Rais Magufuli, ukiwa unatoka Chato pitia Hospitali ya Mlonganzila iliyobatizwa Vingunguti

Kazi ya daktari sio kuzuia kifo. Kazi yake ni kutibu, whether mgonjwa atapona au laa ilo analijua Mungu aliyetupa uhai. Suala la vifo 11 Mloganzila kwa usiku mmoja sio ajabu sana. Naamini hata ukienda MNH ukachukua records za siku nzima ya jana kwa idara zote utakuta vifo zaidi ya kumi na moja. Suala la mgonjwa wako kufa, pole kwanza kwa kufiwa. Lakini ungeuliza zaidi kuhusu sababu ya kifo. Si kweli kwamba ajali ya mguu haiwezi kumuua mtuu. Unajua average blood loss of a femur? Inaeza muua mtu hasa kama alichelewa kupata blood replacement.
Wewe utakuwa ni mfanyakazi wa hapo Mloganzila palalamikiwa, umejitahidi kuwatetea lakini kubali ukatae hapo Hospt kwenu kumejaa uzembe na makusudi nyingi ikiwemo kuwatumia madaktari wanafunzi ambao wengi bado kujua udaktari vizuri, kwa kweli Hiyo Hospt ina mapungufu yake tena mengi sana lazima magufuli afanye ziara ya kushitukiza
 
Pale wanafunzi ni wengi ndio sehemu yao yakufanyia majaribio ya kumpasua mtu, ukipeleka nduguyo aliezidiwa pale wakiona hanasiku nyingi watampasua pasua ili kufanya testing zao..chukueni hiiii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siasa za kujimwambafy kwa uongozi wa awamu hii, ndio imepelekea yote haya pale Mloganzila. Nje ya hapo awamu iliyopita ilikuwa na malengo mazuri sana ya kuifanya ile hospital kuwa bora na ya kisasa ukanda wa maziwa makuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boss USSR Pole sana Mkuu kwa kadhia uliyopata.

Nakumbuka hata Utawala wa JK kuna Kashfa iliwahigi kutoka kuhusu Hospitali hii.

Mimi binafsi nashangaa, pamoja na Ukali wa Mh. Rais lakini Viongozi na Watumishi ni vichwa ngumu, Ufisadi ndio kwa kwenda mbele, madudu kila kona. Sijui ndio wanamkomoa au ndio wamekata tamaa na maisha.
 
..inawezekana alifaulu vizuri form 4 ndiyo maana akafika Ihungo high school.

..nimeshuhudia mtu amepata 1 form 4. Then O form 6. Akaenda kusomea medical assistant, sasa hivi ana PhD ya medicine.

..kufeli form 4 au 6 haimaanishi kwamba mhusika atashindwa maisha.
Zamani watu walikuwa wanaendelea na div four wakitegemea ku resit au kusakafia baadhi ya masomo ili waweze kufanya mtihani was form six .
Hivyo kuendelea kwake form five hapo ihungo hakuna maana kwamba alifaulu four.
Kuhusu ku feli au kufanikiwa maisha hakuhusiani na shule wapo watu wengi waliofanikiwa bila shule. Kwa juhudi zao na wengine kwa kuachiwa
 
Zamani watu walikuwa wanaendelea na div four wakitegemea ku resit au kusakafia baadhi ya masomo ili waweze kufanya mtihani was form six .
Hivyo kuendelea kwake form five hapo ihungo hakuna maana kwamba alifaulu four.
Kuhusu ku feli au kufanikiwa maisha hakuhusiani na shule wapo watu wengi waliofanikiwa bila shule. Kwa juhudi zao na wengine kwa kuachiwa

..siyo kweli.

..Div 4 ilikuwa huwezi kuendelea na A-level ktk shule za serikali.

..labda wakupeleke polisi au jeshini.
 
Hii habari sio kweli, nawewe ni mpiga dili na unashirikiana na mabeberu kutaka kuichafua nchi yetu, tunaelekea uchumi wa kati, masuala ya afya yapo vizuri, tumejenga vituo vya afya kila kata na tumeajiri wataalamu wa kutosha, we are on the right track, tutembee kifua mbele..


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole na msiba hila ukisoma malalamiko yako kitu ambacho umeona sio tatizo ‘Human Resources’ ndio moja ya msingi wa tatizo kutokana na maelezo ukiyafanyia evaluation.

Watu washapiga kelele sana kuhusu hiyo wizara kuanzia waziri, katibu mkuu na wataalamu wote ni clueless when it comes to health service delivery, managing outcome and quality of services.

Kuna mambo mengi sana yanaepukika kisera tu na mikakati thubuti ya usimamizi.

Huo tu ulikuwa mtihani tosha bado tena kilaza kama Ummy Mwalimu umpe na nyongeza ya ulinzi wa wazee na watoto; watachinjwa tu, kujazwa mimba na kulawitiwa kirahisi (sisemi kwamba anauwezo kuzuia binadamu kufanya matendo ya uovu) lakini hakuna jitihada zozote za supervision to deter people from commiting such acts.

Halafu sasa Magu anavyowasifia kwa utendaji wakati ukiwasikia tu waziri na naibu wake unaona kabisa the two of them know nothing about health and social care management.

Mambo wanayozuungumza sivyo kabisa wenzetu wanavyo approach na sio kwamba wana akili sana kwa sababu over 90% ya muongozo wa kisera za afya na maswala ya jamii source zake ni WHO directives ambazo kila nchi inapewa wao wanafanya implementations sahihi kwa sababu wana watu waliosomea management ya afya na kuweza kusimamia utekelezaji wake kwa viwango vinavyolengwa kufikiwa kwenye kutoa huduma.
 
Chadema wanasemaje?
Kwa mujibu wa ccm Chadema sio wazalendo, Wale madaktari wengi wamesomea udaktari chuo cha Chadema

Kwanini hukumpeleka ndugu yako kwenye hospital ya CCM?

Wewe ni mpumbavu kabisa, Mwana ccm usiyejitambua na mpuuzi, Peleka ndugu zako kwenye hospital za ccm watapona

Achana na hiyo hospital ya Chadema
Kwanza nikupongeze kwa kuweza kuifanya hospitali hii kuwa na hadhi ya kimataifa in terms of infrastructure and human resources ila nikutaarifu tu kuwa wananchi wamepabatiza jina kuwa VINGUNGUTI yaani ni kama machinjio ya mifugo kule vingunguti inaima!

Ni kweli kuwa hospital ya Mlonganzila inapokea wangonjwa walioshindikana katika hospitali nyingine hapa nchini kwa maana ya rufaa ila hapa ni zaidi ya graveyards, mtu kutoka hai/kupona ni nadra sana.

Nikuombe tu pitia pale labda kuna vitu sisi wageni /wapitaji hatujui ila wewe unaweza kupata ukweli

NILICHOSHUHUDIA

Nilikwenda kumwongezea damu kaka yangu nikiwa katika foleni nikaambiwa niende ofisi za juu nichukue form; nikapanda lift hadi eneo husika huko nikakuta madaktari (wako bize na simu na story za simba na yanga wakiume walikuwa kama 4 hivi upande wa pili wa kike walikuwa kama 5 hivi) wote vi vijana wa mjini mjini hivi na viduku kibao. Nikaambiwa anayetoa form hayupo nisubiri mimi na wenzangu tukaelekezwa bench tukae tukiwa hapo akaja mama mtu mzima akawaita wale madaktari wakawa kama na kikao kidogo wakiwa wamesimama yule mama akaanza kusema tena kwa sauti akiwakaripia wale vijana kwa uzembe na kusema deaths zimezidi yaani usiku mmoja wamekufa watu wote wale watu kumi na mmoja sio normal. Wakati anafoka daktari mmoja akajibu kuwa ni kweli uzembe umezidi wakaanza kurushiana maneno huku sisi tukishangaa. Akawa anawaonya kuhusu kutoroka na kwenda mtaani usiku na kuwaachia wagonjwa manesi. Inauma hii ni live nasikia tena kutoka kwa madk wenyewe.

Baadae akaja nurse akatuita akatupa form, ndugu yangu alikuwa amepata ajali ya mguu hivyo sikuwa na hofu sana na alikuwa amekaa pale siku tano akifanyiwa stretching maana aliumia kifundo cha mguu ila cha kusikitisha alivyoingia chumba cha upasuaji hakutoka mzima. Inauma sana hii, mguu hadi kifo vipi ingekuwa moyo, kichwa au uzazi!

Usiombe kufika pale, usikubali kulazwa pale, Mlonganzila ni zaidi ya Mwananzila! Mh Rais pale kuna majipu sio mchezo kila mtu analia heri ubaki Mwananyamala, Temeke au Muhimbili sio Mlonganzila. Vijana wanajifunzia udaktari kwenye miili ya wapendwa wetu.

USSR

====

Soma pia:
Haya yanayosemwa kuhusu Hospitali ya Mloganzila ni kweli?
na
Mloganzila yakanusha juu ya taarifa za vifo vya wagonjwa
 
Sasa tukusaidie kitu gani wewe mwana ccm

Ulitaka afe nani?
They don't care mkuu wako na utoto mwingi nikikumbuka yule Dada anawaonesha madk wenzake picha kwenye simu eti yule mchepuko alipigwa chini na jamaa huyu hapa ,wote wakarundikana kungalia picha na story zikaanzia hapo sisi tupo kwenye mstari tunasubili wao wanaoneshana picha za michepuko ,wapuuzi sana hata ndugu yangu kafa kwa uzembe tu

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kama ndugu yako amekufa hapo kwenye hospital ya Chadema

Kwanini msingempeleka ulaya na wewe ni mwana ccm

Huo ni upumbavu kwenda hospital ya Chadema mlongazila
Nikisema mnyika amelitelekeza jimbo la kibamba amejipa ubunge wa taifa kama zzk mbunge wa kigoma mjini yupo mabibo sokoni,kkoo,temeke na mbagala anakusanya kero za wafanyabiashara wakati ujiji masoko kibao na hawajawahi kumuona

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom