani "so special" mlichofanya ambacho huko nyuma hakikufanywa, mnatoa povu. Tuwakumbushe tu, tangia mwanzoni mwa 1900, nchi hii ilianza kuwa na reli, mlipokuja mjini mlipita katika mabarabara ya lami toka huko mlikokuwa.

Kila kijiji mlikuta kina shule ya msingi, kila kata mlikuta kuna shule ya sekondari. Madaraja yote makubwa yalishajengwa. Yote hayo yalifanyika kwa combination ya resources za ndani na nje kwa njia ya ushirikiano. Self-seclusion itatufikisha wapi katika Dunia ya leo jamani.

Now mnageukia "mabeberu". Jamani "mabeberu" si washindani wetu kwenye maendeleo wala si size yetu. Tunawaita mabeberu ila wao wakituita manyani tunapayuka Dunia nzima. Maana maneno huuma nayo. Let's promote harmony, peace and unity.
 
Ni demokrasia gani magufuli na ccm wanaitaka? Kama hata ndege unanu ua kwa mzungu weweu azalisha nini?

Na aliyewauzia hizo mali ni nani kama sio ccm?

Baba yako akipungukiwa akili si lazima na wewe ukose akili, waliokosea ccm sio hao wanaoiongoza ccm siku zote, na ndio maana wanabadili wenyeviti kila mara. Kwahiyo wazo lako sio ishu.
 
Matatizo ya nchi yetu ni Wazungu?Kwakuwa kila kukicha Mara mabeberu, utadhani tungepata Uhuru Jana! Bila misaada ya Mabeberu tungekuwa zero. Iko Siku tutawatafuta.
CCM bwana wao ndio waliosaini hiyo mikataba kwa kujali.matumbo yao, leo kibao wanageuzia wazungu, wanadhanu wazungu ni mazuzu kama wao?
 
Nyie chezeeni mabeberu tu lakini mjue hayana shida na sisi ndio maana bado tuko mtaani tunadunda.

Mabeberu yalimfanya Sadam na ubabe wake akakamatwa amejificha kwenye shimo kama panya na yakamnyonga live mbele ya TV,yalimfanya Ghadafi aokotwe huko mtaroni,yameifanya Zimbabwe kichane kimoja cha ndizi mbivu kuuzwa Zimb. Dollar million 500

Endeleeni kuyataja taja ,yanaweza kusikia wito wetu.
 
Hizi quotes huwezi kuona umuhimu wake sasa lakini iko siku watu watamuenzi huyu muheshimiwa kwa hekima zake,hakuna kugeuka nyuma,piga kazi Baba Magufuli tuko nyuma yako...

Sent using Jamii Forums mobile app

Lengo hasa la hotuba za kutaja mabeberu ni kama kujaribu kuficha mwenendo mbaya wa demokrasia hapa nchini. Anafahamu fika wazungu ndio wanaohoji uminywaji wa demokrasia hapa nchini, hivyo anawataja kwa ubaya ili kupumbaza wananchi hata hapo wazungu wakihoji huu udictator, aseme wanahoji kwakuwa kawazuia kuchukua rasilimali zetu.

Hatudanganyiki, hakuna mzungu anayekuja kuchukua rasilimali zetu bila kufuata sheria za nchi yetu, wazungu wote wanaochukua raslimali zetu wameingia mikataba na viongozi wetu. Tena viongozi wetu ikiwemo yeye mikataba hiyo huifanya kuwa ya siri. Kama kweli analinda raslimali zetu aweke mikataba wazi tuone inasemaje.
 
zebedayo musibha,
Si Rahisi kwa Kizazi hiki danganywa kikaelewa Uzalendo unaofanywa na awamu hii. Ni muda mrefu sasa watu wamedanganywa na hata ma puppet ya Nje wakidhani wanafundishwa Democracy kumbe wanafanyiwa manipulation ili wazidi kidhoofisha Jamii yetu.
Raising Magufuli ni Mzalendo wa kweli tena anayepambana na maadui wa Uchumi wa Nchi yetu
 
Kwa nini kila azungumzapo yeye ni kulialia tunahujumiwa, hatupendwi, mabeberu wanatuonea nk nk?
Hivi tuna nini sisi hapa duniani kilicho cha kipekee hadi tushambuliwe kiasi hicho?
Tumeharibu biashara wenyewe, tumeua kilimo cha biashara chenye kuweza kubadili maisha ya watu wetu wenyewe na tumevunja mahusiano ya kijamii na kikanda kwa ubaguzi tulio anzisha wenyewe halafu tunatupia lawama za kilaghai kwa wengine?
CCM mtaacha lini usanii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatudanganyiki, hakuna mzungu anayekuja kuchukua rasilimali zetu bila kufuata sheria za nchi yetu, wazungu wote wanaochukua raslimali zetu wameingia mikataba na viongozi wetu
Mkuu dunia ya leo hawawezi kuwadanganya wananchi ambao wana data zote mikononi mwao

Ninachokiona hapa ni himaya yao inazidi kumomonyoka na wao wanaliona hilo wanaona kabisa ulaji unawaponyoka wanaweweseka nakulaumu kila kitu na kila mtu

Mfano nzuri ni kesi ya mkulima na ndege walimnyang'anya mali zake akaenda mahakamani akashinda kwa hiyo huyo hakimu alikuwa ni Beberu au Mzalendo anayelinda sheria na katiba ya nchi yake?
 
YUPO KIONGOZI FULANI ALIJIAMINI SANA AKAANZA KUTOA MANENO YA SHOMBO DHIDI YA MABEBERU AKAJIKUTA KWENYE SEPTIC TANK LA KINYESI CHA BINADAMU, HIVYO WALE MNAO KAA NAYE KARIBU MWAMBIENI MKULU YAPO MAMBO MENGI SANA YA KUZUNGUMZA LAKINI SIYO KUTOA MANENO YA KEJELI KAMA HAYO KUNA SIKU YATAMGHARIMU
 
Back
Top Bottom