Rais Magufuli unawatesa walinzi wako

Rais Magufuli unawatesa walinzi wako

Walinzi ndio washauri wake wa hayo mambo wanaoshauri hivyo kuwa asafirije.Fani za watu hizo achana nazo.

Usafiri hata wa anga kabla ya kusafiri wanausalama lazima wakwambie tumia.Hata angani si salama hujasikia maraisi ndege zao kutunguliwa.

Walinzi wanajua cha kufanya waachie kazi yao.Si watu wa kuchoka hovyo.Walinzi wa RAISI UNAFIKIRI ni sawa na walinzi wa CHADEMA wale wanaovaa miwani ya kuchomea magrill?

CHEKI WALINZI WA CHADEMA NA MIWANI YAO YA KUCHOMEA VYUMA
Mbeya3.jpg

Rais ni wa Watanzania sio CCM, uchama wako hautasaidia pale Rais atakapouwawa... Pili ni hatari inaweza zua vita dhidi ya nchi ambayo Rais anatakuwa ameuwawa.
Ndege ni ngumu sana kutungua, tofauti na usafiri wa barabara. Wanaweza kutega mines, etc... Hali ya ki usalama sio nzur ukanda huo.
 
Watanzania, bwana...kazi kwelikweli, yaani wanajua kila kitu...Hivi wewe unadhani RAIS anakurupuka tu kusafiri?! Itabidi utafutwe ili utoe ufafanuzi zaidi uwasaidie PSU kuhusu masuala ya ulinzi.

Hawezi kukurupuka ,kwanza anasahau yeye ni raisi.ulinzi ote tulionao unamlinda yeye...
 
Magufuli anawatesa kila mtu kwa moja kwa moja au indirect..... mambo mtaani magumu .... biashara haziend... mzigo hautoki kama zamani dukani... ni miez sita tu kashika hatamu na mambo yashaanza kuzingua.
wadhamini wetu washaanza kusepa, bandarini shughuli za kibiashara zinashuka kwa asilimia kubwa tu....

niko nje ya mada lakini Rais wangu inabidi aangalie vizuri kuhusu kupunguza government expenditure kuna athali gani kwa sekta binafsi

Vuta subira,umeme umeshuka,mafuta yameshuka,pole pole ndo mwendo
 
Ndege ni ngumu sana kutungua, tofauti na usafiri wa barabara. Wanaweza kutega mines, etc... Hali ya ki usalama sio nzur ukanda huo.

Kwa hiyo mlitaka raisi asafiri kwa ndege kutoka chato hadi rusumo!!! Vichwa vyenu vibovu.Chato na Rusumo hakuna uwanja wa ndege!!! CHADEMA kila kitu kubeza.LOWASA kushindwa kumewapa ukichaaa
 
Oh! Nilichogundua hapa, tatizo ni chuki dhidi ya Kagame na sio Magufuli kutumia batabara.
Read between the lines, Hatuongelei CHUKI HAPA , BALI TUNAIPINGA "PRIDE" NA TUNATAKA PEACE, PROSPERITY NA SECURITY KWENYE NCHI YETU.

Kumbuka, Rais anaouwezo mkubwa wa kutusimamisha au kutuangusha; Hivyo basi ni jukumu letu sote kukosoa pale tunapoona anafanya UKANJANJA!
 
Sioni sababu ya kumlaumu mleta mada. Yawezekana siyo hoja muhimu lakini dhamira yake ni nzuri. Anataka Rais wetu awe salama wakati wote. Tunataka Rais afike kila mahali ikiwezekana lakini usalama wake ni jambo muhimu la kwanza.

Kwa hali ya nchi ilipo, na vuguvugu jipya la uwajibikaji na uadilifu alilolileta Rais Magufuli, tunapenda Rais huyu awe salama wakati wote ili yale aliyoyapanga kwa Taifa hili aweze kuyatimiza.

Tuna wataalam wa masuala ya ulinzi lakini siyo kosa kupokea ushauri kutoka kwa wasio wataalam. Hata asiye Daktari, kuna wakati maelezo yake humfanya daktari afanye kazi yake vizuri zaidi. Kumbukeni tulikuwa na Waziri Mkuu Sokoine, siku ya kifo chake, nasikia Mwalimu alimshauri asafiri kwa ndege toka Dodoma kwenda Dar, ushauri haukupewa uzito wowote. Pamoja na utaalam wote wa walinzi wetu, kilichotokea wote tunajua. Rais Samora wa Msumbiji wakati anatoka kwenye mkutano, nasikia kuwa alishauriwa kuwa ndege yake isipite kwenye anga la South Afrika, wana-usalama wake wakapuuza, kilichotokea sote tunajua.

Tunawashauri wana-usalama wa Rais wetu kuwa ni aheri kuchukua tahadhari zinazozidi kiasi kuliko kuchukua tahadhari pungufu. Tunamwombea Rais Magufuli, pamoja na ulinzi wa kibinadamu, Mungu amjalie ulinzi wa ziada, na daima awape hekima wale wote wanaosimamia usalama wake ili wapate kuyaona yote yahusuyo usalama wa Rais kabla ya kutokea.
 
usalama wako vizuri,....nawaamini vijana wetu
tena nyanja ya kagame najua vijana wanajua wanaenda uwanja wa vita........
no 1 wakumtrust kule
 
Oh! Nilichogundua hapa, tatizo ni chuki dhidi ya Kagame na sio Magufuli kutumia batabara.

Kama huwezi kujenga urafiki na jirani yako, huko kwingine hakuna maana.

Jirani yako anaweza either kuhifadhi maadui wako/kukufanyia uhaya ua pia anaweza kuwa msaada kwako kwa kiasi kikubwa.

Nimeshakujua, mapovu yote hayo ni ya nini?!
Ndugu, ujuaji hausadii bali unabomoa; pendelea kuwa Muelewa. Uelewa unajenga.

ACHA UJUAJI. Kujua kitu sio kukielewa. Kukielewa kitu ni kukijua zaidi.

Pia acha kusoma post kwa kutumia miwani. Hiyo miwani ndio inakutia uchizi na kukufanya uwe mjuaji kupitiliza bila hata ya kuelewa nini kinaongelewa.

#Acha kuingilia fani za kina Blaza K
 
usalama wako vizuri,....nawaamini vijana wetu
tena nyanja ya kagame najua vijana wanajua wanaenda uwanja wa vita........
no 1 wakumtrust kule
Asilimia zaidi ya 95 ya watu wa Usalama Tanzania wanaishi chini ya Hisia zao. Wengi sana wana amini katika Elimu ya vitu vinavyoonekana, ; hawana Elimu ya vitu visivyoonekana; Wengi hawana Visions ( Sense Knowledge Truth + Revelation Truth) . Wengi sana ni wajuaji, walevi, Malaya, wabishi, wala Rushwa,

Hayo ndiyo yanaendelea kuwafanya akili zao kuwa tegemezi; I mean , kila kitu kutegemea kufundishwa na Adui au kuiga kutoka kwa watu wengine. Sio wabunifu !!!
 
Kwani akitumia ndege hawezi shambuliwa....?
Mbona Rais wa Rwanda na Burundi walitunguliwa....??
 
Sioni sababu ya kumlaumu mleta mada. Yawezekana siyo hoja muhimu lakini dhamira yake ni nzuri. Anataka Rais wetu awe salama wakati wote. Tunataka Rais afike kila mahali ikiwezekana lakini usalama wake ni jambo muhimu la kwanza.

Kwa hali ya nchi ilipo, na vuguvugu jipya la uwajibikaji na uadilifu alilolileta Rais Magufuli, tunapenda Rais huyu awe salama wakati wote ili yale aliyoyapanga kwa Taifa hili aweze kuyatimiza.

Tuna wataalam wa masuala ya ulinzi lakini siyo kosa kupokea ushauri kutoka kwa wasio wataalam. Hata asiye Daktari, kuna wakati maelezo yake humfanya daktari afanye kazi yake vizuri zaidi. Kumbukeni tulikuwa na Waziri Mkuu Sokoine, siku ya kifo chake, nasikia Mwalimu alimshauri asafiri kwa ndege toka Dodoma kwenda Dar, ushauri haukupewa uzito wowote. Pamoja na utaalam wote wa walinzi wetu, kilichotokea wote tunajua. Rais Samora wa Msumbiji wakati anatoka kwenye mkutano, nasikia kuwa alishauriwa kuwa ndege yake isipite kwenye anga la South Afrika, wana-usalama wake wakapuuza, kilichotokea sote tunajua.

Tunawashauri wana-usalama wa Rais wetu kuwa ni aheri kuchukua tahadhari zinazozidi kiasi kuliko kuchukua tahadhari pungufu. Tunamwombea Rais Magufuli, pamoja na ulinzi wa kibinadamu, Mungu amjalie ulinzi wa ziada, na daima awape hekima wale wote wanaosimamia usalama wake ili wapate kuyaona yote yahusuyo usalama wa Rais kabla ya kutokea.
Sifa kubwa ya MTU wa Usalama ni kuishi juu ya Hisia zake. MTU wa namna hii lazima awe na Visions.

Vision ni Mama wa Usalama. Mwl. NYERERE alikuwa mwana Usalama mzuri sana.

Kiufupi; Huwezi kuwa na sifa hizo kama wewe ni Malaya, mzinzi, mlevi, muongo, sio Mcha Mungu, etc
 
Unajua wakati mwingine ukiwaza shida TOO MUCH kwamba wewe ni mtu wa shida sana kuliko mataifa mengine shida nazo zitakufata sana sometimes its better to think abundantly hata angalau kwa safari ukatumia ndege ukapunguza risk za transport na waste of time., just thinking
 
Tanzania inachukua nafasi ya tatu kwa ulinzi wa Rais ikitanguliwa na Misri nafasi ya kwanza, South Africa nafasi ya pili hivyo ulinzi ni hakika. Hata hivyo kujiamini kupita kiasi inaweza kuwa ni mwanya wa adui kukumaliza.
hiyo umeitoa wapi leta ushahidi tukuumbuwe
 
Si anataka sifa hili watu waone anabana matumizi? Ila yote yanawezekana mchana kula ugari na nyanya chungu, (si wote tunaona?) usiku (tukilala) ukala wali kuku! Hapa kazi tu!
Una roho ya kwa nini na mawazo ya kimaskini
 
Kwa hiyo mtazamo wako unadhani, yeye Rais ameamua kutumia barabara hivi hivi tu bila kujiandaa na kuandaliwa?!

Unafikiri suala la kumlinda anajiamulia yeye!?

Naiamini system yetu ya usalama! Ukiona wameruhusu, jua wamejiandaa; Wanajua wanachokifanya.

Au movie za porini za akina Van Damme zinakupa mawazo hayo?!

Bachi! Mimi nichicheme mengi (In mmakonde's voice)!
Ni kupoteza muda wa kuwafanyia kazi watanzania.kwani akitumia ndege tatizo liko wapi?au ndo zile rumors kwamba ana aleji na ndege?
 
Tabia yako ya kusafiri kwa gari umbali mrefu hujui ni mbaya kiusalama?

Unawapa wakati mgumu sana walinzi wako kukulinda.Uwe unapokea na ushauri mheshimiwa Rais.

Hivi huko maporini mtu akijificha na Rocket-Propelled Grenade akakuvizia itakuwaje wakati unajua fika ukanda huo silaha kibao toka Congo zinapatikana.

Hujui pale unapopanga na mahasimu wako wanapanga pia?

Halafu pia kutumia masaa 6 barabarani wakati ungeweza kutumia saa 1, matano ukafanya kazi nyingine ni,jipu au uvivu.

Hivi mkuu nikuulize kidogo wewe na Mheshimiwa Magufuli nani anachungu wa maisha yake? hivi unadhani yeye ni mjinga wa kiasi unachofikiri kwani vita na watu kaanza baada ya kuwa Rais kumbuka alivyokuwa ujenzi ni watu wangapi walilia baada ya kuvunjiwa na wakajiapiza kuwa ataona hatimaye amekuwa Rais ulisha sikia hata gari yake imepata pancha kama ya mkwere ilivyokuwa inachomoka matairi ???? Sasa kwa taarifa yako amini Magufuli habahatishi kokote anakokwenda na kila analofanya ana uhakika nalo mimi sina hata chembe ya shaka juu yake wale walinzi ni kama kiungo tu kwenye mboga ila ulinzi ni wa Mungu ambao anao Magufuli. Keep in mind that No one can protect you than yourself.
 
Back
Top Bottom