Rais Magufuli unamuua mama yangu

Rais Magufuli unamuua mama yangu

Huyu mama umeambiwa kuwa ana zaidi ya miaka 25 kazini chini ya utendaji wake ni vijana wengi sana wamepata elimu kupitia kwake,si ajabu ukakuta wengine waliopata elimu chini ya huyu mama ni hawa hawa wanaowaita wenzao watumishi hewa au wanaweza wakawa ni ndugu zao au wanaweza wakawa ni watumishi katika serekali hihi ya kuwaita wenzao watumishi hewa,sasa je kama huyu mwalimu ana itwa mtumishi hewa na wale waliopata mafanikio kwa kupitia elimu yake waitwe akina nani?.

Twende mbele turudi nyuma.

Watu wanachanganya HEWA na KUGHUSHI CHETI. Kiuhalisia huyu mama anastahili kusamehewa na kulipwa mafao yake kwa utumishi wake wa miaka 25. Nitaeleza.
Huyu mama alitumia cheti cha shule cha marehemu shangazi wa mleta hoja. Hivo alisoma chuo akamaliza, akafaulu na kupangiwa kazi/shule ya kufundisha. Kwa maana ya HEWA huyu siyo MWALIMU HEWA!! Mwalimu hewa(ghost worker) ni yule asiyekuwepo kazini kwa maana ya jina lililoko kwenye Payroll lakini huyo mtumishi hayupo popote lakini kuna Afisa Utumishi, Mkurugenzi, Mhasibu au yeyote aliyetengeneza hilo jina anachukua huo mshahara!!!

Kwa kesi ya huyu mama alifaulu Chuo cha Waalimu na kafanya kazi kwa miaka yote zaidi ya 25. Je, ni wanafunzi wangapi wamepitia mikononi mwake?Bila shaka ni maelefu kwa maelfu wengine ni Waalimu,Madaktari, Wahandisi,Wahasibu n.k.
Hivo kumfukuza kazi mtu kama huyu ni Uonevu uliopitiliza na wa kinyama. Mbona kuna Watumishi wengi tu kwa ngazi za Uwaziri, u-RC, u-DC n.k huwa wanafanya makosa na kinachotokea Wanahamishwa sehemu ya kazi au Wanastaafishwa kwa Manufaa ya Umma lakini wanalipwa HAKI ZAO. Kwanini basi huyu mama naye kwa misingi hiyo hiyo akastaafishwa kwa manufaa ya Umma na akalipwa stahili zake ukizingatia kuwa bado mwaka 1 tu astaafu!!!

Tatizo la Viongozi wetu ni roho mbaya na kutopenda kusamehe. Wazungu huwa wanasema USITAKE KUMFANYIA MTU JAMBO AMBALO WEWE MWENYEWE HUTAKI UTENDEWE!!! Yaani watu wanaangalia kosa moja tu kati ya 100 mema aliyofanya mtu basi wana amua kuchukua hatua za kudhulumu mtu haki zake. Mbona kuna Mafisadi wamekomba MABILIONI ya Fedha za EPA,ESCROW, KAGODA n.k lakini mpaka leo wanatanua tu mitaani? Huyu maskini mwalimu na vimilioni vyake vya HELA YA MBOGA kama mara kumi hivi imekuwa nongwa!!!!Hebu tujaribu na kumwogopa Mungu sote tu binadamu.
 
Wapo watakaosema hekima itumike mana miaka yote hiyo tulikuwa wapi kuyaona haya au kujua kuwa anatumia vyeti ambavo sio vyake.

Hekima hizi hizi za kupindisha sheria ndio zinafanya tuwaite viongozi fulani wadhaifu,,,hekima hiz hizi ndio vizazi vijao vitatuhukumu tulikuwa wapi kuyatengua haya mabamu mana wakati huo digitali itawachuja wote.

Tushukuru Mungu tumempata Rais ambaye amethubutu kurekebisha makosa ya wasaidizi wake(waliokuwa wanajikinga na mwavuli wa hekima) na tuombe Mungu asitetereke na atakae kuja aaendeleze.

Ndugu zangu watanzania kama tunataka kweli kusonga mbele lazima tukubali mabadiliko na aliyeharibu bila kujali ni mtoto wa mkulima au mtoto wa kigogo au mwanasiasa ni lazima awajibishwe.
 
Watu wangapi miaka yote hiyo wamepata elimu duni toka kwa mtu ambae hana sifa? Sio ajabu kuna watu wamefeli mtihani na wanateseka kwa ajili ya udanganyifu wa huyu mama na nduguze wana ukoo.
Sawa unachosema lkn je na wale waliopass kwa kupitia kwa huyu mama unawaweka kundi gani?
 
Hii ni kweli jamani ni story imemkuta mama mdogo

Mamdogo ni mwalimu wa msingi na anatarajia kustaafu mwakani hivyo kwenye akili yake alishajiandaa kustaafu

Kitu ambacho hatukujua ni kuwa muda wote aliofanya kazi hakuwa akitumia cheti chake halisi( shangazi alifariki zaman sana hivyo ukoo ukakubaliana kumpa mama mdogo cheti cha shangazi akaingilia chuo cha ualimu miaka hiyo ya sabini na..
Mpk akaajiriwa)

Sasa kwa hesabu ya haraka mwakani anapaswa astaafu!! Ila ukaguzi huu wa Magufuli umemkumba

Mama anateseka presure inapanda asubuhi na jioni, vyeti vimehangaikiwa mpaka viapo vya kubadilisha jina ila wapi? Baraza wamekaba kooo!

Tunajua yawezekana ni kweli amekosea kutumia cheti cha mtu kazini lakini tutumie ubinadamu mama huyu kafanya kazi miaka zaidi ya 25 na alikuwa anategemea mafao yake karibia million 100 mwakani halaf leo hii ziyeyuke kirahisi hivi??

Rais Magufuli watu wa aina hii ya mama waonee huruma jamani mama atakufa hivi hivi tunamuona!
Watu rika ya mama yako mdogo ndo wanaoendelea kukiweka CCM madarakani kwa imani kwamba wapinzani hawana uzalendo.

Muache mama yako asome namba.
 
Wapo watakaosema hekima itumike mana miaka yote hiyo tulikuwa wapi kuyaona haya au kujua kuwa anatumia vyeti ambavo sio vyake.

Hekima hizi hizi za kupindisha sheria ndio zinafanya tuwaite viongozi fulani wadhaifu,,,hekima hiz hizi ndio vizazi vijao vitatuhukumu tulikuwa wapi kuyatengua haya mabamu mana wakati huo digitali itawachuja wote.

Tushukuru Mungu tumempata Rais ambaye amethubutu kurekebisha makosa ya wasaidizi wake(waliokuwa wanajikinga na mwavuli wa hekima) na tuombe Mungu asitetereke na atakae kuja aaendeleze.

Ndugu zangu watanzania kama tunataka kweli kusonga mbele lazima tukubali mabadiliko na aliyeharibu bila kujali ni mtoto wa mkulima au mtoto wa kigogo au mwanasiasa ni lazima awajibishwe.
Mbona hayo tunayaona kwa wanyonge tu?
Wapi Benjamini mkapa alijimilikisha mgodi yeye na familia YAKE?
Yupo mwiguru nchemba hadi Leo anatumia jina LA MTU mwingine?
Yupo Paul makonda nae anatumia jina si lake hadi sasa.
Sasa tunajiuliza hizi action ni kwa wanyonge tu wasiokua na uhusiano wa kisiasa na mkuru peke yao?
 
Makoye;

Tunaposema hewa tunajumuisha wote wasio kazini na makoye muajiriwa wa bot lakina anatumia cheti cha mshana jr,,,hao wote wametenda kosa na wamewanyima haki ya kupata ajira wale wanaostahili.

Kusoma chuo na kufaulu isiwe shida,tufuate taratibu; leo ni sababu hiyo lakini kesho anafanya kosa la jinai anapelekwa mahakamani anakana jina anasema yeye sio mshana jr yeye ni makoye.

Leo hii watu wana vyeti vyeki vya ndoa ili serikali iwape stahiki za muajiriwa mwenye ndoa, tunapoacha kuwachukulia hatua watu wa aina hii ndio hao tukiwapa madaraka wanapokea mishahara ya wafanyakazi zaidi ya mmoja mana akili zao zinawaza kugushi vitu.
 
Hii ni kweli jamani ni story imemkuta mama mdogo

Mamdogo ni mwalimu wa msingi na anatarajia kustaafu mwakani hivyo kwenye akili yake alishajiandaa kustaafu

Kitu ambacho hatukujua ni kuwa muda wote aliofanya kazi hakuwa akitumia cheti chake halisi( shangazi alifariki zaman sana hivyo ukoo ukakubaliana kumpa mama mdogo cheti cha shangazi akaingilia chuo cha ualimu miaka hiyo ya sabini na..
Mpk akaajiriwa)

Sasa kwa hesabu ya haraka mwakani anapaswa astaafu!! Ila ukaguzi huu wa Magufuli umemkumba

Mama anateseka presure inapanda asubuhi na jioni, vyeti vimehangaikiwa mpaka viapo vya kubadilisha jina ila wapi? Baraza wamekaba kooo!

Tunajua yawezekana ni kweli amekosea kutumia cheti cha mtu kazini lakini tutumie ubinadamu mama huyu kafanya kazi miaka zaidi ya 25 na alikuwa anategemea mafao yake karibia million 100 mwakani halaf leo hii ziyeyuke kirahisi hivi??

Rais Magufuli watu wa aina hii ya mama waonee huruma jamani mama atakufa hivi hivi tunamuona!
He!!! Anamuuaje? Kwanini alitumia cheti cha mtu aliyekufa? Hilo ni kosa kubwa sana sana. Kutumia cheti cha mtu mwingine ni kosa la jinai. Kwanza wana bahati hawafunguliwi makosa ya jinai.
 
Yaani unajiendeleza kwa kutumia cheti cha mtu,na anakibali cha kufanya hivyo,naomba kujua sheria za kipindi hicho zilikuwaje maana kichwa hapo kimekuwa hewa.
 
inatia simanzi/huzuni lakini kwenye sheria tukianza kuangalia zaidi athari ya zoezi la uhakiki wa watumishi hewa na wasio na sifa kwa mtu mmoja mmoja tutaharibu maana ya zoezi zima.
 
Inaleta majonzi sana, wamsaidie astaafu kwa amani jamani. Kaz ya ualimu siyo mchezo then mwishoni unyimwe mafao yako, so sad
hajanyimwa mafao yake,wewe unaingiza mada nyingine...yeye kavunja sheria na sheria inamhukumu lakini angefuata sheria mafao yake yapo pale pale.
 
Bhebe mami, Mimi nasema si sawa kwa mtu uliyetumikia nchi miaka 30 au zaidi ukaambiwa wewe ni hewa. Haya mambo yalikuwepo kwa sababu na system iliruhusu labda na udhaifu wa uhakiki uliokuwepo kipindi hicho.

Umezungumzia kurudia shule hii nayo haikuwezekana kwa majina yako halisi. Ilibidi upate mtoro na kuendeleza jina na namba yake. kumbuka kisa cha akina Mwigulu na hata walipofika 0 leval waliruhusiwa kubadili majina mahakamani.

Anyway pamoja na kasoro zake kulitumikia taifa kwa miaka 30 au zaidi halafu uitwe hewa si sawa. Wapo wengi kwenye majeshi yetu, waalimu wetu, viongozi wetu n.k.
mkuu huyu si hewa ila ni mtumishi asiye na sifa.
 
Mbona hayo tunayaona kwa wanyonge tu?
Wapi Benjamini mkapa alijimilikisha mgodi yeye na familia YAKE?
Yupo mwiguru nchemba hadi Leo anatumia jina LA MTU mwingine?
Yupo Paul makonda nae anatumia jina si lake hadi sasa.
Sasa tunajiuliza hizi action ni kwa wanyonge tu wasiokua na uhusiano wa kisiasa na mkuru peke yao?

Suala la Marais waliopita ni la kikatiba sitaliongelea;

Ila kama kuna viongozi wengine au wafanyakazi wengine wa juu serikalini ambayo wanatumia vyeti bandia/majina ambayo sio yao na ushaidi ipo usiokuwa na shaka, kuna njia nyingi ambazo zitafanya nao panga hili liwapitie.

1; Kusanya ushahidi wako peleka mahakamani(unayohaki ya kumfungulia mashitaka mana analipwa mshahara kwa kodi yako)

2; Tumia vyombo vya habari ila uwe tayari kutoa ushahidi pindi itakavyohitajika

3; Tumia mitandao ya kijamii,ila ijiweke wazi ili upatikane pindi ushahidi utakapohitajika.

Ukifanya hayo hao watu unaowahisi watachunguzwa na vyombo husika na kuchukuliwa hatua
 
ndugu yangu hapo unachojaribu kukisema ni tutumie ubinadamu na tuweke pembeni sheria,mpaka lini tutaendelea kuchukuliana na kubebana hivi???mbona kama unajaribu kuturudisha kulekule enzi za rais msataafu maana yeye alikua anawachukulia watu na kuwabeba watu lakini bado hatukumuona anafaa na watu wakawa wanafanya watakavyo...inabidi tubadilike hakuna kumwangalia mtu usoni wa kumuonea soni mtu,umevunja sheria twende na maji tu hakuna namna muda wa kuconsider wewe ni nani umekaa muda gani haupo kwa sasa.hapa tuna mzungumzia huyu mama lakini ukae ujue wapo wa aina hii wengi tuu huko maofisini tena ofisi nyeti nao tuwachukulie kama wewe unvosuggest??
 
Back
Top Bottom