Rais Magufuli, ukiwa unatoka Chato pitia Hospitali ya Mlonganzila iliyobatizwa Vingunguti

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,664
Kwanza nikupongeze kwa kuweza kuifanya hospitali hii kuwa na hadhi ya kimataifa in terms of infrastructure and human resources ila nikutaarifu tu kuwa wananchi wamepabatiza jina kuwa VINGUNGUTI yaani ni kama machinjio ya mifugo kule vingunguti inaima!

Ni kweli kuwa hospital ya Mlonganzila inapokea wangonjwa walioshindikana katika hospitali nyingine hapa nchini kwa maana ya rufaa ila hapa ni zaidi ya graveyards, mtu kutoka hai/kupona ni nadra sana.

Nikuombe tu pitia pale labda kuna vitu sisi wageni /wapitaji hatujui ila wewe unaweza kupata ukweli

NILICHOSHUHUDIA

Nilikwenda kumwongezea damu kaka yangu nikiwa katika foleni nikaambiwa niende ofisi za juu nichukue form; nikapanda lift hadi eneo husika huko nikakuta madaktari (wako bize na simu na story za simba na yanga wakiume walikuwa kama 4 hivi upande wa pili wa kike walikuwa kama 5 hivi) wote vi vijana wa mjini mjini hivi na viduku kibao. Nikaambiwa anayetoa form hayupo nisubiri mimi na wenzangu tukaelekezwa bench tukae tukiwa hapo akaja mama mtu mzima akawaita wale madaktari wakawa kama na kikao kidogo wakiwa wamesimama yule mama akaanza kusema tena kwa sauti akiwakaripia wale vijana kwa uzembe na kusema deaths zimezidi yaani usiku mmoja wamekufa watu wote wale watu kumi na mmoja sio normal. Wakati anafoka daktari mmoja akajibu kuwa ni kweli uzembe umezidi wakaanza kurushiana maneno huku sisi tukishangaa. Akawa anawaonya kuhusu kutoroka na kwenda mtaani usiku na kuwaachia wagonjwa manesi. Inauma hii ni live nasikia tena kutoka kwa madk wenyewe.

Baadae akaja nurse akatuita akatupa form, ndugu yangu alikuwa amepata ajali ya mguu hivyo sikuwa na hofu sana na alikuwa amekaa pale siku tano akifanyiwa stretching maana aliumia kifundo cha mguu ila cha kusikitisha alivyoingia chumba cha upasuaji hakutoka mzima. Inauma sana hii, mguu hadi kifo vipi ingekuwa moyo, kichwa au uzazi!

Usiombe kufika pale, usikubali kulazwa pale, Mlonganzila ni zaidi ya Mwananzila! Mh Rais pale kuna majipu sio mchezo kila mtu analia heri ubaki Mwananyamala, Temeke au Muhimbili sio Mlonganzila. Vijana wanajifunzia udaktari kwenye miili ya wapendwa wetu.

USSR

====

Soma pia:
Haya yanayosemwa kuhusu Hospitali ya Mloganzila ni kweli?
na
Mloganzila yakanusha juu ya taarifa za vifo vya wagonjwa
 
Hi hospital ni janga la taifa, kuna ndugu yangu nae aliondoka kimasihara masihara tu. Ummy Mwalimu sijui kama anajua kinachoendelea pale

Sent using Jamii Forums mobile app
They don't care mkuu wako na utoto mwingi nikikumbuka yule Dada anawaonesha madk wenzake picha kwenye simu eti yule mchepuko alipigwa chini na jamaa huyu hapa ,wote wakarundikana kungalia picha na story zikaanzia hapo sisi tupo kwenye mstari tunasubili wao wanaoneshana picha za michepuko ,wapuuzi sana hata ndugu yangu kafa kwa uzembe tu

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
They don't care mkuu wako na utoto mwingi nikikumbuka yule Dada anawaonesha madk wenzake picha kwenye simu eti yule mchepuko alipigwa chini na jamaa huyu hapa ,wote wakarundikana kungalia picha na story zikaanzia hapo sisi tupo kwenye mstari tunasubili wao wanaoneshana picha za michepuko ,wapuuzi sana hata ndugu yangu kafa kwa uzembe tu

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Nadhani wanasahau viapo vyao wakiwa wanakufa kwa njaa huko vyuoni kwao
 
Mh Mnyika wiki ilyopita baada ya kuonana na wasela alivyosema kuhusu hiyo bucha wewe USSR ulisemaje
Nikisema mnyika amelitelekeza jimbo la kibamba amejipa ubunge wa taifa kama zzk mbunge wa kigoma mjini yupo mabibo sokoni,kkoo,temeke na mbagala anakusanya kero za wafanyabiashara wakati ujiji masoko kibao na hawajawahi kumuona

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom