Rais Magufuli, ukiwa unatoka Chato pitia Hospitali ya Mlonganzila iliyobatizwa Vingunguti

Wewe utakuwa mpiga dili au CDM mawakala wa mabeberu nyie, mnataka kuichonganisha Serikali na Wananchi..Watu kama nyie ndio mnamkatisha tamaa Rais wetu kipenzi..

Awamu ya tano chini ya Jemedari Dr JPM haiwezi kuwa na uzembe wa hivyo, nidhamu kwa sasa imerudi makazini, watu wanawahi makazini na wanapiga kazi kama mchwa, heko awamu ya tano, heko Rais wetu kipenzi Dr JPM..
 
Aisee ni hatari pole mkuu.Hospital za serikali ni majanga sana madaktari hawana kabisa weledi na hii ni kwa hospital zote usipokua na fedha utakufa huku unajiona.

Mtag Mayalla au Polepole ujumbe ufike kwa haraka mkuu.
 
Wewe utakuwa mpiga dili au CDM mawakala wa mabeberu nyie, mnataka kuichonganisha Serikali na Wananchi..Watu kama nyie ndio mnamkatisha tamaa Rais wetu kipenzi..

Awamu ya tano chini ya Jemedari Dr JPM haiwezi kuwa na uzembe wa hivyo, nidhamu kwa sasa imerudi makazini, watu wanawahi makazini na wanapiga kazi kama mchwa, heko awamu ya tano, heko Rais wetu kipenzi Dr JPM..
Dah! acha utani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wewe!
Hujitambui kiasi hiki?
Mimi nilichukua majeruhi eneo la ajali, jambo la kwanza nilipiga simu polisi kuwa naleta majeruhi waandae pf3, nilipofika niliwapelekesha na dk 3 maelezo tayari nikaelekea hosp ya Mount Meru.
Sikuamini macho yangu
Wauguzi na madaktari
Hawajali, naomba kitanda cha kubebea mgonjwa hakuna anayejigusa.
Nilipiga kelele vibaya mno wakatawanyika
Kutafta kitanda cha kubebea, ghafla kila mmoja aksja na kitanda chake.
Baada ya majeruhi kuingizwa akawa anaangaliwa tu hakuna huduma za dharura hadi nilipie.
Nikaenda kufuata taratibu zote na kulipa.
Akapewa kitanda lkn hakuna cha huduma.
Niliingia kwa daktari kwa mkwara mzito...yaani ghafla walijaa kumshughulikia majeruhi...waliniogopa balaa..
Wakawa wanasema huyu ni polisi na kila mtu akawa ananihofu lkn nilifurahi majeruhi alihudumiwa na baada ya siku 3 akaruhusiwa.

Tuwandekeza sana hawa...
Hivi ulinyamaza je mnawekwa bila huduma na mijitu inacheza cheza hapo?
Ungemkaba mmoja na kumtishia kumpiga na wananchi wangekusapoti.
They don't care mkuu wako na utoto mwingi nikikumbuka yule Dada anawaonesha madk wenzake picha kwenye simu eti yule mchepuko alipigwa chini na jamaa huyu hapa ,wote wakarundikana kungalia picha na story zikaanzia hapo sisi tupo kwenye mstari tunasubili wao wanaoneshana picha za michepuko ,wapuuzi sana hata ndugu yangu kafa kwa uzembe tu

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali iweke hotline kila wizara kuripoti madudu.Mzaha kwa afya za watu ni mbaya zaidi ukizingatia wanavitendea kazi na miundombinu ya kutosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo wakati mwingine ni uelewa mdogo walionao hao tunao waita madaktari. Siku hizi kila kitu Tanzania ni siasa hata madaktari wengi wanaomaliza mafunzo yao zama hizi ni tofali tu wamefyatuliwa hivyo huko mahospitalini ni tia maji, tia maji.

Hakuna kitu kinaleta stresses kama kufanya kazi usiyoielewa vizuri hasa ikiwa ni kama hiyo ya kutibu watu. Na kuiacha uwezi maana msharahara unautaka, mwisho wa siku unaishia kwenda na kupiga soga tu mpaka muda wa kazi ukiisha unarudi zako nyumbani!

Shida ya mlonganzila hasa ni hii madaktari wazuri hawataki kwenda, wako muhimbili, kule mlonganzila wengi ni internships na wale wapya wapya ambao mbaali na uelewa mdogo walionao hata uzoefu hawana.

Lakini pia hiyo hulka ya kutofanya kazi ni asili ya watanzania karibu wote, sasa usitegemee eti kwa kuwa ni daktari basi atakuwa na asili tofauti na mkata vitamburisho kule nida au mtoa international passports kule uhamiaji au tofauti na mwalimu wa shule asiyefundisha. Watz ni wale wale uzembe kwa kwenda mbele haijalishi hata kama ni daktari.
 
Mh Ummy Mwalimu ni dawa yao tosha. Atawatokea Kama juice ya pili pili. Vuta pumzi atatuahapo manne asubuhi na mapema
 
Tutawalaumu madaktari bure lakini ukiingia kiundani unadhani kwa nini hawafanyi hivyo hospital za binafsi? Mishahara yao ni sh. Ngapi? Tangu lini hawajaongezwa mishahara, watapata wapi motivation?

Wengine hapo walikuwa ni Clinical officers wakaenda jiendeleza kwa level za degree wamerudi scale za mishahara zipo pale pale na mkuu hana nia ya kuongeza, wakidai watajikuta lupango kwa makosa ya utakatishaji fedha Sasa nani ajitume happy?

Na sisi wananchi tunawapigia makofi daily wanasiasa. Tusifu na kuabudu ila tujue na matokeo yake.
 
..halafu NDUGAI alikuwa anasisitiza LISSU atibiwe hapa nchini.

..nakwambia yule angekufa kwa tatizo dogo sana na siyo majeraha aliyoyapata.

..kati ya maamuzi ya busara kabisa ya Mh.Mbowe, pamoja na zero aliyopata form 6, ni kumuwahisha Lissu Nairobi.

..MUNGU pia ambariki Dr.Mpoki aliyesisitiza kuwa Lissu apelekwe Nairobi na siyo Muhimbili.

Cc tindo
 
Sometimes Zero=Hero
..halafu NDUGAI alikuwa anasisitiza LISSU atibiwe hapa nchini.

..nakwambia yule angekufa kwa tatizo dogo sana na siyo majeraha aliyoyapata.

..kati ya maamuzi ya busara kabisa ya Mh.Mbowe, pamoja na zero aliyopata form 6, ni kumuwahisha Lissu Nairobi.

..MUNGU pia ambariki Dr.Mpoki aliyesisitiza kuwa Lissu apelekwe Nairobi na siyo Muhimbili.

Cc tindo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watumishi hawana morali hawana nyongeza za mishahara,vyeo,nk ndo umuharibia anaweza akawa na nia njema akajikuta ngoma anacheza mwenyewe wengine kuwa wapenzi Wa tazamaji.Awaboreshee watumishi hali zao nao wataongeza tija,asikamue ng'ombe bila kuwalisha
 
Hii hospital haifai, nishapoteza jamaa wawili kwa nyakati tofauti kwa uzembe Wa wazi kabisa!
Yaani ukuiona Ndugu yako amepewa rufaa pale omba sana vinginevyo kifo kiko mlangoni!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom