Rais Magufuli: Wasiotutakia mema wanatumia Asasi za Kiraia na NGO kutuhujumu ili kufifisha jitihada zetu kujikomboa kiuchumi kwa maslahi yao binafsi

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
579
1,000
Kuna hujuma dhidi ya jitihada za Serikali zinazofanywa na baadhi ya wasioitakia mema Tanzania zikilenga kufifisha jitihada zetu za kujikomboa, kiuchumi kwa maslahi yao binafsi, kamwe hawataki kuona tunadhibiti rasilimali walizokuwa wakivuna na kusafirisha bila kuulizwa.

Wanaotuhujumu hawatakubali tutekeleze miradi ya kimapinduzi itakayoharakisha maendeleo, ikiwemo Bwawa la Nyerere, SGR au Kufufua Shirika la ATCL, wasingependa tutoe elimu bure n.k, wangependa tuendelee kuwategemea wao, ilihali wao wanaishi kwa kutegemea rasilimali zetu.

Wanatumia kila njia kufifisha jitihada zetu na kupenyeza ajenda zao,muda mwingine wanatumia Asasi za Kiraia na Mashirika yasiyo ya Kiserikali na kujifanya wanatufundisha Demokrasia na Haki za Binadamu, ilihali wenyewe wanavunja misingi hiyo kwa kujenga mifumo ya kinyonyaji.

Wanajifanya wanatufundisha Demokrasia ilihali wenyewe wanachochea machafuko na kuingilia uhuru wa Mataifa mengine, wanajenga hadi mazingira ya taharuki na kusema EBOLA imeingia Tanzania ili ionekane Nchi haiko salama, tusiposimama imara na kujenga uzalendo hatuwezi kushinda.

======

‘Foreigners’ sabotage our efforts: Magufuli

Dar es Salaam. President John Magufuli said his quest to transform the country’s economy has been encountering obstacles, including sabotage from some ‘foreign’ agents and organizations who do so through locals.

In his live televised address to members of the ruling CCM’s Central Committee, President Magufuli accused some civil society organizations (CSOs) and non-governmental organisations (NGOs) of being used by ‘foreigners’ to push the latter’s agenda.

The Head of State explained that his administration has been implementing reforms in order to make Tanzania financially independent - something which does not seem to bode well for some foreign countries and organisations.

In that regard, President Magufuli said some ‘foreigners’ have been using CSOs and NGOs to sabotage his efforts.

The President said that the government has embarked upon implementation of strategic development projects such as the revival of Air Tanzania Corporation Ltd (ATCL), construction of the standard gauge railway (SGR) and the Nyerere Hydro-electric project on the Rufiji River at a place that was popular as ‘Stiegler’s Gorge.’

However, Dr Magufuli said some locals and foreigners have been using nefarious tactics to frustrate his efforts.
Advertisement

“They use NGOs and CSOs to push their agendas, pretending that they are teaching us democracy and human rights while, in actual fact, they are the ones who are breaking them by creating oppressive systems,” said the President, who also doubles as the CCM chairman.

He added that, “through their operations, they interfere with other countries’ sovereignty, creating chaos as well as unnecessary alarms... For example, they claimed that there was an Ebola outbreak to portray that the country wasn’t safe.”

The President called for Tanzanians to remain united because every journey to transform any country’s fortunes must encounter challenges. He said that, to win ‘the economic war’ (transforming the economy) Tanzanians should be patriotic.

The Head of State also took a dig at some Tanzanians who weren’t ready to accept the on-going changes.

“There are some people who don’t understand that we are in a new era where the main priority is to build the economy; to make Tanzania financially independent; to create integrity and discipline in resource management,” Dr Magufuli lamented.

The Head of State’s remarks come just a few days after reports emerged that the Tanzanian government has written to withdraw the right of individuals and NGOs to directly file cases against it at the Arusha-based African Court of Human and People’s Rights (AfCHPR).

Tanzania has the highest number of cases filed by individuals and NGOs as well as judgments issued against it by the African Court. Out of the 70 decisions issued by the court by September 2019, a total of 28 decisions, or 40 percent, were on Tanzania.

Constitution and Legal Affairs Minister Augustine Mahiga said earlier this month that reports that Tanzania had withdrawn its AfCHPR membership were untrue, noting that the country was only asking for a review of a protocol it believes was contentious.

“The decision to withdraw our membership will only come after they fail to change the protocol that is contentious in the court’s operations,” Dr Mahiga said.

However, he didn’t site the protocol, which he thinks it is contentious.


thecitizen.co.tz


428547C1-711D-4A1C-980A-74CAB3209466.jpeg
 
For the English Audience
Magufuli: CSOs and NGOs are used to undermine our development efforts

"There has been accusations against the government's efforts aiming to undermine our efforts, never wanting to see us control the resources they were exploiting without question.

Our exploiters won’t allow us to pursue revolutionary projects that will trigger development. They would like us to depend on them, while they rely on our resources.

They pretend to teach us democracy, at the same time they are inciting anarchy and invading the freedom of other nations.

If we do not stand firm and advocate for patriotism, we will not win."

While others have applauded President Magufuli’s leadership, others have questioned how patriotism has been defined in this particular context.

emalau

JF-Expert Member
Apr 25, 2009
2,743
2,000
On the contrary kauli za namna hii si za kizalendo bali ni kibaguzi na kugawa watu, ionekane kuna kundi fulani ndiyo linaipenda nchi na lingine linahujumu nchi. Hii si kweli, when i read between lines anataka kuwafanyia ubaya kundi fulani la watu kwa kisingizio cha uzalendo.

Hakuna mtanzania asiyeipenda nchi yake, wanaokosoa wanakosoa ili taifa lisonge mbele na hii ni kawaida kwa mtu yeyote aliyepitia development studies misuguano ni jambo la kawaida. Na kwa waliosoma physics they know that there is no movement without friction. We unataka kuongoza nchi ambayo watu wametulia kama maji ya mtungi we ni nani? hakuna nchi ya hivyo, ajifunze kupanua kifua cha kupokea anayoyataka na asiyoyataka. That is what leadership entails.
 

Kasimba G

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
3,435
2,000
Nahisi "uzalendo" huo umechochewa na kauli ya NGOs Jana kutaka uchaguzi shirikishi, huru na Wenye kuzingatia haki ukiwa ni pamoja na kuwa na tume huru nk!!

Uzalendo huo sio uzalendo. Uzarendo hautaki uchaguzi wa haki na wala hautaki kusikia habari za tume huru Bali uzalendo unahitaji hivyo!
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
39,902
2,000
Hizo sio kauli za kizalendo, bali ni kauli za kuhadaa umma ili kujipa uhalali wa kukandamiza haki za watu wenye mtazamo tofauti na yeye. Kauli za hivyo hutolewa na madictator wengi ili wale wote wanaohoji udhalimu wa makundi mengine ionekane wao wanatumika na nchi za nje.

Ni hivi huyo jamaa sio rais mzuri, bali ni rais wetu, na hana uzalendo wowote bali ni mwenye uchu wa madaraka, hivyo anajiwekea mazingira ya kukaa muda mrefu madarakani kwa kisingizio cha uzalendo.
 

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,447
2,000
Uzalendo gani katika maneno hayo zaidi ya kubagua ili ionekane baadhi ya watu, hususani wapinzani wa kweli hapa nchini hawaipendi nchi yao na wanatumika na mabeberu kutaka kile anachoita Magu kuwa wanadhoofisha maendeleo yetu

Jaribu ku-imagine hivi mwananchi atawezaje kudhoofisha maendeleo ya nchi hii wakati pesa yote ya hazina ya nchi "inathibitiwa" na yeye mwenyewe Jiwe?
 
Oct 26, 2019
85
125
Ikumbukwe harakati za wapigania uhuru wa Africa wakina kwame, lumumba, samora, kaunda, Mugabe na wengineo walipo jaribu kuinganisha Africa na kuifanya kuwa moja ma imperialist waliujumu juhudi zao wengi kuchochewa na kuuwawa wengine kuwekewa vikwazo.

Bado Africa ni kivuli cha masilai ya hao mabeberu ndio maana leo wanajichomeka ktk koti la demokrasia na haki za binadamu

Embu tujiulize nilini mabeberu wamekaa wakafuta ule mkataba wa kuligawa bara la Africa ulio fanyika kule Berlin? Mbona haikuwepo maliziano ya pamoja ya kuiacha Africa iwe uhuru kama ilivyo kuwa kuitawala

Wito wangu pale tunapo hona kiongozi anaonyesha uzalendo anachukia black imperialist monitoring to Africa tumsapoti tuache siasa.

Tusijifanye tunajua siasa kwenye democracy kuna siri kubwa imejificha ni kama simba yule aungulumae anae tafuta mtu ammeze.

Tazama leo Libya, Sudan na congo wanavyo haha
Tuweke masilai ya taifa mbele bado hatujajikomboa nguvu ya pamoja kama taifa ndio suluhu ya ukombozi wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Halaiser

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
2,722
2,000
Kwanini kila wakati yeye huwachukia wanaotoa mawazo mbadala? Kwanini anaamini mawazo yake binafsi kuliko ya wengine? Kwanini maendeleo kwake ni kuwadharau wengine na hata kufikia hatua ya kuwatenga pale tu wanapoonyesha penye udhaifu ktk uongozi wake?? Kwanini anaona nchi haikupata na haitopata maendeleo bila yeye??

Kwa upande mwigine bila Wazalendo wa kweli kusimama imara ktk maamuzi ya kitaifa na kimataifa huyu Mzee kuna sehemu atatufikisha kila mtu atalia. Sifa za mchezaji uwanjani huonekana kwa watazamaji wa mechi na sio yeye kuanza kuwatuhumu wengine huku akijisifia mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom